TFDA yakamata kiwanda bubu cha kutengeneza vipodozi Arusha

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
Mamlaka ya chakula na dawa kanda ya kaskazini kwa kushirikiana na jeshi la polisi wamembaini na kufanikiwa kumkamata mfanyabiashara mmoja jijini Arusha anayemiliki kiwanda bubu kinachotengeneza vipodozi bila usajili wa TFDA pamoja na shehena ya zaidi ya tani saba ya vipodozi mbalimbali vikiwemo vile vilivyopigwa marufuku vikiwa vimehifadhiwa kwenye ghala lisilokidhi viwango.

Akizungumza na ITV katika eneo la tukio mtaa wa Sakina mkuu wa operesheni wa TFDA Benson Mcheza anasema wamefanikisha zoezi hilo baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema na kwamba mtuhumiwa atachukuliwa hatua za kisheria na kulipia gharama zote za kuteketeza bidhaa hizo.

Kwa upande wake mfanyabiashara anayemiliki kiwanda hicho Chalo Makala amesema bidhaa zilizoko kwenye ghala ni bidhaa za dukani kwake ambazo amelipia kodi zote stahiki na kwamba zile anazozalisha zilikua kwenye majaribio.

Kwa upande wa uongozi wa kata ya Kiranyi kilipo kiwanda hicho wakatoa wito kwa jamii kutoa taarifa mapema pale wanapobaini uendeshaji wa biashara yoyote kinyume cha sheria ili kuepusha madhara kwa watumiaji lakini pia kuziba mianya ya ukwepaji kodi.
Ca2yNUiWwAAeIke.jpg
Ca2yMLZWAAAU30e.jpg
Ca2yNq4XEAA_6nV.jpg

Chanzo: ITV
 
Natafuta mpenzi aninunulie queen Elizabeth lotion elf 90 hizi feki zitatuua jamani
Valentine ndo hiyo
 
Jamaa hakuonyesha ushirikiano kwa TFDA ndio maana kalipuliwa. Viwanda kama hivyo vipo vingapi nchini?
 
Back
Top Bottom