Temeke: Viongozi 15 upinzani wahamia CCM

Aliyenishangaza kuliko wote ni Mtatiro! I thought he had substance but njaa haichezi 🙂 🙂!!!!!
 
HUYO MAKYEMBE NI KIAZI SANA NI DIWANI ZOBA SIJAWAH KUONA ANATOA SABABU ZAKIDUANZI MTONI KWA AZIZ ALI HUKU PAMEMSHINDA ANAKWENDA HUKO ARUDI TENA KUPITIA KIJANI AAACHE UBWEGE
..
..
TUTAMSRATCH KORODANI
Alafu anajifanya mpambanaji kumbe hna lolote.....Kuna siku nlikutana yuko na ki raum chke nlimpa makavu

Ova
 
Viongozi 15 upinzani wahamia CCM

VIONGOZI 15 kutoka upinzani wilayani Temeke, wamekabidhi kadi zao kwa Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamphrey Polepole, baada ya kuvihama vyama vyao na kuhamia chama hicho tawala.

Hafla hiyo ya kupokea viongozi hao wa upinzani ilifanyika juzi na kuhudhuriwa na wanachama wa CCM. Diwani wa Mtoni kwa Azizi Ally, Benard Mwakyembe aliyekuwa Chadema na kuingia CCM, ameahidi kurudisha CCM viti vyote vilivyokua upinzani.

"Nilikua napambana sana na Meya Abdallah Chaurembo, zaidi ya mara 10 tumekosakosa kutwangana makonde kwenye vikao vya madiwani, nimepambana sana na DC sasa nitapambania maendeleo ya wana Temeke, uchaguzi ujao nitagombea naomba wana Temeke msiniangushe," alisema.

Mbali na diwani huyo, Katibu Mwenezi wa ACT- Wazalendo ambaye amewahi kuwa Ofisa Uchaguzi Chadema kabla ya kutimkia ACT-Wazalendo, Steven Shekumkae akinukuu vifungu vya biblia, alidai ameoteshwa na Mungu arejee CCM.

"Mungu aliniotesha ule mstari wa enendeni mkaihubiri injili anayeamini ataokoka, mimi nimeokoka, nimezaliwa upya na wenzangu hali kadhalika sasa tukaitangaze CCM kwa mataifa yote," alisema.

Wengine waliorudisha kadi zao na nafasi zao kwenye mabano ni Amina Batash (Katibu ACT –Wazalendo Pwani, mjumbe Halmashauri Kuu), Abdul Kheri (Katibu Chadema kata ya Chang'ombe), John Matugura (Mwenyekiti Chadema Tuangoma), Charles Gahu ( Katibu kata na Mwenyekitu Bavicha Wilaya ya Temeke).

Said Mohamed (Chadema), James Nyaki ( Mwenyekiti Chadema Kata ya Kurasini), Mohammed Saidani (Chadema), Thomas Elius (Katibu Mwenezi kata ya Mtoni), Juma Said (Chadema) na Kelvin Abiud ( Mwenyekiti vijana ACT Wilaya ya Temeke).

Aidha, Edith Sebastian ( ACT baraza la wadhamini taifa), Ally Mbonde( Katibu wa Cuf, kata ya Tuangoma) na Renatus Lipambile (Mwenyekiti Chadema kata ya Kijichi) nao pia walihama vyama vyao na kutimkia CCM.

Akipokea kadi za wanachama hao wapya, Polepole aliwataka wana CCM kuwapa ushirikiano wanachama hao wapya na kuongeza kuwa bado nafasi zipo kwa watakaotaka kurejea wafanye hivyo kabla ya kufunga dirisha la usajili Desemba 31 mwaka huu.

"Kadi milioni mbili mpya zimeshawasili na Dar es Salaam peke yake kadi 13,000 zimeshatolewa,” alisema.

Meya wa Temeke Abdallah Chaurembo kwa tiketi ya CCM alisema kuwa Temeke ina majimbo mawili Mbagala na Temeke, na katika hayo Temeke ina kata 13 , CCM kata saba na upinzani kata sita.

Wakati Mbagala kuna kata 10 CCM kata saba na upinzani kata tatu zote zikiwa za CUF, serikali za mitaa jumla ni 142, CCM mitaa 102, upinzani 40 kwa Wilaya yote ya Temeke. Kampeni za madiwani na ubunge zinatarajiwa kuanza Novemba 4, kata 26 zitagombewa, wakati ubunge majimbo yatakayowaniwa ni Simanjiro, Serengeti na Babati.
Hawa hawaandiki zile barua ?
 
Hii ni kucheza Biko, nafasi zao wote hapo baadae zitakuwa za wana ccm damu then BunGeni mambo yanakuwa ni ndio mzee
 
Alafu anajifanya mpambanaji kumbe hna lolote.....Kuna siku nlikutana yuko na ki raum chke nlimpa makavu

Ova
Hawajui mbele ya tamaa, kuna mauti.. Huyu dogo namfahamu sana.. Naomba Mungu tu aniweke come 2020, nione wakivuna malipo ya usaliti wao..
 
Wasepe tu, kwenye msafara wa mamba na kenge wamo...And when the going gets tough ONLY the tough get going.
 
Mi nasubilia 2020 watakavyoduwazwa,saiz wanachekewa chekewa nakugombea tena, binafsi naona 2020 watapambana na hali yao cos wapo wanaccm walioanza kujipanga tangu 2015 baada ya uchaguzi tu,mfano jimboni kwetu kwa mujibu wa diwani ambaye nipo naye karibu watia nia wamefikia saba wanaopenya penya kwa madiwani,so nadhani wanao hama wanajimaliza kisiasa kabisa
Kwani umeambiwa wanakuja ccm ili wapate madaraka
 
Mwisho wa mchezo mzima ni mwenye chama kufuta saccos yake walahi
 
Nimesema na nina nena tena CHADEMA KWISHNEY KABISA WALAHI
 
Mwisho wa mchezo mzima ni mwenye chama kufuta saccos yake walahi
Ila kweli ukiwa fisiem lazima ushikiwe ubongo na huruhusiwi kabisa kuongea ile kweli, sasa kama CHADEMA inafutika mbona mnatumia nguvu kubwa mno kupambana nayo?

Figisu mnaanzia kwenye kuchukua form, mkishindwa mnaweka Figisu kwenye kurudisha, mkishindwa kwenye kurudisha mnabadirisha matokeo mnatangaza aliyeshindwa, FISIEM. Mmelaaniwa walahi.
 
Alafu anajifanya mpambanaji kumbe hna lolote.....Kuna siku nlikutana yuko na ki raum chke nlimpa makavu

Ova
KUMBE MKUU UNAMPATA JUZI KATI NILIMWONA KWENYE MKUTANO MMOJA MAENEO YA KWA AZIZ WA CCM NKAWA NAMCHEKA TU
 
Kweli wewe ni ndege John

Back
Top Bottom