Pendo Julliet
JF-Expert Member
- Sep 15, 2017
- 243
- 324
Takwimu za TCU zinaonesha hadi sasa wengi waliofanya application kwa awamu ya kwanza wamekosa vyuo.
Kati ya waombaji 180,640 majina kutoka vyuoni yalitumwa TCU na TCU inaeleza kutokana na kasoro nyingi yalihakikiwa na kupunguzwa hadi 77,756.
Waliochaguliwa na vyuo ni 44,627 tu hii sawa na 57.4% ya waombaji wote.
Waombaji 33,129 waliosalia sawa na 42.6% hawakuchakuguliwa na vyuo kutokana na ushindani au kukosa sifa katika programu walizoomba.
Hadi sasa kati waombaji 44,627 ambao wamechaguliwa na vyuo waombaji 38,831 tu ndiyo wanaoeza kujiunga na vyuo direct ukiacha zile kasoro za multiple selection nk.
Sasa Tume inaeleza imefungua tena maombi kwa awamu ya pili kuanzia tarehe 4 hadi 10 Oktoba 2017 ili kuruhusu walochaguliwa chuo zaidi ya kimoja kutaarifu chuo husika, waombaji walokosa nafasi kwenye awamu ya kwanza kwa ushindani au kukosa sifa katika programu walizoomba na wengine wote waloshindwa kuomba katika awamu ya kwanza waombe awamu hii ya pili yani kuanzia tarehe 4 hadi 10 Oktoba 2017.
Kutokana na ugumu wa zoezi hili la uombaji wanaokumbana nao waombaji hawa kwa sababu ambazo ni za mifumo ile wanayotumia kuomba kuwa unstable[hili siyo kosa la waombaji] muda huu wa siku 6 ni mfupi na hautoshi.
Ni heri sana TCU walione hili na waongeze muda zaidi ya tarehe 10 Oktoba ili wengi wakamilishe zoezi la uombaji ili kuepuka wengi kukosa vyuo na kukatisha ndoto zao za kupata elimu ya chuo ambayo ni haki ya kila Mtanzania mwenye sifa na vigezo vya kujiunga na kusoma chuo.
Nimeona vijana wengi wanahangaika na wengine wanaanza kukata tamaa sababu tu wanaona hawatendewi haki hali vigezo vya kujiunga na chuo wanavyo.
TCU kazi kwenu.