herikipaji
JF-Expert Member
- Aug 23, 2016
- 1,198
- 1,345
Sintofahamu nyingi zinajitokeza na bado zinaendelea kutokea kutokana na hii taasisi inayosimamia elimu ya juu kukosa umakini na kuwajibika ipasavyo kwa makusudi au kwa sababu nyingine wanazozijua wao wenyewe hali inayosababisha usumbufu na matatizo lukuki kwa wanafunzi.
Application ya vyuo vikuu ilifunguliwa tarehe 15 August kwa Diploma holders lakini ajabu ni hawa TCU kufanya deadline tarehe 31 August huu ni muda mfupi sana, siku 15 tuu hivi TCU mna ajenda gani ya siri na mnayafanya haya yote kwa faida ya nani? Kama mnataka watu wasisome basi kuweni wazi tu ifahamike moja.
Baadhi ya vyuo hata matokeo ya final overall hadi hivi sasa bado hayajatoka na wanafunzi wa vyuo hivyo wameshalipia ada ya udahili ina maana hawa wanafunzi wanakosa nafasi na haki yao ya msingi ya kuendelea kusoma? Mlichelewa sana kufungua application na sasa mnawahi kufunga mna makusudi gani hivi?
Ilianza GPA na cut off point kwa A-level watu wamekwishafanya mitihani mnakuja na viwango vipya ni sawa na kwenda kumtoa mfungwa aliyeko gerezani kufuta hukumu yake na kumhukumu upya kwa sheria mpya iliyotungwa, maajabu haya!!
Haya sasa wale wachache waliofikisha hata hizo GPA mnakuja tena kuwachimbia mashimo ya mitego ili tu waanguke kwa kuwapangia siku 14 za application, hivyo vyuo vikuu mnataka nani akasome mwaka huu?
Madudu haya yote mnayoyafanya ni kwa faida ya nani??
Kazi mnayoonekana kufanikiwa kuifanya vema ni kuwachimbia mashimo watu wasisome vyuo vikuu mwaka huu, mmegeuka WACHIMBA MASHIMO.
Hamtendi haki.