Tetesi za usajili wa Rice, Aguero, Mbappe, Vazquez, Haaland, Dembele, Coutinho

Emmanuel Kasomi

Verified Member
Sep 3, 2014
4,107
2,000
Manchester United watatathmini uwezekano wa kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza Declan Rice, 22, katika mkataba wowote kati yao na West Ham utakaomhusisha Jesse Lingard, 28. (Athletic - subscription required)

Leeds United wamejiunga na kinyang'anyiro cha kumsaini mshambuliaji wa Manchester City na Argentina Sergio Aguero, 32, mkataba wake utakapokamilika mwisho wa msimu huu. (90min)

Hatima ya mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe katika klabu ya Paris St-Germain haijulikani baada ya nyota huyo aliye na umbri wa miaka 22- kukataa kusaini mkataba mpya. (Telegraph - subscription required)
Mbappe hatasaini mkataba mpya PSG kwasababu anataka kujiunga na Real Madrid. (Cuatro - in Spanish)

Real Madrid wanajiandaa kumtumia mshambuliaji wa Brazil Vinicius Junior, 20, katika mkataba wa kumsaini Mbappe msimu huu wa joto. (El Chiringuito, via Metro)

Winga wa Real aliye na umri wa miaka 29- Mhispania Lucas Vazquez, ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu, hajaamua kuhamia Bernabeu licha ya Manchester United na Chelsea kuonesha nia ya kutaka kumnunua. (Sun)

Chelsea inapania kuwasajili washambuliaji Erling Braut Haaland, 20, wa Borussia Dortmund na Aguero wa Manchester City msimu huu wa joto. (90min)
Lyon wameweka euro milioni 25 kama bei ya awali ya mchezaji wa Uswidi wa safu ya kati na nyuma Joachim Andersen, 24, ambaye yuko Fulham kwa mkopo. Manchester United na Tottenham pia zinamnyatia. (Metro)

Winga wa Japan Takumi Minamino, 26, anasema "alishangazwa" na uamuzi wa Liverpool kumtoa kwa mkopo kwenda Southampton mwezi Januari. (Independent)

Saints wanajadiliana kurefusha mkataba wa mshambuliaji wa Uingereza Theo Walcott katika uwanja wa St Mary's. Mchezaji huyo mwenye miaka 32- kwa sasa yuko kwa mkopo wa msimu mzima Everton. (Southern Echo)
Liverpool wamemchagua kiungo wa kati wa AZ Alkmaar Mholanzi Teun Koopmeiners,23, kujaza pengo litakaloachwa na Georginio Wijnaldum, 30. (AS - in Spanish)

Mkufunzi wa Brighton Graham Potter ana mpango wa kurefusha mkataba wa mshambuliaji wa Uingereza Danny Welbeck katika klabu hiyo, lakini mazungumzo hayo hayatafanyika hadi mwisho wa msimu wa huu wa joto. Mkataba wa Welbeck aliye na umri wa miaka 30- unakamilika mwezi Juni. (Sky Sports)

Kiungo wa kati wa Chelsea na Italia Jorginho 29, anasema angelipendelea kurejea katika klabu yake ya zamani ya Napoli kabla ya kukamilisha taaluma yake. (Sky Sport Italia)

Mshambuliaji wa Ufaransa Ousmane Dembele, 23, atasaini mkataba mpya Barcelona. (Marca - in Spanish)

Kiungo wa kati wa zamani wa Liverpool na mchezaji wa kimataifa wa Brazil Philippe Coutinho, 28, ni miongoni mwa wachezaji tisa watakaouzwa na Barcelona msimu huu wa joto. (Mirror)
Winga wa Brazil Willian, 32, ana matumaini ya kupata ufanisi Arsenal licha ya kukabiliwa na kibarua kigumu msimu wa kwanza tangu alipojiunga na klabu hiyo kutoka Chelsea. (Mirror)

Sevilla wanamtaka mshambuliaji wa Wolves Mhispania Rafa Mir, 23, ambaye kwa sasa yuko klabu ya La Liga ya Huesca kwa mkopo. (La Razon - in Spanish)
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom