Teknolojia inavyowapotosha wanafunzi

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
3,163
2,000
Kuna siku nilimuuliza mwanafunzi wa chuo kikuu kimoja kama anajua mikoa mipya iliyoanzishwa nchini alibaki anashangaa.

Nikamuuliza kama anajua makao makuu ya baadhi ya mikoa kama vile Manyara, Ruvuma, Rukwa alichonishangaza ni kwamba akawa anashangaa kama hiyo ni mikoa.

Kichwani mwake alijua Songea, Bukoba, Moshi, Sumbawanga, Musoma ndiyo majina ya mikoa.

Hii ndiyo hali halisi ya kizazi cha sasa. Wanafunzi wengi wa Kitanzania sasa hivi hawana maarifa ya kutosha kuhusu nchi yao. Zipo sababu kadhaa zinatolewa na wataalamu kuhusu hali hii.

Wapo wanaosema kuwa mfumo wa ufundishaji wa sasa umeacha kabisa kutoa fursa kwa mwanafunzi wa Kitanzania kujifunza kuhusu nchi yake kuanzia ngazi ya kijiji hadi Taifa na baadaye dunia nzima tofauti na miaka ya zamani.

Lakini wapo wanaosema kuwa mazingira ya sasa yametawaliwa zaidi na anasa na burudani nyingi. Na hii inatokana na matumizi makubwa ya sayansi na teknolojia kwa vijana. Vijana wengi wanatumia muda mwingi katika kustarehe na burudani badala ya kujifunza mambo ya msingi.

Mchora katuni mmoja aliwahi kuonyesha tofauti kati ya vijana wa kileo na wa kizamani. Wale wa kizamani ilipofika wakati wa taarifa ya habari walikuwa wakikaa chini kwa utulivu kusikiliza taarifa ili wapate maarifa, lakini wale wa kileo huipiga teke redio ukifika wakati wa kutangaza taarifa ya habari.

Mchoraji anataka kuonyesha kuwa kizazi cha sasa hakipendi kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano kwa ajili ya kupata elimu ila wangependa muda wote wapate burudani ya muziki, michezo, udaku.

Kwanza ni vema tukakubaliana kuwa tatizo si kuwapo kwa teknolojia bali ni utashi wa watumiaji wa teknolojia hiyo. Kwa mfano, ukiamua kuwa na utashi wa kuitumia teknolojia kwa malengo mazuri basi hakuna athari mbaya za matumizi yake.

Tatizo ni kwamba walio wengi katika nyakati hizi wamejikuta wakiathirika vibaya na teknolojia. Wanafunzi wengi wameshindwa kuzingatia masomo kwa sababu muda mwingi wanautumia kwenye teknolojia kwa mambo yasiyo ya msingi.

Wazazi wengi sasa hivi hujisikia fahari kuwanunulia watoto wao simu na kompyuta. Lakini wazazi hao hao wameshindwa kuwasimamia watoto wao kuhusu matumizi bora ya simu na kompyuta hizo.

Simu na mitandao imekuwa ndiyo njia rahisi zaidi katika kuanzisha uhusiano wa mapenzi. Na wanafunzi wa kike hawaogopwi tena siku hizi kama miaka za zamani. Wanaume au vijana wa kiume hawapati tena wakati mgumu wa kuwalaghai wanafunzi wa kike kwa kuwa simu zimerahisisha yote. Mwanafunzi anapofikisha umri wa kubalehe au kuvunja ungo, hisia za mapenzi na uhusiano huwa kubwa na kiwango cha kufikiria kuhusu athari za uhusiano huo huwa ni kidogo. Wanafunzi wengi hasa wa kike wanajikuta wanaingia kwenye uhusiano wa mapenzi ambao si salama na hatimaye kuathiri masomo yao.

Wanafunzi wengi wenye simu wanatumia asilimia kubwa ya muda wao kuwasiliana, maarufu kama ‘kuchat’, kwenye mitandao ya kijamii kama twitter, facebook, instagram, whatsApp, kucheza michezo ya kwenye simu maarufu kama ‘games’ na mengineyo ya upuuzi.

Wanafunzi wengi wanatumia simu zao kufuatilia habari za wasanii, muziki, picha za matukio ya kijamii, michezo ya kuigiza na hushindwa kuzitumia kujifunza masuala muhimu ya kimasomo.

Jaribu kufuatilia ratiba ya mwanafunzi wa kizazi cha sasa. Asubuhi anamka kwenda shule. Anapokuwa kwenye basi au daladala hafanyi kingine zaidi ya kutumia simu yake kucheza ‘games’ na hana muda wa kujikumbusha masomo au kusoma magazeti apate maarifa ya ziada.

Akifika shuleni simu yake inakuwa imeishiwa chaji na anaamua kuichaji humo darasani ili wakati wa kumaliza vipindi aendelee kuitumia. Anaporudi nyumbani muda wote anaitumia simu kuingia mitandaoni au kuwasiliana na marafiki zake.

Akifika nyumbani atahamia kuangalia vipindi vya filamu kwenye televisheni akihama kutoka televisheni moja hadi nyingine.

Hali hii ipo pia katika matumizi ya kompyuta. Nia ya wazazi wengi ya kuwanunulia watoto wao kompyuta ni njema lakini wanakosa usimamizi. Ilikuwa inategemewa kuwa mwanafunzi atumie kompyuta kurahisisha ufundishaji na kujifunza, lakini kwa bahati mbaya wanafunzi wenye kompyuta wanazitumia kwa mambo yasiyofaa.

Siku hizi gharama za mawasiliano ya simu zimerahisishwa na hivyo kuwafanya wanafunzi kuwa na uwezo wa kumudu gharama za kununulia vifurushi vya kampuni za simu na kuweka kwenye modemu na kuingia mitandaoni kupakua nyimbo, picha za video na michezo.

Chanzo: Mwananchi
 
loddy

New Member
Mar 13, 2017
3
45
Nchi zingine technology wanaitumia vema na kunufaika,sie tunaitumia kuchat,kutafuta wapenzi na kucheza magemu.Mkuu TUSHACHELEWA
Ni kweli tupu naamini kuwa wakati wa kuyatambua haya umefika wazazi na jamii tujikite katika kutoa elimu juu ya matumizi bora ya teknolojia hii.
 
proton pump

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
1,098
1,500

Duu maelezo meengi utadhania riwaya
 
Joowzey

JF-Expert Member
Nov 13, 2015
12,810

Kwa hyo imekuuma sana?
 
silasc

JF-Expert Member
Feb 10, 2013
3,354
2,000
Kuna haja ya kutoa elimu namna ya kutumia hii mitandao ya kijamii kwa hawa wanawafunzi wa siku hizi.
 
Joseverest

Verified Member
Sep 25, 2013
43,844
2,000
Nimekuelewa sana mtoa mada... Teknolojia zimewateka sana wanafunzi wetu kiasi kwamba mambo ya kitaaluma ni 25% na udaku/filamu/muziki/porno ni 75%.. wapo wachache sana wanaotumia teknolojia vizuri
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom