Ni vigumu kwa serikali kufungia Baraza la TEC (Baraza la Maaskofu wa Kikatoliki Tanzania) kwa sababu lipo chini ya Kanisa Katoliki na kila mtu anajua ushawishi mkubwa wa kanisa hili duniani chini ya kiongozi wake mkuu Papa, ambaye hata mataifa makubwa kama Marekani hutambua nguvu yake ya kidiplomasia na kiimani. Zaidi ya hilo, Kanisa lina miundombinu mikubwa kama shule, hospitali, vyuo na vituo vya huduma ambavyo mara nyingi ni bora kuliko hata vya serikali, na vinategemewa na wananchi wengi. Kwa sababu hizi za kimataifa, kijamii na kisheria, kulizuia au kulifungia Kanisa Katoliki kutaleta athari kubwa na ndiyo maana ni jambo gumu sana kutekelezeka hilo unalotamani wahusika wafanye.