TETEMEKO: Ni wakati wa kujitayarisha kwa yajayo

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
17,882
13,172
Tetemeko lililtokea majuzi limewashangaza wengi hasa wanaoishi ukanda huu wa Pwani.

Kama sikosei hili ni tetemeko la pili katika muda wa miaka takriban minne au mitano nlilolisikia lakini kumbe yamekuwepo mengi.
Nimekaa Dar es salaam kwa kipindi kirefu sana lakini sikumbuki kuona tetemeko lililotikisa kama la juzi.

Nimeingia mtandaoni na nimeona kuwa katika miaka tisa iliyopita kumekuwa a seismic activity inayoongezea na data ni kama ifuatavyo:

77
78



about 21 hours ago 5.0 magnitude, 10 km depth
Kilindoni, Pwani, Tanzania

2 days ago 6.0 magnitude, 15 km depth
Kilindoni, Pwani, Tanzania

4 months ago 4.7 magnitude, 10 km depth
Utete, Pwani, Tanzania

2 years ago 4.7 magnitude, 10 km depth
Kisanga, Morogoro, Tanzania

3 years ago 4.9 magnitude, 12 km depth
Utete, Pwani, Tanzania

5 years ago 4.8 magnitude, 10 km depth
Vikindu, Pwani, Tanzania

6 years ago 4.2 magnitude, 10 km depth
Kisanga, Morogoro, Tanzania

6 years ago 4.3 magnitude, 10 km depth
Utete, Pwani, Tanzania

7 years ago 4.1 magnitude, 14 km depth
Kilindoni, Pwani, Tanzania

9 years ago 4.8 magnitude, 10 km depth
Vikindu, Pwani, Tanzania

Tunaona hatya matukio ya matetemeko yanaongezeka na kuwa na nguvu zaidi.

Mengi yanatokea eneo la kuanzia mto Rufiji kupanda huku juu yaani mkoa wa Pwani na Morogoro.

Waaalam wanasema haya matetemeko madogo madogo ndio chanzo cha tetemeko kubwa la kufunga kazi.

Ni wakati muafaka kuwa na sera ya kujua jinsi ya kukabili hali hii na vile vile mainjinia wetu kutengeneza taratibu za kujenga majengo yanayoweza kuhimili tetemeko la hadi Richter Scale ya 10.

Kupitia wizara ya Ujenzi lazima iandae rasimu ya Kitaifa namna gani tunaweza kukabiliana na jango la tetemeko kubwa zaidi.
 
Tetemeko limekuja kuwapa taarifa wana CCM hio. Yajayo ni maamuzi/majibu ya mungu kwa CCM yasiokwepeka, maana walimtaja taja sana kinafiki mungu kwa miaka 5 mfululizo (Msema kweli mpenzi wa mungu, Mungu amshukuru rais magufuli).
 
Tetemeko limekuja kuwapa taarifa wana CCM hio. Yajayo ni maamuzi/majibu ya mungu kwa CCM yasiokwepeka, maana walimtaja taja sana kinafiki mungu kwa miaka 5 mfululizo (Msema kweli mpenzi wa mungu, Mungu amshukuru rais magufuli).
Tetemeko lililotokea kabla ya la juzi lilikuja kuwapa taarifa watu gani?
 
Kituo cha jiolojia kinaitwaje kama kipo, au hatuna?
Tunacho kituo na kinaitwa Geological Survey of Tanzania, GST.Lakini ni kama hakipo kuelimisha jamii.
1597510256254.jpeg

Ila nimeona ramani ya matukio ya matetemeko nchini.
Hiyo dot nyekundu ni tetemeko la majuzi la 5.9 Richter huko Kilindoni baharini, km 90 toka DSM.
 
Back
Top Bottom