Michael Ngusa
JF-Expert Member
- Aug 4, 2014
- 1,637
- 458
Wadau,
Hawa watu wanasema ifikapo June watazima simu zote feki, ajabu washalamba ushuru wa simu hizo na wao wenyewe (serikali) ndio waliotoa kibali ziingie nchini na kuuzwa. Anyway, swali langu ni dogo tu, je, TCRA wana magical button ya kuswitch off simu zote feki? how do they control our phone countrywide? Ningependa kufahamu the technology behind. Isije kuwa mbwembwe tu.
Hawa watu wanasema ifikapo June watazima simu zote feki, ajabu washalamba ushuru wa simu hizo na wao wenyewe (serikali) ndio waliotoa kibali ziingie nchini na kuuzwa. Anyway, swali langu ni dogo tu, je, TCRA wana magical button ya kuswitch off simu zote feki? how do they control our phone countrywide? Ningependa kufahamu the technology behind. Isije kuwa mbwembwe tu.
Habari ndugu zangu,
Ninachoelewa ni kuwa kutakuwa na utaratibu wa ku-track simu zote za mikononi zilizo katika matumizi kujua kama imesajiliwa na kupewa International Identification (IMEI) na la. Utaratibu huo ambao utatumia kwa sasa haujawekwa wazi kwetu sisi walaji. Lakini mimi binafsi naamini inawezekana kufanya hivyo. Tukumbuke kuwa simu zote ambazo ziko katika matumizi service providers (Kama Tigo, Vodacom Airtel na wengine) wanafahamu huyu mlaji/mteja wetu anatumia simu yenye huo usajili (IMEI) au la, lakini kama mteja/mlaji huyo anatumia simu yenye utambuzi huo basi wanajua ni IMEI gani.
Kwahiyo sasa, pia TCRA nao wana uwezo huohuo na zaidi ya hapo. Lakini haimaanishi kuwa watengenezaji wa simu (manufacturers) wataleta orodha ya simu zao na IMEI zao na kuwakabidgi TCRA.. NO doesn't work like that. Hawa service providers wote wanaitambua kila handset kwa IMEI yake kwa zile zote zenye IMEI. Na wanajua kuwa mteja huyu anatumia simu ambayo hana international identification (IMEI) au la. Ndio maana leo hii kama una kumbukumbu ya IMEI ya simu yako then ikaibiwa popote au kupotea.. kisha ikienda tu hewani (yaani mtu mwingine akawa anaitumia) basi inaweza kuwa tracked. Inakuwa tracked kwa kutumia IMEI hiyo. Kwahiyo mfumo wa kum-track mtu huyo ni kwamba IMEI hiyo inakuwa linked na namba ya simu hiyo kisha tower zina-locate mtu alipo.
Kwa faida ya wasomaji wengi, mnaweza kuchungulia IMEI ya simu yako kwa kufungua mtandao huu Check IMEI - IMEI.info ingawa nitahadhalishe kuwa huu mtandao hauhusiani na mfumo wa TCRA kuhakiki IMEI ya simu yako.
Lugha ya kienyeji wanasema "watazima simu zote" haimaanishi simu ambazo IMEI zake haziko registered zitazimika, No.. ila zitakuwa disabled, wakifanya hivyo hazitaweza kuunganisha na service provider hata kama ina SIM card.
Asante kwako.