Acha kukariri? Unadhani tukienda huko ndio mtatubabaisha?Ina maana nyie watu wa Tecno mmeshindwa hata kujenga hoja za ushawishi na kuishia kutiatia huruma Mara tecno Mara tecno!lakini hamsemi hizo simu zina uwezo gani mfano Ram za simu,Android ya simu,quality ya simu, ubora wa camera,security ya simu,speed ya internet etc!.Njoeni na hoja acheni kelele
Mtazamo chanya+Umezungumza mambo mengi lakini nasikitika kukwambia kwamba kiufundi/kiteknilojia hayana mantiki,simu karibu zote zinatumia hardware zinazo fanana kuanzia processor na chipsets mpaka operating systems save iphone na black berry ambazo os zake ni tofauti lakini hardware ni zile zile.
Kusema kweli maoni yako yamekaa kaa kishabeki zaidi kuliko kiuhalisia,lengo lako ni kutaka kuonyesha kwamba Watanzania wanao miliki simu za Techno ni washamba au masikini vile wakati wewe katika maoni yako unaonekana wazi wazi uelewi vizuri jinsi mobile phones zinavyo undwa/ fanya kazi,kuanzia kwenye: hardware,firmware,software:OS na apps zake; ndio maana unatujia na madai eti Techno inasumbua kwenye google!! nani kakwambia kwamba kampuni ya Techno inahusika katika masuala ya ku-code search engines za mitandaoni??? mara eti speaker za techno zinakorofisha baada ya mwaka mmoja kupita, nani kakwambia kampuni ya Techno ina-install an embeded timer ya ku-degrade quality za speaker baada ya mwaka mmoja kupita? mara, sijui iphone haiwezi kuwa hacked - kuna ukweli gani katika madai yako kuhusu suala hilo? Bottom line is: msitake kukatisha tamaa watanzania wenzenu, Watanzania wana akili timamu za kuchagua wanacho kipenda kutegemeana na mifuko/mahitaji yao.
Ukiielewa teknolojia mambo kama haya hata haya kusumbui,kuna utofauti kati ya brand name na device specification,sifa hizi mbili ndio zinamfanya mtu aliye na uelewa wa teknolojia na uchumi kufanya maamuzi ya bidhaa ipi anunue,limbukeni huwa anakimbilia kununua jina na sio kifaa.Mi ni tecno user na siyo kwamba sijawahi kumiliki samsung hapana ila ilinichosha kutokana na kutaka kunigeuza kuwa teja wa kwenye soketi ya umeme.
Toka nimeanza kutumia tecno hizo changamoto kwangu ni no japo hazidumu sana sometime na mapicha picha yake lakini Tecno is the best kwangu.
---inakaa na chaji 24+ hours kama sina mambo ya kufanya online.
__Camera yake iko vizuri .
__Kioo kikubwa
__Rahisi kuitumia haina mambo mengi.
__Space ya kutosha tu 16GB siyo haba kwa matumizi yangu binafsi.
__bei yake ni kawaida tu kwa mimi mjasiriamali au ata mkulima kuweza kuimudu.
__Upande wa data ni 4G+ na hazina ugumu kwenye upande wa Network setting.
Mnaotuponda watumia Tecno mkuje hapa mtupe Utofauti wa simu zenu.
Mi niko hapa natumiaTecno na hii post mnayoina nimeandika kwa kutumia tecno bila shaka mmeiona haina tofauti na atakaekuja kuandika kwa kutumia Samsung au I phone.
Mzk wa tekno utauona ikimaliza mwaka mmoja toka uinunue....yaan hii yangu Mara ijizime,Mara nikiwasha data istucj hadi nireboot,Mara inasearch mambo ambayo sijataka yaan taabu tupu.