Teknolojia wiki hii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Teknolojia wiki hii

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by MziziMkavu, Dec 27, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Dec 27, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Google imetoa taarifa yake ya uwazi ya miezi sita ya mwaka 2011. Inajumuisha maombi kutoka mamlaka mbalimbali duniani zikitaka kuondolewa kwa baadhi ya taarifa au kutaja watumiaji.


  Mahakama na vyombo vya sheria vya Marekani ndio vinaongoza, kwa kuwasilisha maombi 5,950.
  Asilimia 93 ya maombi hayo yalikubaliwa. Mengi yalikuwa kuhusu uchunguzi wa uhalifu.
  [HR][/HR]Kampuni ya usafirishaji watalii anga za mbali Virgin Galactic itasafirisha abiria wake kwa kwanza mwaka 2013.
  Taarifa hizi zimekuja wiki moja baada ya mkurugenzi wa kampuni hiyo Richard Branson kuzindua kiwanja cha kupaa na kutua cha vyombo vya anga za mbali kwenye jangwa la New Mexico.
  Msemaji wa Virgin amesema haiwezi kuwa na tarehe kamili kwa sababu usalama ni kipaumbele kwao.
  [HR][/HR]NetFlix, kampuni ya kwenye mtandao inayokodisha DVD za filamu imetangaza kufikisha shughuli zake Ulaya.
  Kuanzia mwaka ujao, kampuni hiyo itatoa huduma zake Uingereza na Ireland.
  Tovuti hiyo ndio kampuni pekee Marekani inayotoa huduma kama hiyo, lakini imepoteza wateja laki nane hivi karibuni kutokana na kuongezeka kwa bei.
  [HR][/HR]Wahandisi wa zamani wa kampuni ya Apple waliotengeneza iPod wanapeleka nguvu zao kutengeneza vifaa vya nyumbani.
  Ubunifu wa hivi karibuni ni kuunda kirekebisha joto hiki.
  Kifaa hiki kinabadili hali ya joto na baridi kutokana na watu waliopo na jinsi wanavyotaka.
  Watengenezaji wanasema unaweza kuendesha kifaa hicho kiuzwacho dola 249 kwa mbali kwa kutumia simu au hata kompyuta.
  Bonyeza hapa BBC Swahili - Medianuai - Teknolojia Wiki Hii
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Dec 27, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Dec 27, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Kipimo cha nuclear ndani ya simu yako..Kifaa cha kuhariri picha kubadilika.. Je Father Christmas ataombwa zawadi za tabiti? Na Je wewe unaweza kuwa mwana anga wa NASA? Bonyeza hapa kuiona Video BBC Swahili - Medianuai - Teknolojia Wiki Hii

  Google yalipa mabilioni kuinunua Motorola, Microsoft yafunga ukurasa wake wa kitabu cha mtandao, Blackberry mpya 4G iko tayari, na Jaribio la kuvunja rekodi ya kasi yagonga mwamba. Kuiangalia Video bonyeza hapa BBC Swahili - Habari - Teknolojia wiki hii
   
Loading...