Kwa kweli hii mambo yakuchangisha watu kwa ajili ya harusi yako inakereketa mnoo. Wewe una million moja unataka harusi ya million ishirini hii ni ujinga Sana, unaanza kusumbua watu weee mchongo mchongo Tena unawawekea watu na viwango vya lazima eti laki single chini ya laki hupewi kadi, I see hii kitu inaudhi Sana Sasa toa hata hiyo laki ushangae unachokikuta uko harusini ni ujinga mtupu vinywaji vi Tatu, na miwali Yao njegere na mi watermelon yakumwaga baada ya hapo mtacheza ule wimbo hakuna Mungu kama wewee, then kila mtu kwaoo! Jipange muoaji/muolewaji andaa harusi yako invite watu unaowataka wa maana kama Mia wa nguvu waje na zawadi basi tosha yaani mtu unajikuta una mi kadi ya harusi ofisini, nyumbani, kwenye gari yaani yametapakaa ukipiga hesabu ni Ada ya mwanao ya shule miaka miwili dah!