TCU Kwa nini mna kigugumizi?

Shebbydo

JF-Expert Member
Feb 12, 2015
1,174
1,937
Habari wana jf,

Mimi ni mdau mkubwa sana katika kufuatilia mambo ya elimu hapa nchini bila kujali ni mambo yanayohusu hatua ya chini niliokwishapita ama vinginevyo.

Ilikuwa kawaida kwa miaka ya nyuma kwa TCU kutoa kitabu kinachomuongoza mtu anayetaka kuomba kusoma fani mbalimbali vyuo vikuu mwezi wa nne mwishoni kuelekea wa tano. Hii ilikuwa inatoa nafasi ya kutosha kwa waombaji kusoma na kuzielewa program mbalimbali wanazozihita kuwa zinatolewa katika vyuo vipi. Hivyo kuwa na muda wa kutosha kufuatilia ubora wa vyuo watakavyoviomba kwa ajili ya program husika.

Kwa mwaka huu imekuwa tofauti. Mpaka sasa hakuna hicho kitabu online(yaani hiyo TCU guide book). Je, mnataka kukitoa wakati matokeo ya kidato cha sita yakiwa yametoka?

Sasa vijana waliomaliza kidato cha sita mwaka huu na wa nyuma yao ambao hawakuomba kudahiliwa kwa sababu mbalimbali wapo njia panda kwa tetesi wanazozisikia kuwa mwaka huu watakaodahiliwa vyuo vikuu ni wale wenye ufaulu wa daraja la 1&2 tu. Kama kijitabu hicho kingekuwepo tayari, wala uvumi huu usingewasumbua kwa sababu tayari wangekwisha kujua vigezo ni vipi kwa program mbalimbali. Je, mnasubiri muone ufaulu wa mwaka huu upo je ndiyo mtoke na kitabu chenu? Kwa maana serikali ya awamu hii haieleweki mnaogopa kutumbuliwa eti mmedahili vilaza?

Sisi hatujui yaliyowasibu majibu mnayajua nyinyi sisi kama jamii tunabaki na maswali. Awamu hii kila kitu kama kimesimama kinasubiri maelekezo kutoka juu.
 
Wewe Usihangaike Sana Na TCU, Hebu Omba Chuo unachotaka Directly bila ya Kupitia TCU, au Fungua Mtandao Wa Chuo Husika Unachotaka Na Uombe Online.
Na Katika Mitandao Ya Vyuo Vimo Vigezo Na Ada Za Programs mbali mbali.
 
kaka subiria tcu.siku hizi huwezi kwenda direct chuo kikuu bila aproval ya tcu
 
Wewe Usihangaike Sana Na TCU, Hebu Omba Chuo unachotaka Directly bila ya Kupitia TCU, au Fungua Mtandao Wa Chuo Husika Unachotaka Na Uombe Online.
Na Katika Mitandao Ya Vyuo Vimo Vigezo Na Ada Za Programs mbali mbali.
You can only apply via CAS
 
Wewe Usihangaike Sana Na TCU, Hebu Omba Chuo unachotaka Directly bila ya Kupitia TCU, au Fungua Mtandao Wa Chuo Husika Unachotaka Na Uombe Online.
Na Katika Mitandao Ya Vyuo Vimo Vigezo Na Ada Za Programs mbali mbali.
Hujui unachosema.. Siku hizi ku apply hakupo ivo unavodhania
 
Wewe Usihangaike Sana Na TCU, Hebu Omba Chuo unachotaka Directly bila ya Kupitia TCU, au Fungua Mtandao Wa Chuo Husika Unachotaka Na Uombe Online.
Na Katika Mitandao Ya Vyuo Vimo Vigezo Na Ada Za Programs mbali mbali.
Hivi kweli bado kuna mfumo wa kuomba moja kwa moja? Mbona hata hiyo program ya Aircraft maintenance engineering ya NIT wanaelekeza kuomba TCU? Ada nasikia ni 10mil. TCU guidebook ndo ingetoa majibu.
 
Wewe Usihangaike Sana Na TCU, Hebu Omba Chuo unachotaka Directly bila ya Kupitia TCU, au Fungua Mtandao Wa Chuo Husika Unachotaka Na Uombe Online.
Na Katika Mitandao Ya Vyuo Vimo Vigezo Na Ada Za Programs mbali mbali.
Tangu lini Bachelor Degree ikaombwa hivyo?
 
Hizi taasisi sijui zimekumbwa na nini? Mpaka sasa Nacte awajatoa majina ya waliochaguliwa kujiunga na Ordinary diploma, wameacha watu wengi njia panda. Mfano dogo wangu hataki kwenda advance na ame apply Nacte lakn mpaka sasa wako kimya hajui afanye nn. Naomba kama wako wanaohusika na hizo taasisi wafanye kazi kwa uweledi na wazingatie mda.
 
Back
Top Bottom