TCRA yazipiga rungu kampuni za simu

TCRA yazipiga rungu kampuni za simu

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,247
Reaction score
25,191
Dar es Salaam. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezitoza faini kampuni zote za simu kwa kusajili laini bila vitambulisho na kutofuata utaratibu.

Kampuni zilizotozwa faini hiyo na kiwango kikiwa kwenye mabano ni Airtel (Sh1.08 bilioni), Smart (Sh1.3 bilioni), Vodacom (Sh945 milioni), Zantel (Sh105 milioni) na Halotel (Sh1.6 bilioni).

Mkurugenzi wa TCRA, Mhandisi James Kilaba amesema leo (Julai 14) kuwa hii si mara ya kwanza kwa watoa huduma hao kukiuka sheria.

Kiliba amesema kutokana na kurudia kosa hilo, TCRA imezitoza kampuni hizo faini ambazo Airtel imetozwa Sh542 milioni, Smart (Sh37 milioni), Tigo (Sh625 milioni), Zantel (Sh52 milioni) na Halotel (Sh822 milioni).

Pia, kampuni hizo zimetozwa Sh500 milioni kila moja kwa kosa la kuathiri na kuhatarisha usalama wa umma na jamii ya Watanzania kwa kusajili laini bila kufuata utaratibu.

Chanzo: Mwananchi
 
Duuuuuh nooomaaaaa mkuu hivi MBNA wanapgwa faini kila muda hawakomiii
 
Hela za penalty kila kona......hakika makusanyo lazima yavunje rekodi.
 
Tatizo ni hawa vishoka wao wanaokaa huku barabarani

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Wanaendelea kukusanya kodi kama wale jamaa

Sent from my TECNO-J8 using JamiiForums mobile app
 
Wafuate sheria tu maana wizi wa mtandao unakua kwa sababu ya usajili usio rasmi

Sent from my TECNO W4 using JamiiForums mobile app
 
Hapo wateja tutakoma,watahakikisha tunachangia hiyo kitu kama abiria na watu wengine tutakavyochangia sh. 40 ya mafuta kwenye MVL!!

Sent from my HUAWEI CUN-L21 using JamiiForums mobile app
 
Safi sana...watu wanatapeli, wanafanya uhalifu. Watu wanalamika wanatapeliwa na watu ambao ukienda kwenye kampuni za simu wanashindwa kumpata. Watu wanalamika number hizi zinafanya utapeli zinashindwa kufungiwa? Awamu hii wataka sawa tu.
 
Back
Top Bottom