TFDA yakamata dawa bandia, yatahadharisha wanachi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,861
30,278
DAWA BANDIA aina tano zilizoingizwa nchini kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa Malaria zimekamatwa

Dawa hizo zimekamatwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) kwa kugundulika kuwa ni dawa bandia na hazijasajiliwa

Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo, alisema kuwa, dawa hizo zilikamatwa kufuatia ukaguzi uliofanywa na mamlaka hiyo katika maeneo 390 ya kuuzia dawa na kutolea huduma za afya yaliyopo katika mikoa 13 nchini.

Alisema ukaguzi ambao ulifanyika kuanzia Agosti 21 hadi Septemba 8, mwaka huu, ulilenga kubaini ubora na usalama wa dawa zilizopo katika soko na kuchukua hatua stahiki.

Mikoa iliyofanyiwa ukaguzi huo Dar es Salaam, Kigoma, Ruvuma, Dodoma, Mwanza, Mtwara, Lindi, Morogoro, Mbeya, Kagera, Manyara, Pwani naTanga.

Alisema dawa hizo ziliisha muda wa matumizi na kukosekana harufu ya penicillin inayotakwia iwepo kwenye vidonge

Mamlaka hiyo imewataka wananchi kuwa makini na ununuzi wa dawa kuepuka madhara yanayoweza kutokea kutokana na matumizi ya dawa zisizokidhi ubora na usalama.

Dawa bandia zilizokamatwa ni za aina ya Artemether + Lumefantrine (ALU) yenye jina la biashara “Coartem”, dawa ya kutuliza maumivu ya Ibuprofen, ambayo inauzwa kama Erythromycin Stearate BP 250mg; Penizin-V; Elphedrin, Elphedren na Laifin (Sulphamethoxazole + Pyrimethamine) zote zikiwa katika mfumo wa vidonge.

Chanzo: Nifahamishe.comaya ndugu zangu tujihadhari na Madawa Feki.
 

jamii01

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
1,956
1,342
Tanzania bwana watu wamekuwa wazembe wamebaki watu wakupga maneno sana..unaachaje dawa mpaka zinaingia sokoni then unasema dawa hizi ni feki na kama ni feki lazima zitakuwa effect..Hawa watu wa TFDA lazima wawajibishwe na TRA na TPA pale bandarini zinapoingilia na kupewa kibari cha kuingia nchini.ndiyo yale yale ya Vitunguu kutoka china..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom