Bahati haina kwao,
Popote inathibiti.
Ili niwe na upeo,
Nasubiri siipati.
Moyo nimesema nao,Isipokua sijuti.
Sihusudu wapatao,
Ingawa mimi sipati.
Toka kale hadi leo,
Naingoja haizuki.
Ni kwenye watafutao,
Naomba kila wakati.
Moyo wangu wenda mbio,Wachoka kwa harakati.
Ni kwenye wasubirio,
Tena tamaa sikati.
Basi sema nao hao,wajifanyao biyuti.
Wasitese wenziwao,
Wakawa watusaliti.
Uumiao ni moyo,
Na mwisho wake mauti!