Tetesi: Richmond na Kigoda Ikulu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tetesi: Richmond na Kigoda Ikulu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Huduma, Dec 13, 2008.

 1. H

  Huduma Member

  #1
  Dec 13, 2008
  Joined: Jan 26, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  INAELEKEA ajira katika nafasi za juu ikiwemo zile za washauri na waandishi huko Ofisi za juu hazifanyiwi utafiti wa kutoshq na sasa kuna madai kwamba baadhi ya wafanyakazi wa Richmond na Kigoda hivi leo wameajiriwa Ikulu. Katika hao ni pamoja na wale ambao kwa muda mrefu wamekuwa makuadi wa wakubwa mbalimbali na walionunuliwa na Watanzania wasio na asili ya Kiafrika.

  Wamekuwa wakifanya kazi hii sio Tanzania tu bali pia hata nchi za nje ikiwemo Marekani na Uingereza.
   
 2. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #2
  Dec 13, 2008
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Kiongozi Huduma,

  Tetesi yako bado haina nguvu na inapwaya sana . . . JF We Dare to Talk Openly . . .

  Mwaga mtama tetesi ifanyiwe kazi.
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Dec 13, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  akina nani hao????
   
 4. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #4
  Dec 13, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Please give more details.......Kama wapo nao tunawalipua tuu!
   
 5. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #5
  Dec 14, 2008
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  EE bwana Huduma, mwaga michuzi hiyo lete hapa JF.Wadau hapa wachmabua vitu vyote kama karanga!
   
 6. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #6
  Dec 14, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Huduma tuhudumie nasi tuwape huduma watanzania wengine .This is very serious tetesi mkubwa Huduma .Mwaga nasi tuta tawanya
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #7
  Dec 14, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,565
  Likes Received: 18,307
  Trophy Points: 280
  Hii inaonyesha jamaa ana chuki binafsi ama vivu tuu kuwa kwanini fulani awe mahala fulani. Huduma hakuna ubishi jamaa ni kichwa kwenye fani ya habari.
  Katika mchakato wa 2005, chaguo bora alikuwa ni Dr. Salim, japo sio msomi kihivyo ana busara na inteligent kuliko JK.
  Nakuhakikishia jamaa ni kichwa alisimamia zengwe kali mpaka Dr. Salim chali. Hivi jamani kunaubaya wowote kuwashukuru watu waliokusaidia.

  Kama miongoni mwao wana uwezo kuna ubaya wowote kuwapa ulaji?.

  Eti usimpe ulaji mshikaji kwa sababu zamani aliwahi kumtumika fulani.

  Hoja ni kama jamaa amepewa madaraka na huku hana uwezo huo, hiyo ndiyo ingekkuwa issue chini ya hapo ni majungu.
   
 8. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #8
  Dec 14, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Kusema kweli JK anamatatizo na hao washauri wake; kwahiyo sintashangaa kama tetesi hizo ni kweli kwani nasikia pia amemteua jamaa anayeishi na kufanya kazi nje ya Tanzania kuja kuwa mwenyekiti wa bodi ya TIB [Tanzania Investment Bank]; kama hiyo ni kweli bas itabidi huyo bwana alipiwe ticket ya ndege na malazi hoteli kubwa kubwa mara anapokuja kwenye vikao.; hizi ni unnessary burden kwa walipa kodi.Hivi kweli hakuna watu hapa nchini wenye qualification na uzoefu wa kuongoza TIB ambao wangeweza kuifanya kazi hiyo bila gharama za ziada za ndege na hoteli?. Si hivyo tu , huyo bwana aliyeteuliwa ni mkurugenzi wa benki nyingine binafsi hapa nchini sasa huoni kuna conflict of interest kumteua mtu kama huyo kuwa mwenyekiti wa benki ya Umma? Hawa wapambe wa muungwana wanampelekea madudu mengi sana na yeye anayapitisha tu pengine muungwana mensab mdogo anamchosa sana hana time ya kufikiri sana!!
   
 9. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #9
  Dec 14, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Bulesi hapa JF huwa hatusemi tunasikia kwa kurudia .Unaweza kusema umesikia mara moja na ya pili unataja jina .Taja tunyooshe kumbukumbu tafadhali ndiyo maana JF tuko .

  Wito : Jamani kama kuna watu wanakuja hata namwendelezo wa tunasikia na hawataji majina nadhani hawatufai wakake pembeni .Tuko hapa kunyoosha kumbukumbu so taja sisi tutatafuta ukweli nakuusema hapa .
   
 10. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #10
  Dec 14, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Lunyungu mkuu nimekusikia lakini ni vema kuelekezana kwa busara kwani jamvi hili si la wachache wewe na wenzio; huwezi kutoa hukumu ya nani awemo na nani akae pembeni kwa kutomtaja mtu jina!! Ningetumia lugha ya matusi sawa lakini sikufanya hivyo. Heshima mbele. Huyo bwana anaitwa William Lyakurwa yuko Kenya na mkurugenzi wa Akiba Commercial Bank. Lifanyie kazi kama unaweza.
   
 11. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #11
  Dec 14, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Sitaki kuacha kuaminini kwamba anatania, naona kama mtu makini lakini ana "machale"
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #12
  Dec 14, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,565
  Likes Received: 18,307
  Trophy Points: 280
  Tiketi ya ndege is nothing compared to brain power. Naunga mkono wabongo walioko nje kwenye madaraka ya maana, waitwe nyumbani na kutoa consultancy. Jamaaa atakuwa ameyeuliwa kutokana good track record yake.

  Kipindi cha Ben mchumi maarufu wa Chile, Prof. Hernando De Sotto alialikwa nchini. Fee yake ni Dola 100,000 kwa saa. Tulimualika kwa masaa 6. Hapo bado pia tulimlipia first class return ticket na 5star hotel accomodation.

  Hebu tuwe proud na wenzetu waliotoa tongotongo waje japo watuonyeshe njia. Na speed ya maendeleo ya Bongo, utafikia wakati hata sisi wabeba maboxi tutarudi.
  Back to the topic una hoja, ama bado ni majungu tuu?.
   
 13. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #13
  Dec 14, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wewe bwana vipi?Sio kwamba ajira hazifanyiwi uchunguzi,huo ndio mfumo wenyewe sasa.
   
 14. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #14
  Dec 14, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni tetesi tu kama ulivyosema.Lakini sitashangaa kama jamaa hao tayari washametinga Ikulu.Hawa wote si jamaa katika ulaji,sasa watatupanaje?
   
 15. I

  Iga Senior Member

  #15
  Dec 15, 2008
  Joined: Dec 17, 2007
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mbona hii issue kwangu 'clear' au JF hamna habari ni nani na kina nani wako Ikulu hivi leo na historia yao hadi wakafika hapo. Ni dhahiri hakuna serious investigation yoyote iliyofanyika wala vetting ya maana katika kuhakikisha Ikulu haiwi danguro sio kwa wanaotoka nje bali kwa wale waliomo ndani. Na msishangae kuona kinayamkera mara baada ya Krismasi na mwaka mpya.

  Nchi hii ina watu wazuri na wenye vichwa vilivyotulia kumshauri kiongozi wa nchi na sio kama ilivyo sasa eti.....


  Haya ya Chama Tawala kuchota fedha za Hazina, NPF/NSSF/PPF achilia mbali sehemu nyingine hayakuanza jana eti!

  Kabla ya Vyama vingi hili lilihalalishwa kwani Baba wa Taifa alikuwa si mwizi wala hakuwa na mtu wa kuwafanya watoto,jamaa, mke wake kuwa wezi na wao pia maana huyu alikuwa mtakatifu, mcha Mungu, mtu asiye na makuu na aliyewatakiwa mema Watanzania wote kwani alituchukulia wote kama wanawe.

  Kazi ilianza mara tu baada ya nchi kuamua kuwa na vyama vingi na viongozi wote wa chama tawala wanajua ujanja wa kununua Radar Mobovu kwenye miaka ya tisini na miaka ya karibuni ilivyotumika kuipatia CCM fedha; kuna Wahindi kadhaa walipewa tenda zote za kutununulia nafaka kutoka fedha za msaada ili hela hizo ziwe zao na za CCM; wastaafu wanalipwa fedha finyu baada ya chama tawala kuwanya mafao yao kiasi cha kutosha na kutisha!

  Na fedha hizo ndizo hizo hizo zinazotumika kuwahonga wanasiasa uchwara wa vyama pinzani wakachanganyikiwa na kusababisha upinzani kukosa mwelekeo.

  Lakini kiasi kinachoingia kwenye mfuko wa chama kwa taarifa za kuaminika nilizo nazo ni kiasi kidogo sana ukilinganisha na kile kinachoingia kwenye mifuko ya makuwadi na wanasiasa wa chama chenyewe.
   
 16. M

  Mbunge Senior Member

  #16
  Dec 16, 2008
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bila shaka kuna upungufu mkubwa katika kazi ya kupeleleza watu wanaofaa kushika nyadhifa mbalimbali hapa nchini.

  Siwezi kushangaa kukuta mahala kama Ikulu pameajiri watu wale wale wanaopanga kumpangua Mheshimiwa rais kabla ya kumaliza hata kipindi chake cha pili.

  Tunajua magazeti ya Chama na Serikali yapo upande wa rais vipi walio Ikulu nao wawe na magazeti yanayomilikiwa kiajabuajabu na ajenda yake haijulikani. Na watu hawa wamepata fedha hizo wapi kama sio EPA, Kagoda na Richmond ya kununua kampuni nzinma na kiwanda chake cha uchapishaji?

  Maana utakuta kuna watu walikuwa wakifukuza windo na mbwa mwitu na sasa eti wanajidai wanakula na kina Sungura!

  Masuala ya ajira na utiifu na uaminifu kwa kiongozi aliyeko madarakani kwa hakika bado yanahitaji kufanyiwa kazi ya ziada ili tusije tukajikuta tunaajiri wageni wanaojidai Watanzania au askari wa kukodiwa huko Ikulu, Waziri Mkuu, Wizara ya Mambo ya ndani, Wizara ya Nchi za nje na kwingineko!
   
Loading...