kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,307
- 12,602
Tumedahiriwa vyuo vikuu fulani nchini vyenye ada kubwa kuliko 3,1 mil tunayolipiwa na Loans Board kama mkopo, lakini tumesimamishwa masomo Kwa muda usiojulikana eti Kwa kosa la kupungukiwa kidogo na kile kiasi cha nyongeza tulichopaswa kuongeza ili kukamilisha kiasi cha Ada yao yote ya vyuo hivi. Tumesoma lakini tukazuliwa kufanya mitihani yote hadi tutakapolipa Ada yote.hivyo hatuwezi kuendelea na miaka mingine tena, Sisi ni watoto wa wazazi wanaomudu kulipa Ada kidogo kidogo Kwa kadiri wanavyopata lakini chuo wanataka zote hapohapo kabla hujaingia darasani kusoma.
Tunaomba ufafanuzi Kwa maswali yetu yafuatayo.
1. Ni haki kufukuzwa shule wakati hela yetu ya loans board wamechukuwa?
2. TCU na Loans Board mmebariki kitu kama hiki kufanywa vyuoni?
3. Tutalipaje deni la loans board ikiwa tumefukuzwa tusimalize chuo kwasababu ya Ada ya nyongeza ya vyuo?
4. Je, tukileta ushahidi wa kusimamishwa masomo na vyuo hivyo loans board mko tayari kutukopesha zaidi ili tulipe deni la vyuo?
5. Mnatusaidiaje tuweza kumaliza masomo kwenye hivi vyuo ghali Sana?
6. Kutusimamisha masomo Kwa mtindo huu ni sawa Kwa mujibu wa kanuni za TCU na Loans Board?
7. Hatima yetu ya kuendelea kupata mikopo tutakaporejea vyuoni ikoje? sasa hivi nasikia hela zetu zitarudishwa loans board kwakuwa sisi hatupo darasani