Mambo ya sayansi na teknolojia yamesaidia mambo mengi, lakini si kumbukumbu kuhuishwa ukubwani jamani!! Mama mweye umri wa miaka 65 alijifungua mtoto. Aliporuhusiwa toka hospitalini, akarejea nyumbani. Wenzake wakaja kumwona ili kumpongeza kwa tendo hilo la baraka. Wakawa na shauku kubwa kumwona mtoto. "Ebu mwenzetu tuoneshe huyo mjukuu" wakatania kama kawaida. Bibi huyu akakazana kuandaa chai akiwatuliza wasubiri kidogo, kwani mambo ya umri hayo; alikuwa amesahau mtoto amemlaza wapi. Hivyo basi alikuwa akijibaraguza na kupika vichai ili mtoto amke toka usingizini alie ndipo ajue wapi alikuwa amemlaza!!!