Tetemeko la Ardhi Kagera: Serikali imeonesha udhaifu mkubwa sana

MUGASHA THE HERO

JF-Expert Member
Mar 22, 2016
327
204
Mubelwa Bandio ambaye ni mtangazaj katika ktuo cha redio huko Washington DC amesema

"Nyie TBC. Mnataka tuuu tuseme.
Nyie si ndio kituo cha TAIFA?
Nyie si ndio mnaoendeshwa kwa kodi ya wananchi?
Nyie si ndio mnaotakiwa kuhabarisha kinachotokea kule ambako radio za kibiashara haziendi?
Si ni nyinyi mnaostahili kuwa WAZALENDO zaidi?
Nyie si ndio mnaotakiwa kuweka maslahi ya nchi mbele?
Nyie si ndio mnaotakiwa kufanya coverage ya MATUKIO YA KITAIFA?
Iweje mnapuuza TUKIO hili la tetemeko?
Watu 16 wanaingizwa uwanja wa Kaitaba sasa, mamia wameumia na dazeni za nyumba hazifai kwa makazi, mnaendelea na vipindi vya MUZIKI. Seriously????
Mmewapuuza wahanga wa tetemeko hili kubwa.
Na mnaendelea kusema mnahimiza UZALENDO?"

Tetemeko la Ardhi Kagera laiacha Serikali uchi

1. Taarifa tunasubiri wenzetu watoe kwanza ndo tukopi wakati ni tukio ndani ya nchi yetu wenyewe na wasomi tunao wengi mno

2. Taarifa za tetemeko zinapatika ndani ya siku moja na tayari inasomwa taarifa isiyoitwa ya hawali. Tunaambiwa vishindo vimesikika Burundi, Rwanda na Goma lakini hatujaona kifo wala madhara ya kitu kwa wilaya ya Ngara na Biharamulo.

Ni kweli kabisa hayo maeneo hakuna hata ufa mmoja katika nyumba zote? Ama ndo kupunguza idadi ili serikali iokoe pesa kwa kupunguza idadi harisi ya wahanga na hasara za Mali? yetu macho!

3. Siku ya tatu hakuna local wala international organization iliyojitokeza urgently walau kuwajari akina mama na watoto ambao wanalala nje eneo ambalo kila mmoja analielewa lilivyo na baridi ya maana sana, ukimwondoa rais Kenyatta, asante kwake.

4. Nchi ambayo wakati ukiwa msiba wa kitaifa Televisheni ya Taifa iko busy kurusha nyimbo watu wakiserebuka, wanaoombewa, kusaliwa na kuagwa ni kama hatuwafahamu vile.

5. Nchi ambayo tukio la sikukuu ya dini (IDD) linaenda live hewani ila tukio la kihistoria toka Tanzania iwepo halionekani kama ni la maana yoyote.

Nchi yangu Tanzania, nchi nzuri nakupenda.

TBC kushindwa Kuonesha matukio Kagera
Naianza TBC ikiwa ni taasisi ya serikali. Juzi kulitokea tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Vyombo vya habari vya kimataifa mara moja vilidaka habari hiyo na kuitangaza mara kwa mara na kuiweka kwenye websites zao. Niliona BBC, Al jazeera na CNN, wote wakifuatilia na hasa kutaka kujua kiwango cha uharibifu. Ajabu ni pale nilipowahi kuangalia TBC nikakuta mwanadada kapiga wanja na anaendelea na taarabu kama kawaida. Nikawahi ITV, huko nikakutana na maigizo ya Sauzi. Chanel 10 na hata Citizen ya Kenya hakuna kitu, ilikuwa ni jambo la kawaida tuuuu na maigizo ya kispanish!

Leo tena nafuatilia vipindi, yaonekana habari hizi ni kama michapo ya studio tu. Wahusika wanaulizia bi arusi aliyekimbia na kuulizia woga wa wananchi. Hatusikii mchanganuo wowote au kuelimishana juu ya hali hiyo.

Jamani Vyombo vyetu vya habari, kweli munajifahamu au ni mpaka wanasiasa watoe amri.

Jeshi la Wananchi Tanzania halijaonekana kwenye Tetemeko
Inashangaza Jeshi letu limekuwa la kuzuia maandamano na kufanya usafi huku ikitokea kazi ambayo inahitaji jeshi hawapo.

Tumekumbwa na matetemeko sijaona jeshi lakini jeshi liko kwa ulizi na majanga ni aibu kubwa jeshi kuingizwa kwenye siasa badala ya kufanya shughuli za kuwasaidia wananchi pale ambako wanahitaji msaada.

Jeshi inabidi libadilishe mwelekeo

Maafa Bukoba: Serikali ya Kenya ina uchungu sana kuliko Serikali ya Tanzania?

Habari zenu wanajukwaa!!!
Leo nimevisikia vyombo vya habari vikisema kwamba Rais wa Kenya Mh Uhuru Kenyatta amempigia simu Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Joseph Magufuli kwa ajili ya kumpa pole juu ya Maafa yaliyosababishwa na Tetemeko la Ardhi huko Kagera.

Rais Kenyatta pia ameahidi kutoa msaada wa Mablanketi na Magodoro kwa waathirika wa Tetemeko la Ardhi, Aidha msaada huo utawasili leo kutokea Kenya

Baada ya Tetemeko la Ardhi kutokea siku ya september 10, kuna kiongozi mmoja wa siasa wa chama pinzani alionyesha kaguswa na maafa hayo na kupanga safari ya kwenda kuwasabahi na kuwapa pole wahanga hao baada ya siku moja ya tetemeko hilo.

Kilichonishangaza ni kwamba ulipandishwa uzi humu Uliosema kuwa MH RAIS ANA UCHUNGU ZAIDI KULIKO NDUGU EDWARD LOWASSA, Nafikiri hii ilikuwa ni baada ya Kiongozi huyo kuonyesha ameguswa na kuamua kuwatembelea wahanga hao.
Sasa leo tumeisikia serikali ya Kenya ikitaka kutoa msaada wa waathiri wa Tetemeko la Ardhi.

Swali langu:
Je serikali ya Kenya ina uchungu sana kuliko serikali yetu Pendwa???????

My take: Linapotokea suala la Maafa au janga lolote la kitaifa Mtu yeyote anayeguswa anaweza kutoa msaada kwa waathirika kwa hiyo tuache siasa kwenye mambo ya msingi kwa ajili ya Taifa letu!!!

Ahsanteni na Mungu awe Nanyi
 
..Taifa limekosa MAADILI.

..mimi nilipomsikia "mtu fulani" anamsifia na kumtukuza GADDAFIddafi ambaye MIKONO YAKE INA DAMU YA WATANZANIA nilishangaa sana.

..sasa kama "mtu fulani" yuko hivyo unategemea watu wa kawaida watakuwa namna gani?
 
TUMEKUWA tukiandika kuhusu ni jinsi gani TBC na ubunifu wa kurusha matangazo ya kwa muda muafaka lanini hawbadiliki. Wajifunze kwa CNN jinsi walivyo sharp kurusha live matukio ya ghafla pindi yanapotokea(Breaking News)
 
Vyombo vyote vya habari hapa nchini ni matatizo. Tukio la jana la tetemeko ingekuwa wenzetu wangekesha usiku kucha kutuhabarisha. Huku ndio kwanza wanaweka taarabu. Hata Kenya wametuzidi sana. Startv inaweza kufanya coverage ya kampeni ya uchaguzi tu lakini sio matukio haya.
 
Mubelwa Bandio ambaye ni mtangazaj katika ktuo cha redio huko Washington DC amesema

"Nyie TBC. Mnataka tuuu tuseme.
Nyie si ndio kituo cha TAIFA?
Nyie si ndio mnaoendeshwa kwa kodi ya wananchi?
Nyie si ndio mnaotakiwa kuhabarisha kinachotokea kule ambako radio za kibiashara haziendi?
Si ni nyinyi mnaostahili kuwa WAZALENDO zaidi?
Nyie si ndio mnaotakiwa kuweka maslahi ya nchi mbele?
Nyie si ndio mnaotakiwa kufanya coverage ya MATUKIO YA KITAIFA?
Iweje mnapuuza TUKIO hili la tetemeko?
Watu 16 wanaingizwa uwanja wa Kaitaba sasa, mamia wameumia na dazeni za nyumba hazifai kwa makazi, mnaendelea na vipindi vya MUZIKI. Seriously????
Mmewapuuza wahanga wa tetemeko hili kubwa.
Na mnaendelea kusema mnahimiza UZALENDO?"
Mstue mwambie kipindi cha Taifa ni Clouds 360 na matamko yote yanapitia pale so atuache na tbc yetu
 
Mubelwa Bandio ambaye ni mtangazaj katika ktuo cha redio huko Washington DC amesema

"Nyie TBC. Mnataka tuuu tuseme.
Nyie si ndio kituo cha TAIFA?
Nyie si ndio mnaoendeshwa kwa kodi ya wananchi?
Nyie si ndio mnaotakiwa kuhabarisha kinachotokea kule ambako radio za kibiashara haziendi?
Si ni nyinyi mnaostahili kuwa WAZALENDO zaidi?
Nyie si ndio mnaotakiwa kuweka maslahi ya nchi mbele?
Nyie si ndio mnaotakiwa kufanya coverage ya MATUKIO YA KITAIFA?
Iweje mnapuuza TUKIO hili la tetemeko?
Watu 16 wanaingizwa uwanja wa Kaitaba sasa, mamia wameumia na dazeni za nyumba hazifai kwa makazi, mnaendelea na vipindi vya MUZIKI. Seriously????
Mmewapuuza wahanga wa tetemeko hili kubwa.
Na mnaendelea kusema mnahimiza UZALENDO?"
TV Mfu ya Taifa!
 
hee siku hizi mnaangalia TBC si mlisema haifai sasa mbona mapofu mengi,humueleweki kama nanihiiii
wananchi wanalazimika kutizama hiyo TBCcm maana wanalazimishwa kulipia chaneli za nyumbani (isipokuwa TBCcm ambayo labda iko nje ya nchi). na sirikali imeufyata kuhusu hili.
 
Back
Top Bottom