Mdhamini wako anaweza akawa amepanga kukudhamini nauli ya kwendea sehemu fulani, lakini kwa makadirio ya uwezo wake na idadi ya watu anaowafadhili akaamua atakupatia ela ya kukutosha kutumia usafiri wa daladala kila siku.
Sasa wewe ukiamua kutumia bodaboda au taxi kusafiri yeye hana tatizo atakupa hela ya kutosha kupanda daladala kama ilivyo makubaliano.
Sasa ukishindwa kulipa nauli ya bodaboda uliyoamua kupanda na ukishushwa njiani karibu na kufika yeye anahusikaje?
Aje amwambie bodaboda amalizie safari bure?
Au akulipie nauli ya bodaboda wakati kuna watu walitamani hiyo ya daladala na hawakupata?
Mfumo haujakosea na hakuna wa kumlaumu pambana utafute solution nyingine. Na wengine tujifunze kufanya maamuzi yatakayo affect muda mrefu.
Punguza jazba
Mi ninavyofahamu ada ya kozi yako unaijua kabla hujaaply. Tatizo labda kama mtu hatataka kujua hilo au ada imebadilika badae, na bodi wanatoa hela ya ada kulingana na gharama iliyoko katika vyuo vya serikali.
Kwa iyo ukichagua vyuo vyenye ada kubwa na unajua possibility ya kupata mkopo mwisho maybe ni 1.5ml utahitajika kulipa iliyobaki mwenyewe.
Na bodi wanafahamu kabisa kuna vyuo vyenye ada kubwa zaidi ya mkopo wanaokupa na sambamba na hilo wanafahamu kuwa kozi hiyo hiyo katika chuo cha serikali itakuwa inaendana na hela waliyokupa.
Na hawajui kama huna ela ya kuongezea kwa sababu ulichagua mwenyewe.
Sipo apa kuonesha kuwa ulikosea ila natamani uelewe kuwa usijaribu kutafuta wa kumlaumu, bodi haiwezi kuongeza hela kamwe na chuo hawewezi kukuruhusu kuendelea kama ujamalizia kulipa.
Kama ni mapema acha chuo uanze kwingine, kama ushafika mbali tafuta namna ya kulipa iyo ada. Au kama vipi acha chuo kabisa kwa sababu sio kwamba ukimalliza ni guarantee ya mafanikio
Kama hakuna majibu ya TCU tutakwenda kupiga hodi ofisi No 1, aende achukue hela yake kule isipotee bure au bodi ya mikopo kuja kunidai hela hiyo bure wakati sijasoma na kumaliza, sawa na mtu aliyenyanyuliwa juu ya kifua cha mpenzi wake katikati ya "shughuli" muda mfupi karibu na kupiga mshindo.Nadhani namba 4 nikuwa haiwezekani, sababu hiyo ni ada anayolipiwa alieko private , ada ya serkalini haifiki huko, na ukichagua vyuo hivyo maana yake unaweza kumudu.
nadhani utaratibu wa chuo kuwasimamisha hauko vizuri, zaidi waweke utaratbu wa malipo ya awamu, hali si nzuri kwa kila mmoja na vyuo vya serkali haviwezi kuwabeba wote.
Mfano wako ni feki, haufanani na hilo. Hiyo hela ya nauli hakunipa mimi alimlipa mwenye bodaboda ili anisafirishe ninakotaka kwenda, mtoa pesa kamlipa mwenye usafiri hela pungufu kuliko kiasi anachotaka akitegemea kuwa mimi nitatafuta hela ya kujalizia patakapopungua, matokeo yake hela yake imeliwa na yangu pia imeliwa na safari imekomea njiani, tena katikati ya pori nene. Bahati nzuri mtoa fedha anaufahamu vema mji nilikotaka kwenda na gharama yake, pia anafahamu kuwa mimi sina hela ya kuongezea kwenye ile aliyonipa ndiyo maana nilimlilia msaada wa hali na mali. Je, yeye atanidai hela yake hata kama mwenye bodaboda alinishushia njiani, tena porini? au ni yeye amdai mwenye bodaboda amrudishe hela yake kwakuwa hajanifikisha niendako? au ni yeye amuongeze mwenye usafiri ili anifikishe safari yangu ili aje anidai mimi? Kosa la mwenye bodaboda hakumwambia mapema mtoa nauli kuwa ile hela punguvu ingemfikisha mteja wake hadi wapi, alipokea tu na kuitia mfukoni. Angeniambia mapema kama hii hela niliyopewa ingetosha kunisafirisha hadi pale porini aliponishusha kamwe nisingeukubali msaada ule, maana ingekuwa sana na mtu aliyeshonewa shati pekee bila kaptura ya kuvalia lile shati.
Seikali nadhani iache kabisa kutoa hela kusomesha wanafunzi kwenye vyuo binafsi.
Mnakosea kusema hivyo, anayeshindwa kulipa ada sio mwanafunzi bali mzazi wake ambae alidhani ataweza ghafla anajikuta gunia lake la mahindi linakosa bei sokoni.Sasa hapa unachopinga ni nini? Jamaa alikuelekeza vizuri sana na alitumia mfano unao lingana na mazingira yako. Nionavyo vijana wengi huwa hamna uelewa wa kutosha wakati kuchagua vyuo. Serikali ina kiwango cha ada katika kila taaluma, ukichagua chuo unapaswa uangalie na fee structure ya chuo na ukomo wa Serikali. Ukichagua maana yake kinachozidi utalipa wewe.
Katika hili TCU na HESLB usiwabebeshe mzigo hilo ni lako na familia yako.
Huo ni upuuzi, hayo mwambie mzazi wangu sio mm. Lakini kila mtu ana haki ya kupata elimu, vyuo hivi vingetangaza kabisa kuwa mwanafunzi mwenye wazazi wanaolipa Kwa kudunduliza wasikanyage vyuo vyao. Serikali ilinilipia kwao 3.1 m kwa mwaka, je hiyo wamemwambia mzazi na serikali kama inatosha kupata huduma zipi na zipi hapo chuoni? Sio kwamba mzazi asingelipa kiasi kinachotakiwa, angelipa Tu lakini sio Kwa mkupuo kama wanavyotaka wao. Hivi Yuko mtu mwenye akili sahihi atakayekiacha cheti chake chuoni milele bila kukikomboa?Hivi kwa nini usingeacha wewe kwenda ili wenzako wenye uwezo wa kuongeza wapate nafasi kuliko unavyo shauri?