msajili wa vyama vya siasa nchini bw. john tendwa amesema aliyekuwa mbunge wa kishapu kwa tiketi ya ccm bw. fred mpendazoe amekurupuka katika uamuzi wake wa kukihama chama chake cha zamani na kujiunga na chama ambacho hadi sasa si halali kisheria na hakitambuliwi na ofisi yake wala hakimo katika orodha ya vyama vya siasa Tanzania inayopatikana ofisini kwake. akihojiwa na waandishi wa habari waliofika ofisini kwake kupata msimamo wake kufuatia hatua ya mbunge huyo machahari kujiengua kutoka ccm, tendwa alisema kwa kifupi " ametumia uhuru wake kikatiba vibaya"
msajili huyo alifafanua kuwa sheria ya vyama vya siasa nchini hairuhusu chama kutangaza kushiriki uchaguzi mkuu hadi kitakapokuwa kimepata usajili wa kudumu. kutokana na kuwepo ushahidi wa kutosha kuwa CCJ kimepanga kushiriki uchaguzi ujao, alisema ofisi yake inatafakari hatua za kuchukua dhidi ya chama hicho kilichojizolea umaarufu kwa muda mfupi ikiwemo kukifuta katika daftari lake. aidha aliongeza kuwa anaweza kutumia mamlaka aliyonayo kisheria kumpiga marufuku ndg. mpendazoe kugombea nafasi yoyote ya kisiasa katika uchaguzi ujao kutokana na kutangaza hadharani kuwa atagombea kupitia chama ambacho halijasajiliwa. akisistiza hoja yake hiyo aliahidi leo kukutana na waandishi wa habari ofisini kwake kutolea ufafanuzi zaidi juu ya msimamamo wa kisheria katika suala kam hilo;
my take:
embu wajuvi wa sheria ya vyama vya siasa nchini mtufafanulie msingi wa madai haya ya bw, Tendwa.
msajili wa vyama vya siasa nchini bw. john tendwa amesema aliyekuwa mbunge wa kishapu kwa tiketi ya ccm bw. fred mpendazoe amekurupuka katika uamuzi wake wa kukihama chama chake cha zamani na kujiunga na chama ambacho hadi sasa si halali kisheria na hakitambuliwi na ofisi yake wala hakimo katika orodha ya vyama vya siasa Tanzania inayopatikana ofisini kwake. akihojiwa na waandishi wa habari waliofika ofisini kwake kupata msimamo wake kufuatia hatua ya mbunge huyo machahari kujiengua kutoka ccm, tendwa alisema kwa kifupi " ametumia uhuru wake kikatiba vibaya"
kwamba: inatafakari hatua za kuchukua dhidi ya chama hicho kilichojizolea umaarufu kwa muda mfupi ikiwemo kukifuta katika daftari lakemsajili huyo alifafanua kuwa sheria ya vyama vya siasa nchini hairuhusu chama kutangaza kushiriki uchaguzi mkuu hadi kitakapokuwa kimepata usajili wa kudumu. kutokana na kuwepo ushahidi wa kutosha kuwa CCJ kimepanga kushiriki uchaguzi ujao, alisema ofisi yake inatafakari hatua za kuchukua dhidi ya chama hicho kilichojizolea umaarufu kwa muda mfupi ikiwemo kukifuta katika daftari lake.
Hana mamlaka hayo; ajaribu!aidha aliongeza kuwa anaweza kutumia mamlaka aliyonayo kisheria kumpiga marufuku ndg. mpendazoe kugombea nafasi yoyote ya kisiasa katika uchaguzi ujao kutokana na kutangaza hadharani kuwa atagombea kupitia chama ambacho halijasajiliwa.
Hana uwezo huo!akisistiza hoja yake hiyo aliahidi leo kukutana na waandishi wa habari ofisini kwake kutolea ufafanuzi zaidi juu ya msimamamo wa kisheria katika suala kam hilo;
my take:
embu wajuvi wa sheria ya vyama vya siasa nchini mtufafanulie msingi wa madai haya ya bw, Tendwa.
Jamani wakati mwingine muwe mnasoma mnavyoandika; internal contradictions zina assume wote humu hamnazo!
kwamba chama ambacho hadi sasa si halali kisheria na hakitambuliwi na ofisi yake wala hakimo katika orodha ya vyama vya siasa Tanzania inayopatikana ofisini kwake
Halafu:
kwamba: inatafakari hatua za kuchukua dhidi ya chama hicho kilichojizolea umaarufu kwa muda mfupi ikiwemo kukifuta katika daftari lake
Mtu mwenye akili atauliza: Unaweza vipi kufuta chama kutoka kwenye daftari ambalo umesema hakimo?
Hana mamlaka hayo; ajaribu!
Hana uwezo huo!
Ni ya kipuuzi haya msingi katika mantiki na yanathibitha kuwa April Fools bado ipo hai!
ha ha ha kazi hipo.hiki chama kweli kitasajiliwa ? manake inaonekana kinawakosesha wengi sana usingizi.
sasa john tendwa wewe shida yako hiko wapi kama kafanya uwamuzi kwa kukurupuka?
poleni sana wanaJF mlioingia mkenge. siku nyingine kabla ya kuposti chochote, fungueni kwanza kalenda muone ni tarehe ngapi
Tanzania kila siku ni siku ya wajinga, Watanzania tunadangaywa vya kweli mpaka tumepewa jina wadanganyika, tunakaa kimya hatuchekwi mimi naona ingekuwa the other way round. Tushupae na kushituka tunavyodanganywa siku zingine leo tuwe relaxed tukubali kudanganywa kama alivyofanya mwanakijiji.