TEC yaihadharisha Serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TEC yaihadharisha Serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mzambia, Apr 3, 2011.

 1. m

  mzambia JF-Expert Member

  #1
  Apr 3, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  BARAZA la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limeitahadharisha Serikali kuwa tofauti kubwa ya kipato miongoni mwa wananchi inaweza kusababisha kutoweka kwa amani nchini.

  Katibu Mkuu wa TEC, Padri Antony Makunde alitoa tahadhari hiyo katika hafla ya viongozi wa dini ya kuombea amani jijini Dar es Salaam ambapo alisema amani iliyopo sasa hapa nchini inaweza kutoweka kama serikali haitafanya juhudi za kuondoa tofauti hiyo.

  “ Tuilinde amani iliyopo kwa kumaliza kero za wananchi, umaskini unaweza kusababisha tunu ya amani tuliyonayo ikatoweka,” alisema Makunde.

  Katika hafla hiyo iliandaliwa na Jumuiya ya Waislam Waahamadiyya, Padri Makunde alisema ikiwa Serikali haitaheshimu misingi ya kidemokrasia inaweza kusambaratisha amani ambapo alitaja pia kashfa dhidi ya dini za wengine kuwa ni jambo linaloweza kusabababisha kutoweka kwa amani.

  Hata hivyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Stephen Wasira alisema matatizo ya kiuchumi yaliyopo nchini yasiwe sababu ya kutoweka kwa amani.

  “ Tuna matatizo ya kiuchumi, lakini hiyo isiwe sababu ya kutoweka kwa amani, amani ikitoweka uchumi hauwezi kuimarika,” alisema Wasira.

  Kiongozi wa Jumuiya ya Waislam Waahamadiyya nchini, Tahir Chaudhry alisema lengo la kuandaa hafla hiyo ni kuomba amani kwa pamoja kwa sababu kila dini inahubiri amani.

  “ Hakuna dini inayohubiri uvunjifu wa amani, hiyo haitakuwa dini, ndiyo maana tumeona tuwaalike wenzetu wakristo ili tuombee amani kwa pamoja,” alisema.
   
 2. g

  gepema Member

  #2
  Apr 3, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  huu ni ukweli mtupu coz wasio nacho hatakubali kuendelea kuumia wakati watu wachache wakiendelea kuishi kama peponi
   
 3. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #3
  Apr 3, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Washukuriwe viongozi wetu wote wanaotetea amani kwa maslahi ya watanzania. Kwa pamoja dini zote tuombe amani kwa kukataa udhalimu wa wahujumu uchumi.
   
 4. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #4
  Apr 3, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,743
  Likes Received: 6,018
  Trophy Points: 280
  Bravo Sheikh Tahir Chaudhry. Natamani viongozi wetu wote wa dini wangekuwa kama wewe; hakika nchi ingefika mbali. Haya ndio wananchi tunayotamani kuyasikia kutoka kwenu viongozi wetu na sio wale wengine wanaotumiwa na wanasiasa kwa ajili ya kuwatisha wananchi na kueneza hisia za udini na ubaguzi miongoni mwa jamii. Hakika hawa wana kesi ya kujibu siku ile ya hukumu! Hakika huyu jamaa (Sheikh) ni kichwa; nadhani ni mdosi; heshima Sheikh wangu.

  Lakini pia kwa mleta mada; kwani ilikuwa lazima kuweka neno TEC (Tanzania Espiscopal Conference - Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania) kwenye kichwa cha thread wakati kimsingi waliohusika sio Wakatoliki peke yao hata walioandaa sio TEC?
   
 5. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #5
  Apr 3, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Maaskofu 'wagombea' waraka wa Mtikila Send to a friend Thursday, 27 May 2010 10:21 0diggsdigg

  Mussa Mkama
  MAASKOFU waliohudhuria mkutano wa siku moja wa Jukwaa la Wakristo, juzi walifanya kazi ya ziada kupata nakala ya waraka ulioandaliwa na mwenyekiti wa Chama cha Kidemokrasia (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, ambaye alitumia mkutano huoo kuusambaza.

  Mkutano huo ulikuwa wa kuzindua chombo hicho kikubwa cha mshikamano baina ya Wakristo, lakini Mchungaji Mtikila, ambaye anaongoza kanisa la Full Salvation, aliutumia kugawa takriban nakala 60.
  Alikuwa akigawa waraka ambao ulisababisha polisi kuvamia nyumba yake iliyo Mikocheni na kufanya upekuzi kabla ya kuondoka na mwanasiasa huyo ambaye pia ni kiongozi wa kiroho na kwenda kumuhoji kituo cha polisi kwa saa kadhaa zaidi ya mwezi mmoja uliopita.

  Waraka huo wenye kurasa 24 ambao Mwananchi ina nakala yake, unazungumzia harakati za kuwaamsha waumini wa dini ya Kikristo kuamka kutetea dini yao dhidi ya utawala wa sasa ambao mchungaji huyo anautuhumu kuwa unawabagua.

  Waraka huo pia unawataja watu mbalimbali, kuanzia Rais Kikwete, viongozi wengine wa kisiasa na watu maarufu ukiwahusisha na tuhuma mbalimbali kubwa.
  Maaskofu kadhaa walionekana kumfuata Mtikila ili kupata nakala ya waraka huo ambao mchungaji huyo alikuwa amebeba nakala zake kwenye mkoba wa mkononi.

  “Nilikuja na nakala chahe sana... 60 tu, zikaisha na wengine wakawa wanautaka tena," alisema Mtikila mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kuzindua chombo hicho ambacho kazi yake kuu itakuwa ni kutetea haki za Wakristo.

  "Nimegawa hapa kwa sababu viongozi wenyewe waliutaka ndiyo nikaona niwape; nisiwe mchoyo,” alisema Mtikila.

  Mtikila alisema kuwa kuzinduliwa kwa jukwaa hilo ni kuzaliwa kwa tatizo kubwa kwa Rais Jakaya Kikwete na kumtaka ajihadhari, akidai kuwa ajira yake sasa ipo kwenye "danger zone (sehemu ya hatari).”
  Mtikila, ambaye ana ujasiri wa kutoa kauli zisizo na simile, alisema jukwaa hilo ni gharika kubwa kwa Rais Kikwete kwa sababu alizodai kuwa kiongozi huyo wa nchi ni adui mkubwa wa Ukristo.

  “Wakristo nchini tupo milioni 27 hivyo ajira ya JK hivi sasa ipo shakani," alisema.
  Viongozi wa makanisa ambayo yalishirika katika kuunda jukwaa hilo ni pamoja na Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (Tec), Jumuiya ya Makanisa ya Kikristo (CCT) na Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste (PCT).
   
Loading...