Shirikisho la soka Tanzania TFF, limesema litawatia nguvuni kwa mujibu wa sheria na taratibu mashabiki watakaoikashifu serikali ama uongozi wa shirikisho hilo kwa kuingia na mabango uwanjani yenye jumbe tofauti hapo kesho katika mchezo wa kimataifa wa klabu bingwa Afrika kati ya wenyeji Yanga dhidi ya Ngaya ya nchini Comoro.