Temeke: Viongozi 15 upinzani wahamia CCM

Temeke: Viongozi 15 upinzani wahamia CCM

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
24,801
Reaction score
60,645
Viongozi 15 upinzani wahamia CCM

VIONGOZI 15 kutoka upinzani wilayani Temeke, wamekabidhi kadi zao kwa Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamphrey Polepole, baada ya kuvihama vyama vyao na kuhamia chama hicho tawala.

Hafla hiyo ya kupokea viongozi hao wa upinzani ilifanyika juzi na kuhudhuriwa na wanachama wa CCM. Diwani wa Mtoni kwa Azizi Ally, Benard Mwakyembe aliyekuwa Chadema na kuingia CCM, ameahidi kurudisha CCM viti vyote vilivyokua upinzani.

"Nilikua napambana sana na Meya Abdallah Chaurembo, zaidi ya mara 10 tumekosakosa kutwangana makonde kwenye vikao vya madiwani, nimepambana sana na DC sasa nitapambania maendeleo ya wana Temeke, uchaguzi ujao nitagombea naomba wana Temeke msiniangushe," alisema.

Mbali na diwani huyo, Katibu Mwenezi wa ACT- Wazalendo ambaye amewahi kuwa Ofisa Uchaguzi Chadema kabla ya kutimkia ACT-Wazalendo, Steven Shekumkae akinukuu vifungu vya biblia, alidai ameoteshwa na Mungu arejee CCM.

"Mungu aliniotesha ule mstari wa enendeni mkaihubiri injili anayeamini ataokoka, mimi nimeokoka, nimezaliwa upya na wenzangu hali kadhalika sasa tukaitangaze CCM kwa mataifa yote," alisema.

Wengine waliorudisha kadi zao na nafasi zao kwenye mabano ni Amina Batash (Katibu ACT –Wazalendo Pwani, mjumbe Halmashauri Kuu), Abdul Kheri (Katibu Chadema kata ya Chang'ombe), John Matugura (Mwenyekiti Chadema Tuangoma), Charles Gahu ( Katibu kata na Mwenyekitu Bavicha Wilaya ya Temeke).

Said Mohamed (Chadema), James Nyaki ( Mwenyekiti Chadema Kata ya Kurasini), Mohammed Saidani (Chadema), Thomas Elius (Katibu Mwenezi kata ya Mtoni), Juma Said (Chadema) na Kelvin Abiud ( Mwenyekiti vijana ACT Wilaya ya Temeke).

Aidha, Edith Sebastian ( ACT baraza la wadhamini taifa), Ally Mbonde( Katibu wa Cuf, kata ya Tuangoma) na Renatus Lipambile (Mwenyekiti Chadema kata ya Kijichi) nao pia walihama vyama vyao na kutimkia CCM.

Akipokea kadi za wanachama hao wapya, Polepole aliwataka wana CCM kuwapa ushirikiano wanachama hao wapya na kuongeza kuwa bado nafasi zipo kwa watakaotaka kurejea wafanye hivyo kabla ya kufunga dirisha la usajili Desemba 31 mwaka huu.

"Kadi milioni mbili mpya zimeshawasili na Dar es Salaam peke yake kadi 13,000 zimeshatolewa,” alisema.

Meya wa Temeke Abdallah Chaurembo kwa tiketi ya CCM alisema kuwa Temeke ina majimbo mawili Mbagala na Temeke, na katika hayo Temeke ina kata 13 , CCM kata saba na upinzani kata sita.

Wakati Mbagala kuna kata 10 CCM kata saba na upinzani kata tatu zote zikiwa za CUF, serikali za mitaa jumla ni 142, CCM mitaa 102, upinzani 40 kwa Wilaya yote ya Temeke. Kampeni za madiwani na ubunge zinatarajiwa kuanza Novemba 4, kata 26 zitagombewa, wakati ubunge majimbo yatakayowaniwa ni Simanjiro, Serengeti na Babati.
 
Uhuru ni wao na ningependa kusika wengi zaidi ya hao wanahamia upande wanaopingana nao kwa sasa walipo.

Wapo sahihi ila wasiseme uongo tu hapo ndipo wanaponiuzi.

Waseme ukweli tu mimi msaka tonge nimehama kwa kuwa natamani kuwa mkubwa zaidi ya hapa, kunenepa zaidi ya hapa, madaraka zaidi ya haya na huku niliko hakuna matumaini katika uongozi huu wa awamu ya tano upinzani kufurukuta by any means. Hivyo nimeamua kuhamia nitakapo pata mahitaji yangu kwani siasa ni kazi kama kazi nyingine.
 
HUYO MAKYEMBE NI KIAZI SANA NI DIWANI ZOBA SIJAWAH KUONA ANATOA SABABU ZAKIDUANZI MTONI KWA AZIZ ALI HUKU PAMEMSHINDA ANAKWENDA HUKO ARUDI TENA KUPITIA KIJANI AAACHE UBWEGE
..
..
TUTAMSRATCH KORODANI
 
He he heh e
Wanasiasa bana

Eti kaoteshwa na Mungu arudi CCM.
Mungu hadhihakiwi ujue.
Hugo jamaa analeta upumbavu tena wa kijinga. Mungu na siasa za kipuuzi wapi na wapi. Wanataka kubadili gia ya kijinga ya "kuunga mkono mtukufu" sasa iwe ni Mungu Mtakatifu kawashauri.!!!! Bila shaka hawa wanataka kufa vibaya na vizazi vyao vyote.
 
Mi nasubilia 2020 watakavyoduwazwa,saiz wanachekewa chekewa nakugombea tena, binafsi naona 2020 watapambana na hali yao cos wapo wanaccm walioanza kujipanga tangu 2015 baada ya uchaguzi tu,mfano jimboni kwetu kwa mujibu wa diwani ambaye nipo naye karibu watia nia wamefikia saba wanaopenya penya kwa madiwani,so nadhani wanao hama wanajimaliza kisiasa kabisa
 
Naona leo awanajasema wanaunga mkono ila wameoteshwa
 
Mi nasubilia 2020 watakavyoduwazwa,saiz wanachekewa chekewa nakugombea tena, binafsi naona 2020 watapambana na hali yao cos wapo wanaccm walioanza kujipanga tangu 2015 baada ya uchaguzi tu,mfano jimboni kwetu kwa mujibu wa diwani ambaye nipo naye karibu watia nia wamefikia saba wanaopenya penya kwa madiwani,so nadhani wanao hama wanajimaliza kisiasa kabisa
Hawajui hilo kwa sababu ya ujinga sa sijui watakua wageni wa nani
 
NASHUKURU MUNGU KWAMBA DAMU YANGU HAIPO KABISA KWENYE SIASA,MAAAN MWISHO WA SIKU HAYA NDIO YANGENIUMIZA SANA MOYO WANGU.
UNAKWENDA PANGA FORENI HARAFU DUBWANA LINAJIANGALIA YEYE NA FAMILIA YAKE PASIPO ANGALIA NYUMA,shuwaini
 
Endelea kuwanyakua mkuu h.polepole
Watasaidia nini katika kuleta maendeleo ya viwanda mnavyonadi? Hawana hata mtaji wa kuuzia karanga zaidi sana mmewapokea ombaomba na wazee wa mizinga! Ni zamu yenu kikondeshewa mifuko yenu na kuzivuruga bajeti za nyumbani kwenu kwa mizinga mtakayokuwa mnapigwa na hao wahamiaji haramu! Laiti kama wangelikuwa ma mitaji ya chochote ningesikitika!
 
Sumaye ; Nimeenda Chadema kwa masilahi ya ccm

Sumaye ; Rais Magufuli anatekeleza Sera za Chadema
Tumia akili MBONA wamemnyanganya Mashamba yake ya dar na morogoro maslai yepi sasa
 
Back
Top Bottom