TCRA yaweka namba ya kucheki simu fake! Kuanzia tarehe 17 June simu zote fake kufungiwa

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,056
10,721
TCRA wametoa maelekezo ya kucheki simu yako kama ni fake!

Tangazo hili limekuja na onyo kwamba ifikapo mwezi wa sita simu zote fake zitafungiwa.

Unachotakiwa kufanya ni dial *#06# ili upate namba ya IMEI, na kisha hiyo IMEI number uitume kwenda namba 15090.

Hata hivyo, chakushangaza nimetuma namba hiyo nikajibiwa "kama namba ya IMEI haioani na simu, niwasiliane na muuzaji au nibadilishe...".

Swali nitajuaje kama vinaoana au la?
 
kama hawataki simu feki si wazuie zisiingie nchini ambazo ztakuwepo nchini ztaisha tu kwa uchakavu na kuharbka
uzuiaje ndo umeanza kwenye grassroot level sasa yaani nyie watumiaji kwa maaana ya kwamba kama simu ni feki usinunue na ukinunua haifanyi kazi so you have the final decision.
 
Mkuu ukijibiwa IMEI haioani na simu, maana yake ni kwamba simu yako ni fake, hivyo ikifika muda huo inafungwa. Hata I phone 6 zipo fake pia
mkuu labda hujaelewa, wangekua wanajibu kuwa "IMEI yako haioani na SIMU" isingekuwa shida... ila wanachojibu ni "kama IMEI yako haioani na simu yaweza kuwa bandia"

sasa swali ni je nitajuaje kama IMEI haioani na SIMU????
ndio swali ambalo wao walitakiwa kujibu
 
mkuu labda hujaelewa, wangekua wanajibu kuwa "IMEI yako haioani na SIMU" isingekuwa shida... ila wanachojibu ni "kama IMEI yako haioani na simu yaweza kuwa bandia"

sasa swali ni je nitajuaje kama IMEI haioani na SIMU????
ndio swali ambalo wao walitakiwa kujibu
Nimekuelewa sasa mkuu. Mwanzo nilidhani kuwa wao ndio wamejibu, kumbe nao wanasema kama haioani. Hapo kuna utata. Lakini kwa mawazo yangu nadhani kama ukipiga hiyo *#06# kama simu ni fake haitatoa IMEI namba. Hivyo automatically simu kama hiyo inabidi uwasiliane na aliyekuuzia. Labda kuna wanaofahamu zaidi watatuelewesha.
 
Back
Top Bottom