TECMN: Wanafunzi waliopata Mimba waruhusiwe Kusoma, Salma kikwete na wabunge wenzie wapingwa vikali

Evans-Arsenal

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
868
1,385
Akiongea leo mkuu wa TECMN amesema wanasikitishwa na wabunge wanaopinga hatua ya wanafunzi waliojifungua kuendelea na shule, TECMN inasema ni haki ya kila mwanafunzi kusoma, pia wabunge wengi wanakandamiza haki ya watoto wa kike kusoma kwa kuwakataza kuendelea kupata haki yao ya kikatiba.

Hii ina maana kwamba mimba kwa wanafunzi wa kike wakiwa mashuleni zitakubaliwa au niaje??
 
Hawajanyimwa kusoma lakini siyo wamama wazazi kwenda kukaa darasani na mabinti zetu. Wajisomee wafanya mtihani kama "Private candidate"
 
Kama wanawaonea huruma wawajengee shule zao pembeni wakawasomeshe wenyewe na ziitwe shule za wazazi. Pumbafu zao
 
Tatizo tunaongelea maoni binafsi badala ya sheria na miongozo. Ni kifungu gani cha sheria za shule kinatoa haki ya kupata mimba? Kama ni huruma, mbona haiongelewi haki ya mtoto kupata maziwa ya mama na mnaiona ya binti kurudi shule? Huruma ni wajibu wa binadamu, sheria nazo ni kuwarudi wanaotoka kwenye mstari.
 
Siku Binti yako wa miaka kumi na moja akiwa moja mzigo ndipo utajua kama haki ya kunyonya anayo mjukuu wako au Binti yako.

Acha upumbavu.
 
Kama wanawaonea huruma wawajengee shule zao pembeni wakawasomeshe wenyewe na ziitwe shule za wazazi. Pumbafu zao

Siku Binti yako wa miaka kumi na moja alipata mimba hope utasema pumbavu zako.

weka maneno akina kuna kesho ndugu.
 
Siku mtoto wako wa miaka kumi akiwa mjamzito ndiyo utajua kama Maharage ni mboga pia.

Weka akiba ya maneno kuna kesho pia
Kwani wakijisajili kama private candidates hawasomi? Haki ya kiumbe kilichozaliwa itapatikanaje huku mama akitakiwa kuwajibika kwa kila kitu kama wanafunzi wengine? Wajengeeni shule zao hao wanafjnzi wazazi kama zilivyo jera za watoto ambao hawajafikisha miaka 18 muwapeleke huko
 
Mtoto wa miaka kumi na moja ajengewe jela ya watoto,hivi una hata mtoto wa kudanganyia??Kwa mawazo hayo Ni najua huna mtoto ndiyo sababu hujui uchungu wa mtoto.

Subiri mtoto wako wa miaka kumi na moja akiwa mjamzito apeleke jela ya watoto.
 
Jela imetumika kama mfano tu, kwani hakuna jela za watoto? Shule za wanafunzi wenye ujauzito au wenye watoto wadogo mpendekeze zitenganishwe na wanafunzi wengine. Kwasababu ni uhakika utaratibu wake na miobgozo yake itatofautina na shule za kawaida. Piganieni kuanzisha shule zao na mimi nitawaunga mkono
 
Hivi mimba ni jinai hadi ukose haki ya kusoma??

Kwani Utoro ni jinai mpaka akose haki ya kusoma?

Ukivunja Masharti na Sheria za Shule ikiwa ni Pamoja na kupata Mimba utapoteza haki yako ya kusoma Kama School candidate
 
Waondoe lile katazo la "Uasherati" mashuleni kabisa ili watoto wajue tu kukaza na kukazwa sio kesi tena.
 
Kama wanawaonea huruma wawajengee shule zao pembeni wakawasomeshe wenyewe na ziitwe shule za wazazi. Pumbafu zao
Kabisakabisaa.... Alafu wajinga. Kwani si kuna private schools... Na hao wa Qt.

Kwanini wanang'ang'ania huku serikalini.??
 
Back
Top Bottom