Team Wasira ni Noma

Team Wasira ni Noma

CCM naipenda lakini huyu jamaa hapana kwa kweli mtanisamehe!!
 
Yupo live apa Itv anasema akiwa Rais...atahskikisha jembe la mkono linawekwa stoo.maana yake anafanya Agrarian revolution.watu wanampigia makofi sana apa
 
Ila kwa huu ukumbi ilivo V.I.P sidhan km mtu wa chin atathubutu kuja kuingia humu..angetafuta ukumbi wa kawaida
 
hapo kwenye red ndipo alipopoteza sifa ya kuteuliwa na CCM
Stephen Masato Wasira-alizaliwa mwaka 1945 Wilayani Bunda,Mkoa wa Mara. Akiwa mdogo Stephen M.Wasira alisoma Elimu yake ya Msingi Shule ya Msingi Balili na Kisangwa Middle School, Wilaya ya Bunda, baada ya hapo aliendele a na masomo yake ya Sekondari katika Shule ya-British Tutorial College.

Aliendelea na Masomo ya ngazi ya juu nchini Marekani huko alipata kusoma shahada Tatu za Uchumi na Utawala. Alisoma Shahada ya Kwanza katika Uchumi na Mahusiano ya Kimataifa,Shahada ya Uzamili katika Uchumi na Shada ya Uzamili katika Utawala, zote kutoka Chuo Kikuu cha Amerika (American University) Jijini Washngton D.C.

Katika Maendeleo yake kama Mtumishi wa Umma,Wasira alipata kushika nyadhifa mbalimbali katika serikali,Kwanza; aligombea na Kushinda kuwa Mbunge wa Jimbo la Mwibara Mwaka 1970 hadi 1975. Katika kipindi hiki cha Mwanzo kama Mbunge aliteuliwa na Mwalimu Julius K.Nyerere kuwa-Naibu Waziri wa Kilimo.

Mwaka 1975,Mwalimu Nyerere alimteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara,alikuwa katika nafasi hiyo tangu mwaka 1975 hadi 1982 alipoteuliwa kuwa Waziri na Afisa Mwandamizi katika-Ubalozi wa Tanzania Washington,D.C.

Mwaka 1985,baada ya kutoka Marekani,aligombea na kushinda kuwa Mbunge wa Jimbo la Bunda kwa miaka mitano,Katika kipindi hiki aliteuliwa na Rais Ali H. Mwinyi kuwa Naibu Waziri wa Serikali za Mitaa, na baadae akawa-Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugomwaka 1989 hadi 1990.

Mwaka 1990, Wasira aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani nafasi aliyoitumikia mpaka mwaka 1991, na baadae Mwaka 1995 aligombea na Kushinda Jimbo la Bunda akiwa kama Mbunge wa Upinzani, hakutumikia nafasi hiyo kwa kipindi chote mpaka 1996 alipoondolewa katika nafasi hiyo.

Takribani Miaka kumi alijielekeza katika Biashara yaKampuni yake iitwayo Siza Cold Storage Ldt iliyokuwa ikisafirisha nje ya nchi mazo yatokanayo na bahari.Mwaka 2005 alirudi tena Bungeni kupitia Jimbo la Bunda nafasi aliyopita bila kupingwa,ameendelea kuwakilisha Jimbo hilo kwa kipindi chote hadi Uchaguzi Mkuu mwaka 2010 alipochaguliwa tena kuongoza jimbo hilo.

Chini ya Uongozi wa Rais Jakaya M.Kikwete, Mhe.Wasira ametumikia Wizara tatu,Kwanza; aliteuliwa kuwa Waziri wa Maji January hadi October 2006. Baada ya hapo aliteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika mpaka 2010, Pia aliweza kutumikia kwa muda Ofisi ya Waziri Mkuu kama-Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mikoa(TAMISEMI)February hadi May 2008. Baada ya Uchaguzi Mkuu October 2010,Mhe.Wasira aliteuliwa kuwa-Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu,nafasi anayoendelea kuitumikia mpaka sasa.

Ndani ya Chama Tawala,Chama Cha Mapinduzi, amekuwa Mjumbe wa Halmashauri kuu miongoni mwa wajumbe 370(NEC) chombo cha juu kabisa cha maamuzi na sera za Chama,Amekuwa katika nafasi hii tangu 2007. Mwaka 2011 alichaguliwa kuwaMjumbe wa Kamati Kuu miongoni mwa wajumbe 28 , baadae alichaguliwa tena katika nafasi hiyo February 2013. Mnamo November 2012 alichaguliwa kwa kishindo kuwa-Mjumbe wa Halmashauri Kuu-kwa kipindi kingine cha Miaka mitano
 
Mbona hujaonesha hiyo team Wassira na unoma wake kwenye thread yako.
Ndorrrroboooooo hujatulia kabisa inabidi tukupepeeee!
 

Attachments

  • 1433097540923.jpg
    1433097540923.jpg
    27.6 KB · Views: 269
aliendele a na masomo yake ya Sekondari katika Shule ya-British Tutorial College.
Hii shule ya sekondari iko wapi? Muda kidogo aliwahi kuonyesha shule ya Sekondari ya Bwiru; nadhani mwandishi umekosea. Ninajua kuwa alisoma Nyambitilwa ila sijui darasa gani.
 
Alipokuwa mkuu wa mkoa wa Mara alikula pesa walizokatwa wakulima kwenye mauzo ya Pampa kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa. Mpaka sasa lile jengo limebaki kuwa gofu kule mlimani.
 
Mtoa mada unadai eti kwa miaka 10 Wassira alijikita ktk biasha za kampuni yake baada kutolewa ktk ubunge 1996. sasa si useme tu ukwel kuwa baada ya Wassira kuvuliwa ubunge na mahakama kwa kushinda kwa kutumia rushwa, alipigwa ban asigombee nafasi yoyote kisiasa hadi after 19 yrs. sasa wewe badala ya kuwa muwazi unasingizia alikuwa akifanya biashara!! weka yote wazi!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom