Kylian Mbappe Kuiongoza Ufaransa

Izy_Name

JF-Expert Member
Apr 9, 2020
647
1,295
Kylian Mbappe ndiye mshambuliaji aliyechaguliwa kuwa mbadala wa Hugo Lloris ambaye alistaafu kuchezea timu ya taifa Januari 2023, mwezi mmoja baada ya Ufaransa kupoteza Kombe la Dunia kwa Argentina.

Mbappe ataanza kazi yake ya unahodha katika kikosi kwa mara ya kwanza itakuwa Ijumaa, Machi 24, katika mechi ya kufuzu kwa Euro 2024 dhidi ya Uholanzi Mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann aliteuliwa kuwa naibu wa Mbappe baada ya beki wa kati wa Manchester United Raphael Varane pia kustaafu Kylian Mbappe ndiye nahodha mpya wa timu ya Ufaransa, akimrithi Hugo Lloris ambaye alistaafu.


Kylian Mbappe Ateuliwa Nahodha Mpya wa Ufaransa Baada ya Lloris Kustaafu.
Mshambulizi huyo wembe wa Paris Saint-Germain mwenye umri wa miaka 24, alikubali cheo hicho baada ya kufanya mazungumzo na kocha Didier Deschamps mapema siku ya Jumatatu, Machi 20. Lloris, ambaye ni Mlinda mlango wa Tottenham, alistaafu mashindano ya kimataifa mnamo Januari 2023, mwezi mmoja baada ya Ufaransa kupoteza Kombe la Dunia kwa Argentina. Lloris, 36, alishikilia nafasi ya unahodha kwa zaidi ya muongo mmoja.

Mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann aliteuliwa kuwa naibu wa Mbappe baada ya beki wa kati wa Manchester United Raphael Varane pia kustaafu kufuatia ushinde wa Argentina mnamo Disemba 2022. Mbappe, ambaye ameiwakilisha nchi yake katika mechi 66, alikuwa akipigiwa upatu kupewa cheo hicho.
Hii ni baada ya nyota huyo kuipa Ufaransa hat-trick katika fainali ya Kombe la Dunia zilizo chezwa Qatar na pia kuisaidia Les Bleus kutwaa taji hilo mwaka wa 2018.



Kando na majukumu mapya aliyopewa katika timu yake ya taifa, mshambuliaji huyo wa zamani wa Monaco pia ni nahodha msaidizi wa PSG akimsaidia Marquinhos wa Brazil.

Mbappe ndiye aliongoza klabu hiyo wakati wa mechi ya Jumapili dhidi ya Rennes ambapo PSG walipoteza.
Kibarua chake cha kwanza kama nahodha kitakuwa Ijumaa, Machi 24, katika mechi ya kufuzu kwa Euro 2024 dhidi ya Uholanzi kwenye Uwanja wa Stade de France nchini ufaransa.

SOURCE

Kylian Mbappe Kuiongoza Ufaransa

 
Mbape anafaa maana anainua sana sprit ya team
Ila msaidizi wake angekuwa Tchoumen yule dogo wa Madrid ingekuwa poa
 
angekuwa assistant captain halafu faza mmoja awe ndio captain sasa, sidhan kama ana leadership traits japo ana kipaji kikubwa, angeendelea kuwa nyuma ya mwingine na kujifunza zaidi angalau baada ya miaka 2 ndo awe first choice, hata kule psg ucaptain wake ndo umezidisha ubinafs badala ya kuunganisha timu.
 
Mbape anapenda ukubwa ila kama ni muungwana alitakiwa akatae hyo nafasi maana bado mdogo sana ana mda wa kujifunza
 
Back
Top Bottom