Teknolojia imekua, Taasisi za Serikali undeni mifumo rafiki itayolinda faragha za wafichua maovu

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565
Salaam Wakuu,

Kwanza, nawapongeza TAKUKURU na taasisi nyingine za kiserikali kwa jitihada zao na kazi nzuri wanazozifanya katika kupambana na rushwa na maovu nchini. Tumeshuhudia watu kadhaa wakiwekwa hatiani na wengine wakipoteza nafasi zao kwa tuhuma za rushwa.

Pamoja na jitihada hizo ukweli mchungu ni kwamba, bado rushwa ni tatizo na imekithiri katika maeneo mengi nchini. Ni wazi kwamba Matukio ya maovu na rushwa yanayoifikia serikali ni machache sana kutokana na kukosekana kwa mfumo rafiki uliotengenezwa kulinda faragha za watu wanaotoa taarifa ya vitendo vya rushwa na kuwafanya wawe waoga.

Kulindwa kwa taarifa binafsi za watoa taarifa kutaondoa uoga na kuongeza ari ya kufichua na kuripoti maovu vikiwemo vitendo vya rushwa nchini.

Hivyo ipo haja ya Taasisi zote za Serikali kuamka na kutumia vyema teknolojia kutengeneza mfumo wa salama wa kidijitali utakawawezesha watu kuripoti matukio ya maovu bila kuweka wazi taarifa zao binafsi.
 
Back
Top Bottom