Tendwa aionya tena CHADEMA...

Mzee wa watu lazima ajikombe kwa maccm,vinginevyo watasitisha mkataba wake wa kibarua maana muda wake umekwisha.Tanzania ya leo hata kama umesoma ili maccm yakupenda lazima uwe mnafiki kama maccm.
 
Ameshikwa pabaya anaweweseka kwani anaona giza mbele ktk maisha yake yanayoelekea kukoma siku za karibuni hapa duniani.ROHO YA MAREHEMU MTARAJIWA JONI WA KUTENDWA IPATE REHEMA KWA SHETANI IPUMZIKE KWA MISUKOSUKO.
 

Nimesoma weeee..... nimekarudiarudia weeee..... naona madudu tu.
 
Wakati mwingine unajiuliza kwa nini watanzania ni mabingwa wa kukwepa kodi....sababu ni matumizi mabaya ya kodi yenyewe kama inavyotumika vibaya ktk ofisi ya huyu mzee.
 
Hiki ni kizazi cha dotcom ukimwaga mboga namwaga ugali na kama ni mbwai mbwai unatakiwa kujitetea mwenyewe kabla ya kutafuta mtetezi wako.hapo busara za babu Tendwa hakuna hata Taifa ambalo halina jeshi ni rahisi kuvamiwa lakini adui anapofahamu kuna jeshi inakuwa vigumu kukuchokoza. Babu acha kutumika na sisiemu
 


Tendwa amekubali kutumika ndani ya siasa ya ccm acha avue aibu
 
Wazazi ya zamani nachanganya, walimu dasarani nachanganya, kwa uzushi, na maneno mbofu mbofu! 01-Mr. Ebbo - Maneno Bofu Bofu - YouTube
 
Haha ha bora angekaa kimya tu.Amechanganyikiwa.Haturudi nyuma

Nashauri Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa ialikwe kwenye makambi ya mafunzo kusudi ijiridhishe na yanayoendelea huko.

No research no right to speak. Tendwa anatunga maneno halafu anayatolea matamko. Namna hii hatuwezi kufika

cb
 
Kawaida watu hatuangalii mtu alianzaje bali alimalizaje, huyu mzee anamalizia vibaya uzee wake. Hata -------- hawezi kuwekewa ushahidi wa wazi kama picha na vielelezo mbalimbali jinsi Green Guard wanavyofanya akajifanya havioni na kang'ang'ania mawazo au maoni ambayo hata hayajaanza kufanyiwa kazi!

Pia kama watalaamu wa majina na wanazuoni wa dini mbalimbali wanavyosema, jina huwa linaweza kutafsiri tabia ya mtu! Hivyo CCM wametumia mwanya huo wa kuweza kumtenda John ili awe msemaji wake. Huyu ametendwa kirahisi kwa sababu jina lake lina ruhusu kufanyiwa hivyo! Sasa sishangai anapokosa busara na kuanza kuitisha CDM ambayo haijaanza kutekeleza mipango yake ya kujilinda na kuwaacha Green Guard (Mungiki ya Tanzania) wanao ua na kuumiza watu! Kila mara vyombo vya habari vianatangaza Mh. Mbunge Nassari alipigwa na kujeruhiwa na Green Guard, kwanini hili halikemei?
 
Tendwa ni kati ya wazee ambao bila shaka ameshaingiliwa na magonjwa ya uzee, na ni mwana-CCM hai kwa hivyo ukimuuliza kambi za CCM zilizokuwa zinaonyeshwa dhahiri na green guard kubeba silaha kubwa, bunduki na nyinginezo atasema hakuambiwa!! au atasema CCM hawazitumii, walikuwa wamebeba kama geresha tu! akiulizwa kwanini Green Guard wanatumia nguvu kuteka kupiga, kung'a kucha na meno na kuua wanaharakati na wanachama wa vyama vingine atasema hajawahi kusikia??

Tendwa ni kati ya viongozi hovyo..wanaojilamba-lamba, na wasio na direction ya kusimamia hali na maendeleo ya demokrasia kwa tanzania au taifa lolote changa...! hii siyo mara ya kwanza kwa Tendwa kujiuma-uma, anaona taifa ni kama kambi ya kuku au mifugo ya kuswaga bila kufikiria! Kwa kawaida huyu jamaa ni mwoga, mnafiki na mla-kuwili (double std), ndio maana kampa msaidizi wake kuwasilisha tamko, maana alijua wana-habari wasio makanjanja wangemuuliza maswali mengi, angeanza kutetema!

Chadema inatakiwa kumpuuza Tendwa kwa kila asemalo dhidi yao hadi apate akili mpya, na ikiwa hapati akili, awekwe ktk agenda ya watu ambao wanaua demokrasia, 'anailea' CCM na magaidi wao waliojaa ktk kambi za mafunzo ya Green Guard. "Demokrasia Tz bila Tendwa -- inawezekana vyema sana", kama ilivyo "Tanganyika mpya bila CCM inawezekana mapema sana!"
 
nimesikia anaendeshwa na nguvu ya whisky
Labda kama amehamia huko ila huyu mzee ni noma kwa viroba,umri huo anaendekeza ulevi ovyo kabisa halafu anapewa kazi nyeti kama hiyo na njaa nayo inamnyemelea akitoka tu kwa hiyo ofisi kwishney,atabaki historia tu.
 
huyu babu kavurugwa sasa kama mtu anamfanyia fujo ataenda polisi kwanza bila kujitetea? na kwa dunia ya sasa huwezi kujitetea bila kuwa fiti babu kwa ujumla wake kavurugwa. VIVA CDM VIVA M4C

Huyu John Tendwa anasumbuliwa na Bingo ya Lukuvi ya Milioni 100!
Alivoshupalia swala la Red Brigade inaonyesha kabisa kuwa kuna msukumo nyuma yake wa Serikali ya CCM!

Huwezi kuwa Msajili wa Vyama vya siasa na ukawa unafanya kazi kwa mtindo wa "Double standard"! Kusema kuwa sheria hairuhusu vikundi vya ukakamavu na wakti huohuo CCM wana kikundi cha Greenguard kinacholinda Vigogo wa CCM ni unafiki na ushabiki wa kipumbaf uliopitiliza mipaka.

Ni bora Tendwa akanyamaza kimya na kuachana kabisa na hoja hii inayozidi kumdhalilisha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…