Tetesi: Kweli Tutafika kwa mtindo huu!!

Tetesi: Kweli Tutafika kwa mtindo huu!!

Alafu hizo Bilioni 800 si kweli Km ndio zinazokusanywa itakua wanakusanya Zaidi!
 
duchi:hapa Mzee Mkapa anaingiaje?hata hivyo mtu mwenye akili timamu hawezi kumlinganisha MKAPA NA KIKWETE
Ni kweli hata mwendawazimu hawezi kuwalinganisha huyo na huyu
- Aliyejenga mabarabara mara mbili ya idadi ya kilomita alizozikuta
- Aliyejenga madaraja makubwa sana 3 kati ya 5 aliyoyaahidi Nyerere
- Aliyeleta vyuo vikuu zaidi ya 44 mara 4 zaidi ya waliowakuta
- Aliyezesha wanafunzi 160,000 wa vyuo vikuu mara 4 zaidi ya aliowakuta
- Aliyejenga chuo kikubwa kuliko vyote EAC.
- Aliyejenga chuo kikubwa cha sayari kwenye ukanda huu cha Nelson Mandera
- Aliyepeleka sekondari hadi kwenye kata
- Aliyezalisha umeme wa mega wait 1500 mara mbili zaidi ya alioukuta
- Aliyeanzisha umradi wa kupeleka umeme vijijini?
- Anayejenga bomba la gesi kubwa toka Mtwara hadi DAR
- Anayejenga barabara ya mabasi yaendayo haraka.
- Anayekubalika na viongozi wote wakubwa wa Dunia hii
- Aliyeanzisha hospital ya tiba ya moyo nchini nk.

Lakini una point maana nasikia huko kwneye Halmashauri pesa zikishafika wakurugenzi wanazifanya kama za kwao binafsi wanazitafuna weee!!!![/QUOTE]

Acha kubwabwaja maneno, kwanza siku hizi halmashauri zimekauka, fuatilia ujue,kilichopo sasa hivi ni kuleta hela za kulipa mishahara, miradi ya maendelo imesimama! Sasa wakurugenzi wataiba mishahra ya watumishi?
 
Kwanza hongera kwa kukusanya mara mbili zaidi ya Serikali ya Mkapa.
Pili pesa zinakwenda kwenye miradi mikubwa ya barabara na grsi ambayo miaka michache ijayo itakuwa ni mkombozi wetu

Acheni uongo, sasa barabara zinajengwa na pesa zipi maana tunaambiwa deni la taifa linaongezeka kwa kwa sababu tunakopa ili tujenge miundo mbinu sasa mnasema hizo hela zijajenga barabara. Huu uongo una mwisho na mtaumbuka soon.
 
duchi:hapa Mzee Mkapa anaingiaje?hata hivyo mtu mwenye akili timamu hawezi kumlinganisha MKAPA NA KIKWETE

Anajaribu kuringanisha mav.i na tope(Mkapa),mkapa aliweza kudhibiti thamani ya pesa.1US$=Tzs 700. mfuko wa saruji Tzs.4,000,Sukari 1kg Tzs.250 Bati ft 10 Tzs. 7,500 pia alijitahidi kudhibiti huu mfumo wa undugu na kujuana kwenye swala la kupata ajira,sasa shida kwa huyu fast jet yaani nadhani kila mtu anaona kinachoendelea,yaani shaghalabaghala.
 
Ni kweli hata mwendawazimu hawezi kuwalinganisha huyo na huyu
- Aliyejenga mabarabara mara mbili ya idadi ya kilomita alizozikuta
- Aliyejenga madaraja makubwa sana 3 kati ya 5 aliyoyaahidi Nyerere
- Aliyeleta vyuo vikuu zaidi ya 44 mara 4 zaidi ya waliowakuta
- Aliyezesha wanafunzi 160,000 wa vyuo vikuu mara 4 zaidi ya aliowakuta
- Aliyejenga chuo kikubwa kuliko vyote EAC.
- Aliyejenga chuo kikubwa cha sayari kwenye ukanda huu cha Nelson Mandera
- Aliyepeleka sekondari hadi kwenye kata
- Aliyezalisha umeme wa mega wait 1500 mara mbili zaidi ya alioukuta
- Aliyeanzisha umradi wa kupeleka umeme vijijini?
- Anayejenga bomba la gesi kubwa toka Mtwara hadi DAR
- Anayejenga barabara ya mabasi yaendayo haraka.
- Anayekubalika na viongozi wote wakubwa wa Dunia hii
- Aliyeanzisha hospital ya tiba ya moyo nchini nk.

Ni kweli Kikwete kafanya haya, lakini ulinganishe kodi iliyokuwa ikikusanywa enzi za Mkapa kwa mwez na mambo aliyofanya Mkapa, kisha linganisha makusanyo ya kodi kwa mwezi wakati huu wa Kikwete na hayo unayosema kafanya, Nenda kwa Mwinyi na Nyerere fanya ulinganifu huo huo! Alafu linagnisha mapato hayo kwa awamu zote hizi na matumizi yale yaliyoenda kwenye miradi ya wananchi na yale ya yaliyoenda kwenye matumizi ya kawaida ya serikali! Nafikiri wote walifanya vizuri,lakini Nyerere alifanya vizuri zaidi!
 
Lakini una point maana nasikia huko kwneye Halmashauri pesa zikishafika wakurugenzi wanazifanya kama za kwao binafsi wanazitafuna weee!!!!

Acha kubwabwaja maneno, kwanza siku hizi halmashauri zimekauka, fuatilia ujue,kilichopo sasa hivi ni kuleta hela za kulipa mishahara, miradi ya maendelo imesimama! Sasa wakurugenzi wataiba mishahra ya watumishi?[/QUOTE]
Huko Idara gani kwenye Halmashauri? Duh! jamaa amekuwa makali kuambiwa wanapiga meno mapesa!
 
800 bilioni ni pesa ndogo sana kwa nchi yenye watu 45 million.
kwa wastani kila mwananchi anachangia 18,000 kwa mwezi kama kodi,hii inaonyesha bado tax base yetu tanzania ni ndogo sana,ndio maaana rais anahaa kutafuta misaada kwa wahisani.

800b kwa mwezi ni sawa na 9.6 trillions, sasa tuambie pesa ya ndani inachangia asilimia ngapi katika bajeti ya taifa. Na hii yote ingekuwa reflected kwenye budget ingekuwaje? JK hangekuwa na haja ya kuangaika iwapo angesimamia vizuri makusanyo na matumizi ya mapato ya ndani. Hakuna hoja madhubuti ya kutetea matumizi maalum hapa.
 
duchi:Mkapa alitumia pesa alizokusanya kujenga maendeleo na pesa ilikuwa na thamani mdogo wangu,JK miradi yote ya maendeleo ni mikopo.KAMA WEWE MFATILIAJI TANZANIA TUNADAIWA KIASI GANI?KUKMBUKA MKAPA ALIFUTA

duchi:KABLA HUJAANDIKA SHUGHULISHA AKILI YAKO
 
duchi:Mkapa alitumia pesa alizokusanya kujenga maendeleo na pesa ilikuwa na thamani mdogo wangu,JK miradi yote ya maendeleo ni mikopo.KAMA WEWE MFATILIAJI TANZANIA TUNADAIWA KIASI GANI?KUKMBUKA MKAPA ALIFUTA MADENI YOTE.

duchi:KABLA HUJAANDIKA SHUGHULISHA AKILI YAKO
 
Kwanza hongera kwa kukusanya mara mbili zaidi ya Serikali ya Mkapa.
Pili pesa zinakwenda kwenye miradi mikubwa ya barabara na grsi ambayo miaka michache ijayo itakuwa ni mkombozi wetu

wakati wa mkapa kilo ya sukari ilikuwa sh 400 sasa ni sh 2000.....dola sh 720 sasa 1600...
soma vibao vya ukandarasi wa barabara utajuwa kuwa barabara ni mkopo ila ikinunua diesel kila lita unachangia road fund
 
Bilioni 800 ukajenge Barabara, ulipe mishahara ya walimu, ulipe madaktari, ulipe polisi, wanajeshi, wabunge,halmashauri, ulipe madeni nje, mashirika kimataifa, utoe michango huko kwenye mashirika ambayo sisi wanachama, utoe mikopo ya wanafunzi, ujunge mashule, vyuo, nk

Lakini una point maana nasikia huko kwneye Halmashauri pesa zikishafika wakurugenzi wanazifanya kama za kwao binafsi wanazitafuna weee!!!!

Mkuu nikujulihe tu kuwa serikali ina vyanzo vingi sana vya mapato tuna mbuga za wanayama(utalii), Serikali ina hisa kweye makampuni kibao, kuna adhabu, ada mbalimbali za huduma, michango ya wafadhili, etc na bado hatuusogei tukubali kuna shida mahal
 
Bilioni 800 ukajenge Barabara, ulipe mishahara ya walimu, ulipe madaktari, ulipe polisi, wanajeshi, wabunge,halmashauri, ulipe madeni nje, mashirika kimataifa, utoe michango huko kwenye mashirika ambayo sisi wanachama, utoe mikopo ya wanafunzi, ujunge mashule, vyuo, nk

Lakini una point maana nasikia huko kwneye Halmashauri pesa zikishafika wakurugenzi wanazifanya kama za kwao binafsi wanazitafuna weee!!!!

kwani kila mwezi unapanga bajeti mpya ?
 
Kwanza hongera kwa kukusanya mara mbili zaidi ya Serikali ya Mkapa.
Pili pesa zinakwenda kwenye miradi mikubwa ya barabara na grsi ambayo miaka michache ijayo itakuwa ni mkombozi wetu

lete ushahidi .
 
800 bilioni ni pesa ndogo sana kwa nchi yenye watu 45 million.
kwa wastani kila mwananchi anachangia 18,000 kwa mwezi kama kodi,hii inaonyesha bado tax base yetu tanzania ni ndogo sana,ndio maaana rais anahaa kutafuta misaada kwa wahisani.

TATIZO HAPA NI HIYO KAZI MAALUM na wala siyo kiasi kinachokusanywa .
 
duchi:hapa Mzee Mkapa anaingiaje?hata hivyo mtu mwenye akili timamu hawezi kumlinganisha MKAPA NA KIKWETE

Ulinganifu huo ulenge kupata aliye afadhali kati ya wabovu waliohusishwa.
 
duchi:Mkapa alitumia pesa alizokusanya kujenga maendeleo na pesa ilikuwa na thamani mdogo wangu,JK miradi yote ya maendeleo ni mikopo.KAMA WEWE MFATILIAJI TANZANIA TUNADAIWA KIASI GANI?KUKMBUKA MKAPA ALIFUTA MADENI YOTE.

duchi:KABLA HUJAANDIKA SHUGHULISHA AKILI YAKO

Nikiwakumbuka Netgroup solution!!! Sina hamu na Nkapa.
 
Ni kweli Kikwete kafanya haya, lakini ulinganishe kodi iliyokuwa ikikusanywa enzi za Mkapa kwa mwez na mambo aliyofanya Mkapa, kisha linganisha makusanyo ya kodi kwa mwezi wakati huu wa Kikwete na hayo unayosema kafanya, Nenda kwa Mwinyi na Nyerere fanya ulinganifu huo huo! Alafu linagnisha mapato hayo kwa awamu zote hizi na matumizi yale yaliyoenda kwenye miradi ya wananchi na yale ya yaliyoenda kwenye matumizi ya kawaida ya serikali! Nafikiri wote walifanya vizuri,lakini Nyerere alifanya vizuri zaidi!
Ni kweli Mwl. Nyerere alijitahidi sana lakini bado nikikumbuka haya machache yafuatayo kati ya mengi nasikia machungu sana.
§ Tulitembea kilomita nyingi kufuata zahanati na ukifika huko uongee faragha na daktari umpe chochote ndiyo upate matibabu.
§ Hatukuweza kumudu kunywa chai, sukari ilikuwa haipatikani hali ya kuwa pesa tunazo.
§ Tulifulia nguo kwa kutumia majani ya mpapai au mrenda, sabuni ilikuwa shida kufipatikani. Nakumbuka sabuni za mbuni, gardenia, Ilula nk. Ilikuwa ni issue kuzipata.
§ Maduka ya kaya na RTC walikuwa ni miungu watu kwa vile bidhaa muhimu zilikuwa adimu
§ Nakumbuka wazanzibari walivyokuwa wanatuchukulia dada zetu kilahisi shauri ya kupe kitu kidogo kama collogate tu
§ Kumiliki redio cassete tu ilikuwa issue lakini hivi sasa hata msukuma mkokoteni anamiliki TV
§ Mmiliki wa pikipiki wakati huo alihesabika kuwa ni tajiri lakini hivi sasa hata muuza genge anaweza kumiliki bodaboda.
§ Nakumbuka tulivyokuwa tunavaa nguo sare za kiwanda cha Urafiki na viatu sare vya kampuni za Bora shoes na Moro shoes kama watoto wa shule, lakini navyo kupata ilikuwa ni issue mpaka ulanguliwe.
§ Ukitaka kusafiri kwenda bara wakati huo usafiri ni mabasi ya kampuni ya Kamata au Treni uweke booking miezi miwili au mitatu kabla.
§ Usafiri wa mjini kwa kutumia UDA ni balaa watu wanagombea kuingia ndani ya bus kwa kupitia madirishani.
§ Timu za michezo zilikosa sare za michezo, ilkuwa ni kawaida timu kubwa kama Simba na Yanga kuiona sare ya aina moja kwa miaka miwili bila ya kubadilisha.
§ Ukitaka mawasiliano ya simu ni issue, ni jambo la kawaida pale Dar maeneo ya usahilini kama Temeke, Tandika, Ilala, Buguruni na Magomeni, mtaa mzima ukakosa mtu mwenye simu kuweza kuwasiliana pindi itokeapo dharura ya msiba nk.
§ Rushwa ilienea kila sehemu hata kwa mambo madogo madogo na ilitambulika kwa majina mengi kama vile mrungula, propoza, mlango wa nyuma, zunguka mbuyu, shati la mikono mirefu, chai, mchicha, hongo nk.
§ Bidhaa muhimu kama mchele, unga wa sembe, unga wa ngano, sabuni, mafuta ya kupikia, dawa ya meno, mabati, saruji, viatu, nguo, nk. Havipatikani isipokuwa kwa kutoa hongo.
 
Back
Top Bottom