Election 2010 TEMCO: Wakuu wa mikoa na wilaya waliisaidia CCM kampeni

n00b

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2008
Messages
981
Points
500

n00b

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2008
981 500
Thursday, 04 November 2010
Exuper Kachenje, Mwananchi

TIMU ya Waangalizi wa ndani wa uchaguzi mkuu (Temco) imetoa tathmini yake ya awali kuhusu uchaguzi huo uliofanyika Oktoba31, ikionyesha kuwa baadhi ya wakuu wa mikoa na wilaya walikisaidia chama tawala katika kampeni zake.

Temco pia imeonyesha kuwepo kwa dalili za kuvunjwa kwa sheria ya gharama za uchaguzi kutokana na baadhi ya vyama kutoa mabango mengi na vifaa vingine vya kampeni hizo vyenye gharama kubwa.

Katika taarifa yake hiyo ya awali mbele ya wanahabari jana Temco kupitia mkwenyekiti wake, Profesa Rwekaza Mukandala imetaja kuwepo kwa vitendo vilivyotishia uvunjifu wa amani na vurugu ikibainisha kuwa vyama vya CCM, Chadema na Cuf kuhusika.

"Mambo yasiyofaa yaliyobainishwa na timu ya waangalizi wa Temco si mageni, lakini yameonekana kuchukua nafasi kubwa katika uchaguzi wa mwaka huu,"alisema Profesa Mukandala na kufafanua:
Wakuu wa mikoa na wilaya walitumia rasilimali za taifa kama magari katika kampeni za urais kumsaidia mgombea anayetetea nafasi yake."

Mwenyekiti huyo wa Temco aliongeza kuwa mara kadhaa katika kampeni zake mgombea urais huyo alitumia nafasi yake kama kiongozi wa nchi kutoa au kubadili uamuzi wa serikali kama ahadi kwa wapiga kura ili kujipatia wapiga kura jambo ambalo wagombea wengine hawakuweza kulifanya.

Temko ilitembelea majimbo 135 kati ya 223 ikiacha majimbo ya uchaguzi ambayo wagombea wake walipita bila kupingwa na kutoa alama A mpaka E kwa majimbo.

Mukandala alisema kuwa mgombea kutoa ahadi si jambo baya lakini kutoa ahadi au uamuzi kutumia madaraka aliyonayo mtu ili kuvuna wapiga kura siyo jambo sahihi.

Wakati wa kampeni za kuwania urais, ubunge na udiwani kabla ya uchaguzi mkuu wa Jumapili iliyopita, vyama vya upinzani vililalamikia baadhi ya wagombea nafasi hizo kutumia nyadhifa zao kutoa ahadi kwa lengo la kuvuna wapigakura.

Akizungumzia uvunjaji sheria ya gharama za uchaguzi, mwenyekiti huyo wa Temco alisema kuwa, "Uchaguzi wa mwaka huu ni wa kwanza kufanyika chini ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi uliolenga kudhibiti matumizi makubwa ya fedha, lakini kumekuwepo na vifaa vingi vya gharama kubwa kwa vyama vikubwa hasa chama tawala CCM."

Alisema kutokana na hali hiyo hata waangalizi wa ndani wanaweza kubainisha wazi kuwa uchaguzi ulikuwa wa gharama kubwa kwa chama hicho ambapo hata wagombea wake wametumia fedha nyingi.

"Kwa sababu ya kutumia fedha nyingi kwa chama kikubwa, kampeni za uchaguzi ziligeuka ushindani kwa wasio sawa, vyama visivyo na rasilimali vilionekana kushindwa kampeni dhidi ya chama kikubwa,"alisema profesa Mukandala.

Akizungumzia upigaji kura, Mukandala alisema kuwa waangalizi wa Temco walitembelea vituo 4,332 vya kupigia kura kati 7,363 vilivyopo nchini ambapo alisema asilimia mbili ya vituo hivyo viliendesha upigaji kura kwa uhuru, lakini bila haki.

Hata hivyo alisema asilimia 68.28 ya vituo hivyo viliwezesha wapigakura kuchagua wanaowapenda kwa haki bila matatizo akiongeza kuwa Temco itatoa ripoti yake kamili kuhusu uchaguzi huo kabla ya mwisho wa mwezi huu.
 

Forum statistics

Threads 1,391,043
Members 528,343
Posts 34,071,546
Top