Temeke kujenga nyumba 500 na kuziuza kwa wananchi kwa bei nafuu

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Mkurugenzi wa Manispaa ya TEMEKE Nassib Mmbaga amesema kupitia mradi wa DMDP watajenga nyumba 500 na kuziuza kwa Wananchi kwa bei nafuu.
_
Mratibu wa mradi wa DMPD Wilaya ya Temeke Edward Simon amesema
wanatajaria kupewa zaidi ya BILIONI 260 ili kufanikisha mradi huo,

Chanzo: Millard Ayo
 
Amesema hizo bilion 260 ni kwa ajili ya maendeleo mbalimbali kamal miundombinu, institutional capacity strenghening n.k. ikijumuisha uboreshaji wa systems za Mapato, Magari ya taka, kujenga barabara km 91. Pia watajenga nyumba 500 za bei nafuu zikiwa na huduma za shule na zahanati. Pia mifereji ili kuondokana na mafuriko. Pia mabwawa ya maji kukusanya maji ya mvua wakati wakielekeza katika mifereji baadaye. Pia kijichi kujengwa soko na sehemu za kukusanya taka pamoja na kuweka mataa. Pia kupanda miti.. kujenga masoko ya kisasa maeneo mbalimbali na viwanja vya mipira na bustani za mapumziko.
 
Ndugu wamesema hizi pesa zimetengwa kwa miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba 500 za bei nafuu na siyo kwamba wanataka kujenga nyumba moja kwa sh milioni 500
Tatizo kuna kukurupuka ku react badala ya kusikiliza kwa makini mkuu. Ukwelli clip inajieleza vizuri sana sana kama mtu ukisikiliza huwezi kabisa kukejeli. Hongera kwa kuisikiliza mkuu.
 
260,000,000,000÷500 = bei nafuu......

Nitarudi ngoja nitafute 'pawa benki'
DMDP unahusisha ujenzi wa miundo mbinu,viwanja vya wazi,maeneo ya kucheza watoto na makazi kwa maeneo fulani jiji la Dar. Mradi mzima ni kama $300m na zitagawanywa kwa manispaa tatu Temeke,Ilala na Kinondoni. Hivyo si kwamba Tzs 260b zote wanajengea nyumba.
 
Ok....

Ila Hizo gharama zilizojificha za viwanja vya wazi na miundombinu nk zitarudije????
 
Huu mradi unafadhiliwa na World Bank. Hakuna hata 100 itakayochakachuliwa hapo. Tunahitaji miradi ya aina hii Dar nzima ili kuleta ahueni kwa wananchi juu ya upatikanaji wa makazi mazuri kwa bei nafuu.
 
Haitochakachuliwa kwenye ujenzi ila itachakachuliwa kwenye uuzaji...wabongo achana nao
 
Mpango mzuri, wangejenga nyingi kama 100,000 hivi halafu wawape watu mortgage. Pesa zitajilipa zenyewe na faida juu.

Pia na kuweka miundombinu mizuri sehemu nyingi hapa Dar.
 
Back
Top Bottom