Elections 2010 Tendwa Unasemaje Magari ya Serikali Kutuma Kwenye Kampeni za CCM

Nsololi

JF-Expert Member
Mar 8, 2007
298
80
Je na kwa hili Wa TZ tutaambiwa Kikwete bado ni Rais kwa hiyo mali ya serikali lazima itumike na CCM kweni kampeni......Basi ni kwa namna gani chama tawala kitakatazwa kutumia resources za serikali katika shughuli zake, hasa kwenye kampeni??

Tunaomba waandishi wa habari wamfuate na kumhoji Mh Tendwa katika hili. Na ikibidi, vyama vya wapinzani waweke pingamizi kwenye tume ya Uchaguzi au iangaliwe namna namna ambavyo issue hii inaweza ikafikishwa mahakamani aidha na pressure group zingine au opposition parties.


Magari ya serikali yapamba kampeni za CCM


Thursday, 26 August 2010 06:57
Frederick Katulanda, Mwanza na Sadick MtulyLICHA ya sheria na kanuni za Uchaguzi kuzuia matumizi ya magari ya serikali, msafara wa mgombea urais wa CCM Jakaya Kikwete umetumia magari kadhaa ya serikali katika mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera.

Mbali na magari hayo, wakuu wa wilaya waliokuwa wameshiriki msafara wa mwenyekiti huyo wa CCM, walitumia magari yao ya kazi yakiwa yamewekwa namba binafsi huku wakivalia sare za chama hicho.

Ukiondoa magari maalumu ya walinzi wa mgombea huyo ambaye pia ni rais, magari mengine ya wakuu wa wilaya na wakuu wa idara mbalimbali za serikali, yalitumika na kuwekwa namba binafsi.

Kwa mujibu wa habari tulizozipata kutoka vyanzo vyetu zinaeleza kuwa hivi sasa Ikulu ya Dar es Salaam ina upungufu kwa kuwa wafanyakazi wa Ikulu hasa madereva pamoja na wapishi na wagawa vinywaji (waandazi), wanatumika katika kampeni za Rais Kikwete.

Wapishi na waandazi hao wamepelekwa mikoani kulingana na ziara za kampeni.

“Cha ajabu ni kuwa baadhi ya wafanyakazi wa Ikulu hasa madereva, wapishi na waandazi wanatumika katika kampeni za CCM kupitia Rais Kikwete.

“Wamegawanywa katika mikoa tofauti kulingana na ratiba za ziara za kampeni za rais,’’ kilisema chanzo chetu.

Juzi jijini Mwanza Mkuu wa wilaya Ilemela, Serenge Mrengo ambaye alifika majira ya saa 4:35 asubuhi uwanja wa ndege na gari lenye namba za STK 3551 huku wote wawili na dereva wake wakiwa wamevalia sare za CCM, lakini baada ya kusalimiana na viongozi wenzake, aliondoka.

Akiwa wilayani Geita, Mkuu wa wilaya hiyo Philemon Shelutete alitumia gari lake la serikali ambalo lilikuwa limebandikwa namba T 804 BCZ huku akiwa amevalia sare za CCM. Pia gari la Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Benson Katala lilitolewa namba za serikali na kubandikwa namba T 180 BKW.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro alitetea hatua hiyo akisema sio kosa kwa kuwa Kikwete bado ni rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanania.

Kandoro, alikiri kutumika kwa magari hayo ya serikali na kusema kuwa viongozi hao waliyatumia kumpokea na baadhi yao waliambatana naye katika ziara hiyo kwa kuwa mbali na kuwa mgombea wa CCM pia anayo hadhi ya urais.

“Huyu ni Rais, amekuja kama kiongozi licha ya kwamba anagombea, bado hajavuliwa urais, sasa ma-DC walikuja kama viongozi wa serikali kumpokea rais. Kama kuna mkuu wa wilaya alivaa shati la CCM alivaa kwa sababu ya mapenzi yake kwa chama,” alifafanua Kandoro ambaye alitumia gari binafsi la kiongozi mmoja wa CCM Kanda ya Ziwa.

"Makosa ni kiongozi wa serikali kufanya kazi za chama na sioni kama kuna kiongozi wa serikali ambaye alifanya kazi za chama,"alisema

Msafara wa Kikwete kuambatana na magari ya serikali haukuishia Mwanza na Geita pekee bali pia hata mkoani Kagera ambako magari mengi yalikuwa na namba za STK.

Katika hatua nyingine, uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando umetoa ufafanuzi kwamba uamuzi wake wa kutoa gari la kubebea wagonjwa katika msafara wa mgombea urais wa CCM kuhakikisha usalama wa mgombea huyo.

Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Dk Charles Majinge alisema kwa kawaida jukumu la kutoa magari huwa lipo mikononi mwa uongozi wa mkoa ambao uliomba gari kwao na wao waliamua kutoa gari hilo la wagonjwa namba T 848 AWN.

“Sisi hatutoi ambulance kwa wagombea, ila tulitoa kwa Kikwete kutokana na kuwa ni kiongozi wa nchi. Kutoa magari huwa ni kazi ya uongozi wa mkoa, lakini sisi kama watalaamu wa matibabu tulichukua tahadhari na kuweka gari hilo,” alieleza Dk Majinge.

Alisema kwa vile akiwa jijini Mwanza aliwahi kuanguka, basi waliamua kuchukua tahadhari kuepuka kukosa huduma haraka iwapo jambo hilo lingejirudia akiwa mbali na hospitali ya rufaa.

Akizungumzia gari hilo, Kandoro alisema uwapo wake ni utaratibu wa kawaida katika misafara ya viongozi wa serikali.

“Huu ni utaratibu wa kawaida katika misafara ya viongozi, tumetoa kama utaratibu wa kawaida….unajua huyu ni kiongozi wa nchi, sasa unataka wakija na wagombea wengine wa upinzani nao tuwapatie magari ya wagonjwa, wao ni akina nani?” alieleza na kuhoji Kandoro ambaye pia aligombea kura za maoni kuwania kuteuliwa na CCM kuwa mgombea ubunge Jimbo la Kalenga na kushindwa.

Akizungumza kwa sharti la kutotaja jina gazetini mmoja wa viongozi ambao walikuwa wakishughulika na kuratibu msafara huo alieleza kuwa gari hilo la wagonjwa ni lile ambalo lilitolewa na serikali ya Ujerumani chini ya ushirikiano wa Jiji la Mwanza na Wurzburg.

“Gari hili liliandaliwa kutokana na maofisa wa usalama kuliomba na hili agizo limetolewa katika mikoa yote ambako atafika, kwani katika kampeni anakuwa amekwenda hadi katika wilaya ambazo haina hospitali na ikitokea dharura akimbizwe haraka hospitali huku akiendelea kupatiwa matibabu” alieleza kiongozi huyo wa chama.

Hata hivyo, alisema gari hilo wao kama chama hawakuambiwa wala kuelekezwa kulilipia kwa vile ofisi ya mkoa ilisema watachukua wao katika hospitali ya Bugando, baada ya kuwasiliana na ofisi ya mganga mkuu wa mkoa.
 
Akina Kandoro na wengine wote ni vibaraka tu wanaopalilia ulaji wao. Kama kweli kuna sheria hapa ndo pa kumuwekea pingamizi Kiwete kulingana na sheria mpya ya gharama za uchaguzi
 
What matters is your mind-set, that is, the kind of vote which you are going to cast on the election day!...Naamini ni watu wachache sana wanaobadilishwa na aina ya kampeni ya mgombea!
 
kwa unafiki wao, sidhani kama watatoa jibu la maana hapa. Sana sana watamleta Salva aje kutoa maelezo marefu kuwa Kikwete sio mgonjwa (na kukwepa swali la msingi hapa) etesetera etesetera
 
Jamani, sidhani kama hii ni kazi ya msajili wa vyama, ukiacha kazi zake chini ya sheria ya vyama ambayo ni: kutoa usajili wa muda, kutoa usajili wa kudumu, kufuta chama, kusimamia ruzuku toka serikalini kwenda kwenye vyama, kusimamia na kuratibu gharama za matumizi ya vyama chini ya sheria ya gharama za uchaguzi. Kwa kweli sioni kazi nyingine, wangemwita "toothless bulldog"
 
Jamani, sidhani kama hii ni kazi ya msajili wa vyama, ukiacha kazi zake chini ya sheria ya vyama ambayo ni: kutoa usajili wa muda, kutoa usajili wa kudumu, kufuta chama, kusimamia ruzuku toka serikalini kwenda kwenye vyama, kusimamia na kuratibu gharama za matumizi ya vyama chini ya sheria ya gharama za uchaguzi. Kwa kweli sioni kazi nyingine, wangemwita "toothless bulldog"

Na huenda utashangaa kukuta kufuatana na jinsi sheria zetu zinavyotungwa na wasanii, haisemi ni nani mwenye jukumu la kusimamia hii!!!!
 
Back
Top Bottom