Tetesi: Kweli Tutafika kwa mtindo huu!!

Tetesi: Kweli Tutafika kwa mtindo huu!!

Kama sehemu ya hizo fedha zinatumika kweli kulipa walimu na kujenga shule, basi Shule ya Msingi Machala isingekuwa na mwalimu mmoja anayefundisha kuanzia chekechea hadi darasa la saba na jengo kama hili unless sehemu kubwa ya fedha hizo ni kwa matumizi ya shule maalum.

attachment.php


Mbunge wa Jimbo hili si ndiye Waziri wa Elimu!!? Ukistaajbu ya Mussa, utayaona ya Filauni. Sasa Filauni anajidhihirisha Ni nani kwenye Elimu.
 
ninajivunia kumpata rais kama Mzee MKAPA,sasa hivi watanzania makini wanamkumbuka na wanatamani kama angekuwa rais tena:duch jaribu kuwa mchambuzi na mtafiti
 
Anajaribu kuringanisha mav.i na tope(Mkapa),mkapa aliweza kudhibiti thamani ya pesa.1US$=Tzs 700. mfuko wa saruji Tzs.4,000,Sukari 1kg Tzs.250 Bati ft 10 Tzs. 7,500 pia alijitahidi kudhibiti huu mfumo wa undugu na kujuana kwenye swala la kupata ajira,sasa shida kwa huyu fast jet yaani nadhani kila mtu anaona kinachoendelea,yaani shaghalabaghala.

“Chakuangalia siyo kupanda kwa bei kwa mfuko wa saruji, bati au mchele ila cha kuangalia ni je mwananchi anaweza kumudu kununua vitu hivyo? Kwa kweli nguvu ya mwananchi kumudumu kununua imeongezeka, na haya ndiyo mafanikio ya Serikali ya CCM” Aliyasema haya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Sera Steven Massatu Wassira
 
wakati wa mkapa kilo ya sukari ilikuwa sh 400 sasa ni sh 2000.....dola sh 720 sasa 1600...
soma vibao vya ukandarasi wa barabara utajuwa kuwa barabara ni mkopo ila ikinunua diesel kila lita unachangia road fund
“
Chakuangalia siyo kupanda kwa bei kwa mfuko wa saruji, bati au mchele ila cha kuangalia ni je mwananchi anaweza kumudu kununua vitu hivyo? Kwa kweli nguvu ya mwananchi kumudumu kununua imeongezeka, na haya ndiyo mafanikio ya Serikali ya CCM” aliyasema haya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Sera Steven Massatu Wassira




 
Bilioni 800 ukajenge Barabara, ulipe mishahara ya walimu, ulipe madaktari, ulipe polisi, wanajeshi, wabunge,halmashauri, ulipe madeni nje, mashirika kimataifa, utoe michango huko kwenye mashirika ambayo sisi wanachama, utoe mikopo ya wanafunzi, ujunge mashule, vyuo, nk

Lakini una point maana nasikia huko kwneye Halmashauri pesa zikishafika wakurugenzi wanazifanya kama za kwao binafsi wanazitafuna weee!!!!
umeni pre-empty mkuu. yeye akiona bilioni 800 anapagawa wakati km 1 tu ya barabara ya lami ni bilioni 1.
 
Ni kweli Mwl. Nyerere alijitahidi sana lakini bado nikikumbuka haya machache yafuatayo kati ya mengi nasikia machungu sana.
§ Tulitembea kilomita nyingi kufuata zahanati na ukifika huko uongee faragha na daktari umpe chochote ndiyo upate matibabu.
§ Hatukuweza kumudu kunywa chai, sukari ilikuwa haipatikani hali ya kuwa pesa tunazo.
§ Tulifulia nguo kwa kutumia majani ya mpapai au mrenda, sabuni ilikuwa shida kufipatikani. Nakumbuka sabuni za mbuni, gardenia, Ilula nk. Ilikuwa ni issue kuzipata.
§ Maduka ya kaya na RTC walikuwa ni miungu watu kwa vile bidhaa muhimu zilikuwa adimu
§ Nakumbuka wazanzibari walivyokuwa wanatuchukulia dada zetu kilahisi shauri ya kupe kitu kidogo kama collogate tu
§ Kumiliki redio cassete tu ilikuwa issue lakini hivi sasa hata msukuma mkokoteni anamiliki TV
§ Mmiliki wa pikipiki wakati huo alihesabika kuwa ni tajiri lakini hivi sasa hata muuza genge anaweza kumiliki bodaboda.
§ Nakumbuka tulivyokuwa tunavaa nguo sare za kiwanda cha Urafiki na viatu sare vya kampuni za Bora shoes na Moro shoes kama watoto wa shule, lakini navyo kupata ilikuwa ni issue mpaka ulanguliwe.
§ Ukitaka kusafiri kwenda bara wakati huo usafiri ni mabasi ya kampuni ya Kamata au Treni uweke booking miezi miwili au mitatu kabla.
§ Usafiri wa mjini kwa kutumia UDA ni balaa watu wanagombea kuingia ndani ya bus kwa kupitia madirishani.
§ Timu za michezo zilikosa sare za michezo, ilkuwa ni kawaida timu kubwa kama Simba na Yanga kuiona sare ya aina moja kwa miaka miwili bila ya kubadilisha.
§ Ukitaka mawasiliano ya simu ni issue, ni jambo la kawaida pale Dar maeneo ya usahilini kama Temeke, Tandika, Ilala, Buguruni na Magomeni, mtaa mzima ukakosa mtu mwenye simu kuweza kuwasiliana pindi itokeapo dharura ya msiba nk.
§ Rushwa ilienea kila sehemu hata kwa mambo madogo madogo na ilitambulika kwa majina mengi kama vile mrungula, propoza, mlango wa nyuma, zunguka mbuyu, shati la mikono mirefu, chai, mchicha, hongo nk.
§ Bidhaa muhimu kama mchele, unga wa sembe, unga wa ngano, sabuni, mafuta ya kupikia, dawa ya meno, mabati, saruji, viatu, nguo, nk. Havipatikani isipokuwa kwa kutoa hongo.
Hii nayo imeingiaje?
 
"
Chakuangalia siyo kupanda kwa bei kwa mfuko wa saruji, bati au mchele ila cha kuangalia ni je mwananchi anaweza kumudu kununua vitu hivyo? Kwa kweli nguvu ya mwananchi kumudumu kununua imeongezeka, na haya ndiyo mafanikio ya Serikali ya CCM" aliyasema haya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Sera Steven Massatu Wassira

Kwa jinsi watu wa hali chini wanavyonunua bodaboda na simu za mikononi
kama pipi naungana na kauli ya Steven Wasira.



 
Kwanza hongera kwa kukusanya mara mbili zaidi ya Serikali ya Mkapa.
Pili pesa zinakwenda kwenye miradi mikubwa ya barabara na grsi ambayo miaka michache ijayo itakuwa ni mkombozi wetu

Madini hayakutakiwa kuwa mkombozi wenu mkuu?na yameanza lini kuchimbwa?je unafikiri kutakuwa na jipya huko kwenue gesi?tafakari ,tumia akili.
 
Back
Top Bottom