Hii barua ya mtendaji inanitambulisha NIDA au popote nchini, Ikiwa barua ya mtendaji ni muhimu kiasi hicho kwanini wanapuuzwa na hawalipwi vizuri kama wabunge? sasa mtu akiwa gaidi akamtishia huyu mtendaji uhai wake na kumalzimisha amuandikie barua hiyo ili apewe passport au cheti cha uraia,serikali itakuwa imejikingaje na hili la raia fake? Na vipi akihongwa vizuri ili atoe barua hiyo kwa mtu asiye mtanzania na akafanya hivyo, huoni itakuwa ni tatizo la serikali kuwapa majukumu makubwa hawa watu halafu malipo yao kiduchu, au ndio wameambiwa wawe wazalendo tu, na huo uzalendo unaliwa?