Tetesi;noti ya elfu hamsini

Tetesi;noti ya elfu hamsini

Kweli mkuu maana jana imekabidhiwa kwa rais wa zanzibar, ila kiuchumi tutakuwa hoooi kama Zimbabwe muda c mrefu au wanatengeneza mazingira ya kuiba fedha nyingi kiurahisi

Haujajichanganya kweli mkuu?!!
 
Iliyokabudhiwa kwa rais wa zbar ni sarafu ya sh. 50.000 na haitaingizwa ktk mzunguko! Wengine wanaeleza vitu wasivyovijua. Na vema kama huna taarifa za kutosha bora ukae kimya
 
Mkuu mleta thread nadhani umechanganya
Kwenye kusikia kwako kinachosemwa ni
sarafu yenye thamani ya elfu hamsini na sio
noti kama ulivyosikia pia pesa hiyo hatatumika kwenye mzunguuko huu wa kawaida.

Yaani kama kununua chochote kama unga,sigara n.k zaidi ni maalum hasa Zanzibar inapiadhimisha miaka hamsini.

Kama sijawakuelewesha vizuri nadhani pia
watakuja watu wengine kwaufafanuzi nzuri.
ngoja nisubirie wenye data zaidi
 
Sarafu hiyo ya sh. Elfu 50 imetolewa maalumu kama
maadhimisho ya miaka 50 ya
mapinduzi ya Zanzibar, haitatumika
kwa manunuzi.
 
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa
sarafu maalumu ya kumbukumbu ya
miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar
yenye thamani ya sh 50,000.
Gavana wa BoT, Profesa Benno
Ndulu, alisema jana kuwa sarafu hiyo
iliyotengenezwa kwa madini ya fedha
kwa asilimia 92.50, imetolewa kwa
ajili ya kumbukumbu tu na
haitaingizwa katika mzunguko wala
kutumika kwa kulipia malipo ya aina
yoyote.
Taarifa kwa vyombo vya habari
iliyotolewa jana na Idara ya
Uhusiano wa Umma na Itifaki ya BoT
ilimnukuu Profesa Ndulu akisema
sarafu hiyo imetolewa kwa idadi ya
vipande 3,000 kwa ajili ya tukio hilo
na kuwahimiza wananchi kuinunua
kwa ajili ya kumbukumbu hiyo.
Kwa mujibu wa Gavana, kutolewa kwa
sarafu hiyo kunakwenda sambamba
na utaratibu wa Benki Kuu kutoa
sarafu maalumu za aina hiyo kama
sehemu ya maadhimisho ya
kumbukumbu ya matukio mbalimbali
muhimu ya kitaifa na kimataifa.
“Kwa kawaida, baada ya muda,
thamani ya sarafu kama hizi
huongezeka na kuwa na faida zaidi
kwa wanaozimiliki,” alisema Profesa
Ndulu.
Gavana Ndulu alieleza sarafu hizo
zitapatikana Januari 5 kwa bei ya sh
50,000 katika matawi ya benki za
biashara zitakazokuwa zimepata
sarafu hizo kutoka Makao Makuu ya
Benki Kuu, Dar es Salaam na matawi
ya Benki Kuu yaliyoko Zanzibar,
Arusha, Mbeya na Mwanza.
“Benki za biashara zinaweza pia
zikasambaza sarafu hizi kupitia
matawi yake,” alisema gavana na
kuongeza taarifa za usambazaji
zitatolewa na benki hizo.
Katika sarafu hiyo, upande wa mbele
unaonyesha sura ya hayati Sheikh
Abeid Aman Karume na maandishi
yanayosomeka: ‘Rais wa Kwanza wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi’. Upande mwingine wa
sarafu unaonyesha nembo ya Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar, maandishi
yanayosomeka: “Miaka Hamsini ya
Mapinduzi”, thamani ya sarafu na
miaka 1964-2014
 
Kwa kuwa uwezekano wa tz shillings kupanda thamani haupo, ni bora watufyatulie noti ya laki moja kabisa.
 
Kweli mkuu maana jana imekabidhiwa kwa rais wa zanzibar, ila kiuchumi tutakuwa hoooi kama Zimbabwe muda c mrefu au wanatengeneza mazingira ya kuiba fedha nyingi kiurahisi

Hakuna not ya elfu hamisi bali bank kuu wametengeneza sarafu ya elf hamsin maalum kwa ajil sherhe za mapinduz zanzibar na haitakuwepo kwenye mzunguko wa fedha
 
Back
Top Bottom