Test | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Test

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Viol, Dec 12, 2011.

 1. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #1
  Dec 12, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Swali la kwanza(marks 40)
  Jinsi ya kumwingiza simba ndani ya friji.
  Fungua friji halafu msukume ndani na ufunge mlango wa friji.

  Jinsi ya kumwingiza twiga ndani ya friji.
  Fungua friji na umtoe simba nje halafu msukume ndani twiga na ufunge mlango wa friji.

  Sasa ni mda wa wanyama wote/viumbe hai nchi kavu na majini kwenda kushiriki mashindano ya mbio huko msituni,
  mnyama ambaye hatashiriki ni twiga aliyefungiwa ndani ya friji.

  Swali inakuja.....kuna ziwa ambalo kuna mamba hatari na ngumu sana kuvuka hilo ziwa bila silaha,na unatakiwa uvuke bila silaha utafanyaje???

  Swali la pili (marks 40)
  Timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ina wachezaji 11,ilienda kucheza nchini Uganda.
  walipofika Uganda waliingia uwanjani,walipoingia uwanjani kulikuwa na mchezaji mmoja wa Tanzania ambaye anacheza
  namba 5,wakati anaingia uwanjani amevaa jezi kama wenzake,kavaa viatu,akavaa soksi.ile anaingia uwanjani
  refa akapiga filimbi ya kumrudisha nje ya uwanja.
  Je huyo mchezaji ana kosa gani??????

  Swali la tatu(marks 5)
  Kuku alipanda mlimani,halafu akaruka juu na kutema chini.
  je hayo mate yatadondokea chini au yataelekea juu?

  Swali la nne(marks 5)
  Ng'ombe ni watanzania ila huwa anaenda kula majani kenya,siku moja akazaa.
  huyo ndama atakuwa wa tanzania au wa kenya?

  Swali la tano(marks 10)
  Unatakiwa uvuke mpaka wa tanzania na kenya,kwa sheria iliyowekwa anayetoka tanzania haruhusiwi kwenda kenya.
  na wakenya harusiwi kwenda tanzania,na pale mpakani kuna mlinzi,unajua mda anaolala huyo mlizi ni sekunde 20,
  unatakiwa uvuke kwa huo mda mlinzi analala,tatizo ile unafika mda umeshaisha na mlinzi anaamka.
  sasa utafanyaje ili uvuke??
   
Loading...