Telexfree

Telexfree

miminani

Member
Joined
Jul 23, 2013
Posts
51
Reaction score
7
habari ndugu zangu.. jmn kuna hii kitu inaitwa telexfree , Naskia unaweza kuchuma pesa hata ukiwa nyumbani, kuna rafiki yng kanielezea sijamwelewa mwenye idea nayo plz anieleweshe maana isije ikawa kama mambo ya desi maana unaweka pesa ili upate pesa.
 
Lol mi nimeshaconvisiwa kujiunga ila nimepuuza,bora nife na umaskin wangu kuliko kuingia huko halafu baadae ikala kwangu
 
Mimi pia nilisha shawishiwa sana kujiunga,ila bado natafakari , sijaielewa kwa undani sana, ila ninachojua ni kama biashara ya network, mtu aliekuingiza anapata commission, unapoingia unatakiwa uwe umedeposit dola 400 au dola 1500 kulingana na package unayoitaka., kazi yako ni kukopy link za matangazo na kuzipaste kwenye website, hizo link wanakupatia na hata hizo website unazotakiwa kutuma hizo link pia wanakupatia. mapato unayoyapata wewe ni dola 20 kwa kila package kwa mwezi, kama una package 3 ni dola 60 kwa mwezi, kwa maelezo zaidi hebu jaribu ku google.
 
Kishanuka mbona,kwani hamjasikia??kuna mdau mmoja alipost uzi hapa
ni pryamidal scheme kama DECI,Wizi mtupu,..
 
Mimi pia nilisha shawishiwa sana kujiunga,ila bado natafakari , sijaielewa kwa undani sana, ila ninachojua ni kama biashara ya network, mtu aliekuingiza anapata commission, unapoingia unatakiwa uwe umedeposit dola 400 au dola 1500 kulingana na package unayoitaka., kazi yako ni kukopy link za matangazo na kuzipaste kwenye website, hizo link wanakupatia na hata hizo website unazotakiwa kutuma hizo link pia wanakupatia. mapato unayoyapata wewe ni dola 20 kwa kila package kwa mwezi, kama una package 3 ni dola 60 kwa mwezi, kwa maelezo zaidi hebu jaribu ku google.

Kama DECI unapanda mbegu
 
mi ni member wa telexfree sidhani kama kuna udeci hapo nagain alot its just simple way of investment ukijicommit kny hii ishu unaweza hata ukaacha kaz, i trust it labda ije kutokea ya kutokea hapo badae na haitaniaffect coz nisharudisha pesa niliyoingilia sasa ni faida tu. ukihitaji maelezo zaidi niambie au unaweza hudhuria semina zao.
 
lol mi nimeshaconvisiwa kujiunga ila nimepuuza,bora nife na umaskin wangu kuliko kuingia huko halafu baadae ikala kwangu
umeona enhee.. Hamna cha bure town jmn..first watakupa pesa afu baadae ukinogewa tu unaenda toa mahela yako yote unapeleka huko.. Inakuwa kama desi baadae.. Lol tufanye kazi jmn hamna cha bure town, mm siamini kbs ktk hili coz huyu rafiki yng anasema kashachukua pesa tayari na amewekeza tena m.25 by april this year anasema zitarudi.. Namuombea tu zirud maana mmh!
 
Uwoga wako ndo umaskini wako ndugu zangu hiyo siyo Deci kawaida za wabongo kuomba na kusemana ila kujaribu na kujishughulisha ndo tatizo,Hiyo ni kampuni inashughulika na technology unapotoa hiyo hela unakuwa kama umenunua hisa then yeneywe haifanyi gawio kama hizo kampuni zingine wewe unarusha matangazo mwisho wa week unapata hela yako kutokana na package uliyoingia nayo.kwa maelezo zaidi nicheck hpa ntakupa details 0715564535.wabongo tusiwe wagumu kuelewa na kujaribu.

tembelea http://www.telexfree.com/
 
tell them wataishia kukalili tu, watu wameshajiwekea moyoni roho ya kutapeliwa hivo hukata tamaa mapema.
 
Sawa mkuu,huu uzi tunauweka reserve siku yakiwa kama ya DECI ,ntaurudisha...mind you THERE IS NO FREE LUNCH NA HAKUNA SHORTCUT TO REAL WEALTH...hata matajiri duniani ts their sweat ndo inawaweka mjini,
labda kwa mliojiunga zamani mkarudisha hela tayari,..but new members soon kitaeleweka
 
Uwoga wako ndo umaskini wako ndugu zangu hiyo siyo Deci kawaida za wabongo kuomba na kusemana ila kujaribu na kujishughulisha ndo tatizo,Hiyo ni kampuni inashughulika na technology unapotoa hiyo hela unakuwa kama umenunua hisa then yeneywe haifanyi gawio kama hizo kampuni zingine wewe unarusha matangazo mwisho wa week unapata hela yako kutokana na package uliyoingia nayo.kwa maelezo zaidi nicheck hpa ntakupa details 0715564535.wabongo tusiwe wagumu kuelewa na kujaribu.

tembelea TelexFREE

em tudadavulie mkuu,unanunuaje hisa af unarudishiwa hela in a week???kwa kazi ipi hasa inayoingiza hela fasta kiasi hiko??can't u vividly see kwamba ni hela za new members ndo zinawalipa kwenda juu,??how long can this kind of scheme survive?
Ki'kawaida kampuni ikiuza hisa inatumia hizo hela kufanya kazi MWAKA MZIMA NDO INATOA GAWIO,nyie weekly dividend ??mhh inaenda against all laws of Capital market...
Ofcz kwa mliowahi kujiunga mmesharudisha hela yenu,but CAN U RESIST THE TEMPTATION Ya ku'invest hela zaidi?
Mdau mmoja kasema hapo kuna mtu kapeleka 25m ,je zitarudii b4 Mikono ya Serikali haijaingilia kati???
Ishatokea b4 and i t proved failure,sio TZ tu hata nchi zingine so MJIHADHARI...wanafaidika waanzilishi,
 
Uwoga wako ndo umaskini wako ndugu zangu hiyo siyo Deci kawaida za wabongo kuomba na kusemana ila kujaribu na kujishughulisha ndo tatizo,Hiyo ni kampuni inashughulika na technology unapotoa hiyo hela unakuwa kama umenunua hisa then yeneywe haifanyi gawio kama hizo kampuni zingine wewe unarusha matangazo mwisho wa week unapata hela yako kutokana na package uliyoingia nayo.kwa maelezo zaidi nicheck hpa ntakupa details 0715564535.wabongo tusiwe wagumu kuelewa na kujaribu.

tembelea TelexFREE

Hatudanganyiki, hatushawishiki!!
 
Ndugu yangu hii mada ilisha andikiwa kama wiki mbili zilizopita hii hapa chini ni undani wake.
Hii ni Scam ya nguvu na imeanza na wakubwa hapa nchini kwahiyo ni ngumu sababu za msingi ni kwasababu ya guarantee income wanayoinadi sasa inafutia watu na ni kweli watu wanatengeneza hela lakina kwa garama ya watu wengi watakaoumia hapo ndipo inapofanana na DECI juwa ya kwamba hata DECI wale waliokuwa juu walitengeneza fedha kweli kweli na hapa ni mfano wake. Bidhaa zao ni Voip ( Ambazo sasa unaweza kupata free skype, viber) kwahiyo kulipa $50 kwa mwezi haina hilo soko, pili ni advertisment ambayo unatakiwa kupost kila siku na malipo guarantee ni 20, 100 au 1400 kutokana na hela iliyoingilia ambayo ni $ 400, $1500 au $16,000 hapa ndipo kwenye questionable practices ambapo hapo ingawa unapewa guarantee hiyo lakini ukweli pesa inatoka kwa watu wanaoingia chini yako maana advertsment hailipi kiivyo kama wanavyotaka uamini maana hata kama tangazo halijanunuliwa wewe utapewa hiyo minimum guarantee income ya hapo juu na likinunuliwa utapewa $44 sasa swali kama halijanunuliwa wewe unapewa hiyo $20 ambayo inatoka kiukweli kwa watu wanaongia chini yako ambao hiyo ndio inaleta kuwa ponzi scheme kwasababu siku utakapokosa watu ndio mwisho wa mchezo na watu wengi wataumia.
Kubwa zaidi huko Brazil ambapo ndiko ulikoanzishwa imefungiwa na watu za millioni moja wameunia wamekata rufaa zaidi ya mara 13 google au angalia kwenye mtandao huu huu utaona mambo hayo. Sasa swali ambalo promoter wa telex free Tanzania hawezi kukujibu kama makao makuu ya kampuni imefungiwa kufanya biashara je hiyo hela unayotuma inaenda nchi gani? na vile vile kwanini haijasajiliwa Tanzania na hili jibu lake haliridhishi maana wanakuambia mbona kampuni nyingi tu zilipoanza hazikusaliwa lakini hii nalo kisheria inawezekana hutaweza kuwabana kikinuka ambacho kipo karibu sana.
Na mwisho ni kwamba hata ukipata hela inabidi uache asilimia 20% ili uweze kuendelea na katika design ya scheme hapa ndipo unapofanya scheme hii iende mbali mno kwasababu ukiacha hiyo inakulipa kwa miezi mitatu kwa hela yako na kwa kuwa ni tamu wewe unaendelea kuita ndugu zako nao wanaingia chini yako, na kurudisha hela yako uliyoweka kama uingizi mtu inachukua miezi mitano so unaweza kupiga kwamba wale wataalamu wa mahesabu ya iteration wamekaa vizuri ndio maana huu schemu hata hapa imedumu kwasababu hesabu zake ni nzuri ila za kuumiza watu wengi na ndipo hapo pyramid inakuwa biashara haramu duniani kwa sababu inaumiza watu wengi na wachache wanapata sana.
Naomba kuwasiliasha
 
kaka hauoni kama huo ni ubinafsi sana wewe ujali ndugu zako wanaoingia wakiumia mradi tu wewe umesharudisha, umeshachukua au bado ziko kwenye e wallet? maana nalo hilo ni delay technique? maana ni rahisi kukurudishia kwenye card kuliko huo mchezo unaofanywa
 
Back
Top Bottom