Team diamond na team Kiba, ni ujinga tu

juvenile davis

JF-Expert Member
Apr 13, 2015
4,752
4,463
Nadhani ni kutojua muziki na ushamba ndio unatusumbua wabongo wengi.

Kwanza niwafunze kitu wote hapa leo, iko hivi: Shabiki hutakiwi kuwa unamshabikia msanii hadi unajiita team fulani, muziki sio mpira!

Msanii anaweza kuacha kuimba je utaendelea kushabikia?? Kwenye muziki huwa tunapenda wimbo na sio msanii, shabikia wimbo na sio msanii, msanii ataacha kuimba lakini wimbo hautapotea milele, so team Kiba na team Diamond kama mpo humu acheni ushamba!
 
Huwa najiuliza, hawa watu wanapata faida gani, maana wanabishana na kutukanana mpaka mishipa inawasimama.
 
Huwa najiuliza, hawa watu wanapata faida gani, maana wanabishana na kutukanana mpaka mishipa inawasimama.

Halafu wenyewe wanaona sifa hao....ukijaribu kuwakanya wanakwambia uwaache.

Teh teh teh.....duniani kuna haki nyingi.

Hata haki ya mtu kutaka kuwa mpumbavu nayo ni haki.

Tena haki ya msingi kabisa....ya kuweza kujichagulia.
 
Haaha haki ni nyingi sana
 
Huwa nachukia sana hata kwenye mashindano ya kimataifa utaskia tusimpigie kura huyo huku wote ni watanzania na heshima ni yetu sote ,au akikosea mmoja ukikosoa utaskia mawe yake hapo,...huo ni ujinga kiukweli
 
Kama unadhani team Diamond/Kiba zinakukera, jaribu Bey-hives au the navy. Ukitaka kutokereka nao, just keep off their biz.
 
Sijawahi kuzielewa hizi clubs usajili wao unakuwaje na faida ni zipi?zaidi ya kutukanana na kupigana ikibidi hawa vijana wetu wote ni watanzania utani upo ila sio wajenge chuki kati ya club na club na khasa linapokuja suala la kimataifa.
 
Back
Top Bottom