Tecno Phantom ushauri tafadhali

Application zote zipo kwa phantom kama zilivyo kwa samsung. Unaweza kudowload nyingine yo yote uipendayo. Mm hutumia Phantom na naridhika nayo sana. Hiyo S 4 ya mabishoo tu haina la zaidi. Nunua phantom usijali. Isitoshe bei ni one third ya s 4 mkuu

kadownload emulator ya dolphin then tafuta game la nintendo wii ikikubali kucheza kwenye tecno nakupa vocha ya 5000.
 
Mzuri kwa vigezo vipi? Weka picha tukuone, sio unajisifia.

hata mie nimemshangaa na hayo ma housing mnayo karabati madukani kila uchwao ndo uzuri wakujitapa,, zuri debe la unga bana kila mtu analihangaikia iwe hiyari au lazima hizo zingine mbwembwe tu.
 
kadownload emulator ya dolphin then tafuta game la nintendo wii ikikubali kucheza kwenye tecno nakupa vocha ya 5000.

utaliwa hela yako mkuu tecno m7 na p5 zinachapa huo mzigo vizuri bila shida.
 
Umeanza vizuri ukaharibu mwishoni. Kama uko serious nitakupa link yao upate kuchati nao roho yako iridhike. Tatizo umeathiliwa na ukolani mambo leo kwa kuona kila anachotengeneza mzungu ni bora.

mwenzangu wengine muwaache nisawa na yule alie kuwa anang'ang'ania kupanda scandnavia kwa bei ghali sana eti kisa wanagawa soda,juicy na cace na bado akifika sehemu ya chakula anateremka kununua wakati mzee unapanda zako zuberi kwa bei ya kawaida na ukifika hotelini nawewe unateremka kununua msosi, tabu ya watanzanaia tulio wengi tunashabikia majina ya bidhaa eti kisa samsung mtu yupo radhi alipe hadi milion wakati katika utendaji ngoma droo na tecno tena misamsung ming huwa inapata moto mapema kuliko tecno sasa sijui wana nunua kwa vile ya majina hata sielewi mh! Eti samsung,iphone,blacberry na makorokocho mengine sijui manini huko!! Aaagh !! Sijui wenyewe bana mie situmii samsung wala tecno bt techo naikubali ni reliable kwa nchi zetu za kiafrica.
 

Kuleta ulayman kwenye mambo ya kitaalamu katu hakukubaliki
Hata mwenye bajaji atafika mbagala kama mwenye vogu

Achilia kampuni mbili za mabasi hapa bongo kuwa na bei tofauti, mahali popote pale duniani ndege ni moja lakini madaraja tofauti na kila daraja lina bei yake tofauti kabisa,mnapanda ndege moja na mnatua uwanja mmoja at the same time.......je hawa nao ni malimbukeni?

Kama kweli hujui kwanini akina Samsung na wenzake wanauza simu zao bei ghali kuliko Tecno na upeo wako ukaishia ni kwa sababu ya majina yao basi upeo wako kuhusu hili ni mdogo sana mkuu
 
Nilishasema mjadala huu umefungwa, sasa nisijue kwa nini mnauendeleza. Mwenye macho haambiwi tazama! Sasa ni kati ya mtu na muono wake kuhusu hizi cm.
X- mass njema wote wanajf. Mi sasa niko naelekea kijijini kwangu Nyarugando nadunda na A+ yangu. Habari yote hapa kiganjani!!
 
Huwezi kujua kibaya kama hujatumia kizuri. Sasa hapa kuna watu wanatetea simu walizo nazo wakati hawajatumia hizo nyingine. Uzoefu wangu hizi kampuni reputable ni tofauti sana bei haipandi bure aiseee!! Hata ukibonyeza buttons tu responce itakuonyesha kuwa simu unayotumia baado sana!!!
 
Xmss njema na phantom langu nasonga nalo......niliziona Sony experia na HTC mpaka za laki 3.5 lakini nikapiga chini nikabeba ili phantom kweli sijutii na wala sijawahi jutia kwani kabla ya chili phantom nilikuwa kwenye ka-samsung gallax s2 sikuenjoy kama kwenye hili phantom A+ kwa matumizi Yang mimi na sio kudownload game na utoto mwongine wanao sifia vijana
 

ninacho kiongea nakifahamu kuliko unavo dhan wewe,, hapa inshu sio majina ila ni system mechanism kama wewe ni mtu wa electronics utakuwa umenielewa ila kama na wewe ni mbabaishaji ila unashabikia tu kwa vile hutumii tecno bora ukae kimya na ufunge bakuli lako then vinginevyo kwa hoja yako basi kusinge kuwa na samsung yenye madhaifu, kuuzwa bei ghali sio kigezo cha kukufanya uone hicho kitu ni durable usiwe mmatengo wewe.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…