TCRA yazipiga faini EATV na E-FM

Olmost

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
337
439
Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), imevitoza faini vituo vya East Africa Television na Entertaiment FM (E- FM) baada ya kukiuka kanuni za utangazaji.

Akisoma nakala ya hukumu hiyo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Joseph Mapunda alisema baada ya kupitia maelezo ya utetezi kutoka kwa viongozi wa vituo hivyo, kamati hiyo imeamua kuitoza EATV faini ya Sh3 milioni na Sh4 milioni kwa E-Fm.

“Pamoja na adhabu hiyo tumetoa onyo kali kwa kukiuka kanuni ya maudhui, lakini pia endapo kosa hili litajirudia tunaahidi kutoa adhabu kali zaidi,” alisema.

Katika maelezo ya awali ya hukumu hiyo, Mapunda alisema adhabu ya EATV imetolewa baada ya kituo hicho kupitia kipindi chake cha muziki mnene kurusha video ya wimbo wa Panya wa kundi la muziki la Bracket kutoka nchini Nigeria uliomshirikisha msanii Techno.

“Baadhi ya mavazi yaliyotumika katika wimbo huo hayaendani na maadili ya Kitanzania. Na kwa upande wa E-FM wameadhibiwa baada ya kurusha kipindi cha Ubaoni kilichotoa simulizi ya msichana mchawi aliyekiri kuua,”alisema Mapunda.

Baada ya kupokea nakala ya hukumu hiyo, Mkurugenzi wa EATV, Regina Mengi alisema hawana tatizo na adhabu hiyo na kwamba, atalifikisha suala hilo kwa uongozi wa kampuni yao.

“Bado siwezi kujibu lolote, uamuzi wa kuikubali au kukata rufaa itategemea na uamuzi wa bodi,” alisema.

Mkurugenzi wa E-FM, Scolastica Mazula alisema ameridhishwa na hukumu iliyotolewa, hivyo haoni kama kuna sababu ya kukata rufaa.

Mamlaka hiyo imevitaka vyombo vyote vya utangazaji nchini kuzingatia maadili na taratibu za sheria zinapofanya kazi ili kuepuka kuleta athari katika jamii.
 
Nyimbo inaitwa Panya!! 😂😂
Huu uzi umenipeleka youtube kuona hiyo nyimbo
 
Tz nzima kuna vituo kama 100, kwa wastani adhabu ni mil 4 kwa kituo.
4,000,000 x 100 = 400,000,000.
Labda waipige fine na mitandao ya simu ndio tunaweza kuikomboa ile ndude.
 
Huo wimbo wa Panya je wamewahi kuupiga marufuku hapa nchini au kwa vile mkubwa mmoja hajapenda hayo mavazi akaamua afunike TUTA.

Serikali haniamini katika uchawi na TCRA ni kitengo chini ya serikali, hayo mahojiano waliofanya na huyo binti kukiri kaua wamefuatilia kujua ukweli wa hilo na kama kakiri kaua TCRA kwanini wasisaidie polisi taarifa hiyo ili mtuhumiwa huwa atiwe nguvuni.

Hizo adhabu wala sijaona adhabu yenye sababu zenye kueleweka hapo.
 
Bodi imekubaliana na hukumu, lengo ni fedha kukomboa ndege yetu.... tutalipa.
 
Ndiyo maana raisi anachukiwa na watanzaia kwa kasi ya ajabu,HAWA E FM kosa lao kubwa hapa sio kupiga wimbo wa panya kosa lao ni kutangaza kama vile wanashangilia kukamatwa kwa ndege yetu SOUTH rejea Maulidi wa kitenge....
 
umenena
Ndiyo maana raisi anachukiwa na watanzaia kwa kasi ya ajabu,HAWA E FM kosa lao kubwa hapa sio kupiga wimbo wa panya kosa lao ni kutangaza kama vile wanashangilia kukamatwa kwa ndege yetu SOUTH rejea Maulidi wa kitenge....
 
Huo wimbo wa Panya je wamewahi kuupiga marufuku hapa nchini au kwa vile mkubwa mmoja hajapenda hayo mavazi akaamua afunike TUTA

Mbona hilo vazi ni common sana kule ufukweni na hasa Bagamoyo, je ni jamii gani ina haki kuliona na ipi haina haki maana kuna watu wengi wanavaa hivyo na kujilaza huku wakijipinduapindua kwenye mchanga wa bahari mchana kweupe hakuna anayewatoza faini wala kuwakamata.
 
Kosa lao kubwa hizò Tv ni kuonesha kufurahishwa ilipokamatwa NDEGE ya jamaa yetu huko South.
Mbona hilo vazi ni common sana kule ufukweni na hasa Bagamoyo, je ni jamii gani ina haki kuliona na ipi haina haki maana kuna watu wengi wanavaa hivyo na kujilaza huku wakijipinduapindua kwenye mchanga wa bahari mchana kweupe hakuna anayewatoza faini wala kuwakamata.
 
👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👊🏽👊🏽👊🏽👍🏽

Upumbavu UMETAMALAKI nchini Mkuu.

Eti "maadili ya kitanzania"?

Rushwa, ufisadi, ujinga na umasikini ndio maadili ya kitanzania!?????

Hawa watanganyika hebu waamke waanze kushughulika na ISSUES waachane na hizi trivialities na tuvitu tuvitu uchwara!
 
Back
Top Bottom