Tendwa awa msemaji wa CCM; aishambulia CHADEMA

Tendwa awa msemaji wa CCM; aishambulia CHADEMA

bullet proof

Member
Joined
Sep 19, 2012
Posts
57
Reaction score
35
Leo katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na ITV, mzee John Tendwa ambaye ni msajili (mlezi) wa vyama vya siasa nchini amekosoa harakati mbalimbali za kisiasa zinazoendeshwa na CHADEMA nchini na kusema kuwa hazina tija zaidi zinachochea vurugu.

Kuhusu 'Operation sangara' ameikosoa akisema CHADEMA wameharakisha kufanya hivyo kwamba watachoka kabla ya uchaguzi hivyo kuifanya kutokuwa na manufaa yoyote. Kuhusu M4C, bila kufafanua vizuri, amesema haina tija yoyote kwani haijaandaliwa vizuri kwa vile CHADEMA wamekurupuka!

Binafsi namshauri mzee Tendwa afanye kazi yake ya usajiri na ulezi wa vyama vya siasa. Wananchi tumeona jinsi M4C na operation sangara zinavyowaamsha watanzania kujua na hatimaye kudai haki zao juu ya matumizi sahihi ya rasilimali za taifa.
 
Uyo mzee anazeeka vibaya sasa.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Kama ndo hivi tendwa anatendwa na masisiem,fanya kazi yako mzee la si hivyo utaadhirika na mziki huu wa vujana....
 
Si ilishasemwa kuwa alikwishafikia retirement age miaka 2 iliyopita??? Au ndiyo analipa fadhira za kubakizwa ofisini. Aangalie aside fia kazini!!!!
 
Ni lazima awe anahaha kujaribu kuikosoa CHADEMA kwani kikiendelea na moto huo, 2015 ndo mwisho wa kibarua chake!
 
Huyu ni msemaji wa sisimweli!
 
Anaendekeza siasa za kichovu. Nasikia anatumia viagra za ku-boost akili yake iliyokwisha choka!
 
Kila mtu anavurunda kwenye nafasi yake?

Swali,hii nchi tunaipeleka wapi?

Viongozi hawa busara iko wapi?

Tendwa wewe ni kama mlezi wa vyama vya siasa hapa nchini, sasa kwa matamshi haya tukueleweje?

Nini faida ya kuwa na wazee kama nyinyi katika taifa?
 
Kweli ukishangaa ya mizengwe iliyopinda utayaona ya mtenda hutendwa. Hivi tangu lini magambaz wakaitakia mema CHADEMA?
 
Si walisema vyama vya msimu??

Hofu kuu imewakamata na hawajui wamkabe nani maana mashambulizi sasa yanatoka kila upande na bila kelele nyingi
 
Mie kila siku huwa nashangaa inakuwakuwaje Mtu kama huyu asiyedhibiti ukereketwa wake juu ya CCM, aendelee kuishi Kama msajili wa VYAMA?!??.. Nchi hii?
 
Mzee Tendwa wewe sio ujione ni mtaalamu sana juu ya masuala ya vyama vya siasa kuliko Watz wengine,kwa taarifa yako hata huku CHADEMA wapo pengine wanauelewa kuliko wewe,tena unawajua fika.LEO LANGU MOJA TU katika kukukosoa mzee wangu Tendwa,nalo ni SI KWELI UNAPOSEMA KWAMBA CHADEMA KITACHOKA MAPEMA KWA MIPANGO YAKE YA OPERATION SANGARA NA M4C,LABDA NIKUPE MFANO MZEE TENDWA,OPERATION SANGARA ILIPELEKEA CHADEMA KU-MULTIPLY[DATA UNAZO HAPO OFISINI],KADHALIKA TANGU MWAKA 1995 MPAKA MWAKA 2010 UMETHIBITISHA KWAMBA CHADEMA NI PROGRESSIVE[PROSPER] PARTY.SASA naomba UKIRI mwenyewe mipango ya CHADEMA NI KABAMBE NA ENDELEVU,KINYUME CHA HAPO MZEE TENDWA UNAKIUA CCM KI-PSYCHOLOGY Kwani unafahamu nini maana ya"HAKUNA KULALA,HAKUNA KULA NA HAKUNA KUNYWA MPAKA KIELEWEKE NDANI YA M4C"MUNGU AJUJAALIE NEEMA NDOGONDOGO NA NEEMA KUBWAKUBWA UFIKE NA UJIONEE MWAKA 2015. I AM MISSING MWL J.K NYERERE.
 
Leo katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na ITV, mzee John Tendwa ambaye ni msajili (mlezi) wa vyama vya siasa nchini amekosoa harakati mbalimbali za kisiasa zinazoendeshwa na CHADEMA nchini na kusema kuwa hazina tija zaidi zinachochea vurugu.

Kuhusu 'Operation sangara' ameikosoa akisema CHADEMA wameharakisha kufanya hivyo kwamba watachoka kabla ya uchaguzi hivyo kuifanya kutokuwa na manufaa yoyote. Kuhusu M4C, bila kufafanua vizuri, amesema haina tija yoyote kwani haijaandaliwa vizuri kwa vile CHADEMA wamekurupuka!

Binafsi namshauri mzee Tendwa afanye kazi yake ya usajiri na ulezi wa vyama vya siasa. Wananchi tumeona jinsi M4C na operation sangara zinavyowaamsha watanzania kujua na hatimaye kudai haki zao juu ya matumizi sahihi ya rasilimali za taifa.
Nimeangalia [ia kipindi hiki na kwa kweli bado tuko mbali na Mzee ameshindwa kufichwa ukereketwa wake.
Kuna mambo yanaweza yakawa kweli lakini hayatakiwi yasemwe na yeye na kama anataka kuonyesha ULEZI wake ilitakiwa awzungumzie viongozi/vyama vyote.Leo Shonza na Mwampamba wanaeneza ukabila na ukanda lakini hakuna anayekemea as long as inawagusa CDM.
 
Thanks mwambie bap 2 ametumwa kila siku natabiria cdm kufa au kuchoka atakufa yeye na ataiacha cdm
 
Tatizo anafanya kazi ya chama tawala na anafikiria kwa kutumia masaburi. Kama anafikiri Chadema itachoka na hizo Operation Sangara na M4C basi ajue amechoka kufikiri na akili yake inaonyesha jinsi gani alivyonyembamba kwa kufikiri. Operation Sangara ndio iliopelekea Chadema kupngeza idadi ya wabunge wake ndani bunge mwaka 2010. Tena wabunge wake wamechaguliwa kihalali na ndio maana mpaka sasa hakuna mbunge hata mmoja wa Chadema aliyevuliwa ubunge kwa kutumia rushwa au kukiuka taratibu za uchaguzi mpaka sasa. Ni ule ubunge wa Leme walitaka kuchakachua bila mafanikio yoyote na bado wanangangania kutaka kuchakachua. Yeye badala ya kuzungumzia kwa nini wabunge wengi wa CCM wamekutwa na makosa ya kukiuka utaratibu wa uchaguzi na kujikuta wamepoteza nafasi zao za uchaguzi na kuliingizia Taifa gharama kubwa za kurudia uchaguzi. Istoshe ofisi yake imekaa kimya pasipo kutangaza tarehe za kunza kampeni kwa ajili ya uchaguzi kama vile Igunga na maeneo mengine. Atajitetea kuwa wamekata rufaa kama ile ya Igunga ambapo Rage alionekana wazi akihutubia mkutano huku akiwa na silaha kiunoni kinyume nataratibu za uchaguzi. Yeye ajue kabisa his days are numbered na itabidi akakamuliwe hizo chunisi huko usoni chini India manake zimefikia ukubwa wa kitovu cha mtoto wa miaka 10.
 
Leo katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na ITV, mzee John Tendwa ambaye ni msajili (mlezi) wa vyama vya siasa nchini amekosoa harakati mbalimbali za kisiasa zinazoendeshwa na CHADEMA nchini na kusema kuwa hazina tija zaidi zinachochea vurugu.

Kuhusu 'Operation sangara' ameikosoa akisema CHADEMA wameharakisha kufanya hivyo kwamba watachoka kabla ya uchaguzi hivyo kuifanya kutokuwa na manufaa yoyote. Kuhusu M4C, bila kufafanua vizuri, amesema haina tija yoyote kwani haijaandaliwa vizuri kwa vile CHADEMA wamekurupuka!

Binafsi namshauri mzee Tendwa afanye kazi yake ya usajiri na ulezi wa vyama vya siasa. Wananchi tumeona jinsi M4C na operation sangara zinavyowaamsha watanzania kujua na hatimaye kudai haki zao juu ya matumizi sahihi ya rasilimali za taifa.

Kelele za John Tendwa mteule wa Rais Kikwete zitanyamazishwa na Katiba Mpya ifikapo 2014.
Pambaf zake!
 
Back
Top Bottom