TCRA yaiamuru Star Tv kurudi Star Times kabla ya 10 jioni leo!

Rutunga M

JF-Expert Member
Mar 16, 2009
1,769
1,382
994804_10200120919412242_1852012791_n.jpg



Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Prof. John Nkoma akitoa maamuzi kuhusu kujitoa kwa Star TV kwenye Star Times.

TCRA imeagiza Chaneli ya Star Tv irudishwe mara moja kwenye Star Times kabla ya saa kumi jioni leo.

Aidha Star Times na Star TV wameelezwa kuwa wote wamevunja sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya 2010 na Kanuni zake na kutakuwa kujitetea tarehe 17 Juni 2013.

Agizo la kurudishwa kwa Chaneli ya Star TV linatakiwa kutekelezwa ili kuhakikisha kuwa wananchi hawanyimwi haki ya kupata habari.

Vile vile wote wametakiwa kufuata Sheria inapotokea kutokuafikiana badala ya kutoa maamuzi bila kumshirikisha Mdhibiti (TCRA)


=======================
Ufafanuzi toka TCRA
=======================

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
TANZANIA COMMUNICATIONS REGULATORY AUTHORITY


Ref. No. A. 70/225/30 Date: 06th June, 2013
Managing Director
Star Media (Tanzania) Limited
P.O.Box 33622,
Mikocheni
DAR ES SALAAM


RE: IN THE MATTER OF REMOVAL OF STAR TELEVISION FREE TO AIR SIGNALS FROM STAR MEDIA DIGITAL PLATFORM

COMPLIANCE ORDER

(Issued pursuant to Section 45 of the Tanzania
Communications Regulatory Authority Act, Cap. 172 of the Laws of Tanzania as amended by Section 179 of the Electronic and Postal Communications Act, Cap. 306 of the Laws of Tanzania)

WHEREAS:
A. On 8th June, 2010 the Tanzania Communications Regulatory Authority
(herein after referred to as "the AUTHORITY") issued to Star Media (Tanzania) Limited (herein after referred to as "the LICENSEE") Network Facilities License (herein after referred to as the "LICENCE") for provision of signal transmission services (herein after referred to as "the SERVICES"), and was assigned frequencies for provision of the Licensed services, and;

B. Under the LICENCE the LICENSEE is obliged to ensure that all free to air channels are accessible without any subscription fees on any digital platform through an integrated digital television or a set top box;

C. On the 9th day of June, 2013 the AUTHORITY apprehended that the LICENSEE had removed from its digital platform the free to air signals of Star Television (herein after referred to as the "CONTENT SERVICE PROVIDER");

NOW THEREFORE the AUTHORITY does hereby:

1. DECLARE that the LICENSEE'S removal from the digital platform of the free to air signals of the CONTENT SERVICE PROVIDER contravenes the must carry obligation of the LICENSEE as prescribed under Regulation 14(2)(a) and availability of services obligation as prescribed under Regulation 13(2)(h) of the Electronic and Postal Communications (Digital and Other Broadcasting Networks) Regulations, G.N. Number 418 of 2011; all of which amount to breach of license obligation;

2. ORDER the LICENSEE to resume the must carry obligation and re-instate in the digital platform the free to air signals of the CONTENT SERVICE PROVIDER by this 10th day of June, 2013 before 4.00 p.m.;

3. ORDER the LICENSEE to appear before the AUTHORITY on Monday 17th June, 2013 at 10.00 a.m. to show cause why legal and regulatory actions should not be taken against it for abdicating its must carry obligation, thus contravening Regulations 14(2)(a) and 13(2)(h) of the Electronic and Postal Communications (Digital and Other Broadcasting Networks) Regulations, G.N. Number 418 of 2011.

Should the Licensee fail, neglect or refuse to comply with this Order, the Authority will proceed to take legal and regulatory actions without any further notice and at the Licensee's own risk as to costs and consequences of the legal and regulatory actions.


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
TANZANIA COMMUNICATIONS REGULATORY AUTHORITY

Ref. No. A. 70/225/30 Date: 06th June, 2013
Managing Director
Star Television
P.O.Box 1732,
MWANZA

RE: IN THE MATTER OF WITHDRAWAL OF STAR TELEVISION FREE TO AIR SIGNALS FROM STAR MEDIA DIGITAL PLATFORM

COMPLIANCE ORDER

(Issued pursuant to Section 45 of the Tanzania
Communications Regulatory Authority Act, Cap. 172 of the Laws of Tanzania as amended by Section 179 of the Electronic and Postal Communications Act, Cap. 306 of the Laws of Tanzania)

WHEREAS:
A. On 16th June, 2000 the Tanzania Communications Regulatory Authority
(herein after referred to as "the AUTHORITY") issued to Star Television (herein after referred to as "the LICENCEE") a Content Services (TV) Licence (herein after referred to as the "LICENCE") for provision of television content services (herein after referred to as "the SERVICES"), and;

B. Under the LICENCE the LICENSEE is prohibited from intentionally interrupting or suspending the operation of the licensed system and services in the normal course of business without having first notified the AUTHORITY in writing and having provided reasonable advance notice to persons affected or likely to be affected by such interruption or suspension;
C. On the 9th day of June, 2013 the AUTHORITY apprehended that the LICENSEE had instructed Star Media (Tanzania) Limited (herein after referred to as the "MULTIPLEX OPERATOR") to remove from its digital platform the free to air signals of Star Television;

NOW THEREFORE the AUTHORITY does hereby:

1. DECLARE that the LICENSEE'S withdrawal of its free to air signals from the digital platform of the MULTIPLEX OPERATOR amounts to intentionally interrupting or suspending the operation of the licensed system and services in the normal course of business without having first notified the AUTHORITY in writing and having provided reasonable advance notice to persons affected or likely to be affected by such interruption or suspension contrary to the provisions of Regulation 19(1) of the Electronic and Postal Communications (Digital and Other Broadcasting Networks) Regulations, G.N. Number 418 of 2011 and is also a breach of the quality of service as enshrined under Regulation 13(2)(h) of the same G.N. Number 418 of 2011 as regards availability of services, all of which amount to breach of license obligation;

2. ORDER the LICENSEE to re-instate transmission of its free to air signals through the MULTIPLEX OPERATOR by this 10th day of June, 2013 before 4.00 p.m.;

3. ORDER the LICENSEE to appear before the AUTHORITY on Monday 17th June, 2013 at 11.00 a.m. to show cause why legal and regulatory actions should not be taken against it for abdicating its obligation, thus contravening
the provisions of Regulations 19(1) and 13(2)(h) of the Electronic and Postal Communications (Digital and Other Broadcasting Networks) Regulations, G.N. Number 418 of 2011.

Should the Licensee fail, neglect or refuse to comply with this Order, the Authority will proceed to take legal and regulatory actions without any further notice and at the Licensee's own risk as to costs and consequences of the legal and regulatory actions.
Star TV ni free to air. Masharti ya leseni yao inawataka wawe hewani bila malipo, wakitaka premium channel basi hawaruhusiwi kuchukua matangazo ya biashara. Tafadhali angalia masharti ya leseni za free to air kabla ya kupotosha kwa hisia. Ukiomba leseni lazima ukubaliane na masharti ya aina ya leseni uliyoomba.

Ni vizuri kuwa na uhakika na kufuata taratibu, Sheria na kanuni za utangazaji. Ukipitia Sheria ya EPOCA na kanuni zake, baadhi ya yaliyotolewa humu ni upotoshaji. TCRA hata siku moja haitajibu tuhuma zinazoongozwa na hisia, tunafanya Kazi zetu kwa mujibu Wa sheria.

Tunaheshimu mawazo na ushauri unaotolewa kwa nia njema. Aidha kila raia ana uhuru kamili kutoa mawazo na hisia zake. Tcra haifanyi kazi kwa matakwa ya kila mtu ambavyo angependa tufanye, wala hatuingilii mawazo yenye nia ya kuharibu au kukejeli. Mtusamehe pale tutakapokaa kimya tunapokna post za kashfa, kejeli au dharau.

Ni vizuri kufuata Sheria, kufanya utafiti kwa jambo husika kabla ya kulaumu au kutoa maneno yanayowachanganya wananchi.

======================
Ufafanuzi toka Star TV
======================


attachment.php



Kwa taarifa kamili pakua file lililoambatanishwa:


Taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu Star TV kujiondoa Star Times.

Tarehe 23 Mei 2013 Star TV kupitia mwanasheria wake iliwataka Star-Times kuiondoa kwenye king'amuzi chao ifikapo saa sita usiku wa tarehe 31 Mei kutokana na kurusha na kuuza maudhui na vipindi vyake bila idhini hivyo kukiuka sheria za haki miliki (Copyright laws).

Katika barua hiyo Star TV iliwakumbusha Star Times kwamba hawakuwa na mkataba wa kurusha kituo hicho kwa mujibu wa sheria ya Mawasiliano EPOCA pia hawana haki ya kutumia maudhui yake bila idhini chini ya sheria ya haki miliki ya Tanzania na Kimataifa.
Tarehe 31 Mei 2013 Star Times/Star Media walijibu na kudai kwamba hawajakiuka sheria yoyote wakasisitiza wataendelea kuirusha Star TV kutekeleza matakwa ya sheria ya EPOCA na kanuni zake.

Tarehe 6 Mei 2013 Star TV iliwaandikia tena Star Times ikisisitiza nia yake ya kuchukua hatua zaidi kutokana na wao kuendelea kukaidi ombi hilo na kuainisha mapungufu kadhaa ya kisheria kwa upande wao yanayoifanya Star TV ijiondoe kwenye king'amuzi chao ifikapo saa sita usiku wa tarehe 08 Mei 20013. Star TV Ilieleza Star Media (T) Ltd. ambayo inamilikiwa kwa pamoja na Star Times
na TBC ina leseni ya miundo mbinu ya kurusha matangazo ya Televisheni kupitia mfumo wa DTT (Multiplex Operator License).

Leseni hiyo inawaruhusu kuingia makubaliano (Service Level Agreement- SLA) na vituo mbalimbali kuwarushia matangazo yao lakini Star-Times hawana leseni ya kutoa huduma ya maudhui (Content Service Provider License-CSP). Star Times ni kampuni ya kimataifa iliyoandikishwa (China) inayotoa huduma ya maudhui katika nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo Tanzania. Ili kupata maudhui inalazimika kuingia mikataba na vituo vya televisheni kabla ya kuviingiza kwenye king'amuzi chake na baadaye kuuza maudhui hayo subscription/Pay TV) kwa watumiaji katika mataifa hayo.

Star Times inachukua vituo vya TV ikiwemo Star TV bila idhini yao na kuviweka kwenye king'amuzi chake kwa kisingizio kwamba wanaruhusiwa na sheria ya EPOCA na Kanuni zake. Sheria hiyo inasisitiza juu ya kuwepo kwa mkataba wa makubaliano (SLA) kati ya pande mbili husika.

Kwamba maudhui ya TV za Tanzania yanauzwa kwa watumiaji katika nchi nyingine kama vile Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda, Nigeria na nyinginezo bila idhini ya wamiliki wake. TV zinazomiliki maudhui hapa nchini hazina uwezo wa kuidhibiti Star Times isirushe maudhui yao nje ya Tanzania kwa kuwa baadhi ya maudhui wanayoyanunua nje kama vile tamthilia na vipindi vingineyo haviruhusiwi na watunzi au wasambazaji wake yarushwe nje ya Tanzania (Territorial Rights).

Lakini pia uhusiano wa makampuni haya mawili Star Media (T) Ltd na kampuni ya Star Times ambayo ni ya China yenye matawi katika nchi mbalimbali za Afrika katika uendeshaji wa matangazo ya Dijitali haujabainishwa vizuri ili kujua nani ni nani na nini anachofanya hapa Tanzania katika misingi ya maelewano ya kibiashara.

Ni kutokana na mantiki ya hoja hizo Star Times waliondoa mara moja Star TV kwenye king'amuzi chao tarehe 08 June 2013 kama walivyoelekezwa na Star TV. Star TV haioni sababu ya kulazimishwa na TCRA kurushwa na Star Times pasipo kuondoa hitilafu hizo za kisheria na bila kuangalia sheria nyingine zinazolinda haki za TV huru kama sheria ya haki miliki na sheria ya ushindani katika soko moja. TCRA kwa kutozingatia hili, inabeba umiliki wa sheria hata zisizokuwa chini ya mamlaka yao (supra organ).

Taarifa iliyotolewa magazetini na Meneja Mawasiliano wa TCRA Innocent Mungy kwamba chaneli tano za kitaifa lazima zirushwe na ving'amuzi vyote bure ni za kupotosha kwa kuwa hata hiyo Star Times haizirushi bure imekuwa ikibadilika badilika mara kwa mara pasipo TCRA kuwachukulia hatua za kisheria licha ya wananchi kulalamika kwamba wanatozwa pesa ili kuona.

Hata hivyo Vituo vikubwa vya TV vikiwemo Star TV, ITV, Channel 10 na TBC na vinginevyo visivyo vya kitaifa vinarushwa na akampuni ya BTL na TING bila malipo yoyote ya mwezi na kwa ubora zaidi kuliko Star Times lakini inashangaza kuona TCRA nawakingia kifua Star Times wanaowalipisha watanzania badala ya kutetea vituo vya ndani visivyotoza chochote.

Star TV inarusha matangazo yake bure kwa wananchi na matangazo hayo yanaweza kuonekana kupitia king'amuzi chochote ambacho kina ubora na kuweza kung'amua matangazo ya bure (Free To Air - FTA). Hata hivyo kwa uchunguzi ilioufanya Star TV
imegundua kwamba ving'amuzi vya Star-Times vimefungwa kupokea matangazo ya FTA kutoka kwa warushaji wengine (network locked). Jambo ambalo linakinzana na sheria za EPOCA na hivyo matangazo ya chaneli ambazo ni FTA hayaonekani kwenye Star Times mpaka wayarushe kutoka minara yao na hivyo kupoteza dhana nzima ya FTA, (kwa maana kwamba wana [re-broadcast] chaneli za FTA badala ya kuonekana moja kwa moja kutoka kwa wamiliki).

Star TV inaamini kwamba kazi ya usimamimizi wa matangazo ya TV inayofanywa na TCRA haipaswi kupendelea upande wowote na haipaswi kuingilia masuala ya kibiashara kuilinda Star Times kwa kuwa sio jukumu lao. Kwa mfano, Star TV na TV nyinginezo nchini zilizimiwa matangazo yao ya analojia na TCRA pahala mbalimbali na hivyo kuwalazimu wananchi kununua ving'amuzi vya Star Times bila dhana nzima ya ushindani na uwezeshwaji wa washindani wa ndani kutiliwa maanani na hivyo kuwanyima Watanzania haki yao ya kupata habari.

Sasa miundo mbinu ya humu nchini imejengwa na kampuni za kizalendo kwa gharama kubwa na kwa ubora zaidi kuliko Star-Times. Sasa inaelekea ushindani umewaelemea Star-Times, hivyo TCRA inajaribu kuwasaidia tena. Hili halikubaliki na tupo tayari uwaonyesha watanzania matumizi mabaya ya chombo hiki kwa maslahi ya wageni na watu wachache wasio waaminifu kwa nchi yao.

Pamoja na kazi ngumu ya kujenga miundo mbinu ya DTT ambayo imewakamua wawekezaji wa Kitanzania, Mkurugenzi wa TCRA hajawahi kuwatembelea kuwatia moyo. Star TV inapinga kwa nguvu zote TCRA kufanya usimamizi kwa mtizamo wa kibiashara kwa kujaribu kuwasaidia Star-Times ambao, nia yao ni kupata bure matangazo yanayotayarishwa kwa gharama kubwa na vituo vya Tanzania na kuhodhi urushaji wa maudhui ya TV za humu nchini kupitia DTT kwa faida yao. Kimsingi Star-Times ni TV ya kigeni na kwa mujibu wa sheria mpya ya EPOCA haistahili kupewa leseni ya ndani ya maudhui kushindana kama local TV.


Hata hivyo, kama inadaiwa kwamba Star Media (T) Ltd na Star Times ni kitu kimoja basi kampuni zote mbili zinafanya kazi kinyume cha sheria ya EPOCA na kanuni zake ambayo kwa mujibu wa kifungu cha 12(h) kinaonyesha jinsi mwenye leseni ya miundo mbinu (Multiplex) anavyotakiwa kutekeleza majukumu yake. Kinasema:"Multiplex Operator hataruhusiwa kurusha maudhui yake mwenyewe, vituo vyake vya TV au kifurushi chenye maudhui yake (Bouquet)".


Kwa hiyo Star TV haiko tayari kujihusisha na Star-Times au kufanya biashara na chombo chochote ambacho mwenendo wake wa kibiashara haufuati matakwa ya sheria. Pia, Star-TV haikubali kusukumwa kwenye makubaliano ya kibiashara kwa matumizi ya nguvu na tafsiri potofu ya sheria zetu. Hii ni kugombanisha watanzania kwa kutumia sheria zao wenyewe zinazotafsiriwa vibaya kukidhi tamaa ya watu wachache.


Intellectual Property Rights ni mali ya mwenye nacho, sio mali ya serikali na hivyo hakuna mtu wa kuamrisha mtu atoe kipindi, wimbo, sanaa, shairi, au mchezo wake kwa mtu mwingine. Sheria ya Hatimilki imetungwa ikizingatia maelekezo ya shirika la biashara la kimataifa (WTO), na Shirika la utambuzi wa hakimilki la kimataifa (WIPO), ambayo Tanzania ni mwanachama. Kulazimisha mtu kutoa haki yake ni uvunjaji wa sheria na haki za kibinadamu. Hakuna yeyote hata kama ni nani anayo haki hiyo isipokuwa mwenye nacho. Tupo tayari kutafuta haki hii mahakamani kama TCRA wanataka tufanye hivyo!


Imetolewa na Meneja Mipango na Utafiti wa Sahara Media Group Ltd.
Nathan Lwehabura
kwa niaba ya uongozi.
 
Star times , TCRA wote lao moja. TCRA huwa hawaangalii TV waone watu wanavyokatikakatika na star times???? kazi kutoa matamko tu quality kwao zero.
 
Walioshika dili la ving'amuzi vya startimes.
Inaonekana bado havijawalipa vizuri.!!
 
star time hawana lolote wehu tu,

Hata kama hawana lo lote hao star time, pamoja na kero zao, hata hivyo Star TV hawana right ya kujiondoa kwenye king'amuzi ambacho ni haki yetu kuwaona. Juzi ilibidi nihamie kwenye king'amuzi cha DSTv kwa kuwa there was a programme nilikuwa naangalia Star TV kupitia hicho king'amuzi. Afadhali.
 
Bado wananchi wananyimwa haki yao ya kupata habari kwa kutakiwa kulipia kila mwezi kwenye kampuni za ving'amuzi hili kuweza kupata local channel ambazo zinatakiwa kuwa bure.

Sio watu wote wana uwezo wa kulipia kwa mwezi. Hizo local channels zilitakiwa kupatikana kwa kununua converter box kwa watu wenye tv za zamani hili waweze kuona hizo channel kwa kutumia antena zao za zamani.

Serikali inakurupuka sana kwenye maamuzi bila kujali hali halisi ya mtanzania.
 
good newz,...at least tcra wamejaribu kutoa maamuzi magumu na mazuri i.e for public interest.
 
Hata kama hawana lo lote hao star time, pamoja na kero zao, hata hivyo Star TV hawana right ya kujiondoa kwenye king'amuzi ambacho ni haki yetu kuwaona. Juzi ilibidi nihamie kwenye king'amuzi cha DSTv kwa kuwa there was a programme nilikuwa naangalia Star TV kupitia hicho king'amuzi. Afadhali.

kweli kabsa kaka...yan star tv walikera sana...hawana haki ya kujitoa kwan wanatunyima haki yetu ya kupata habari
 
Hata kama hawana lo lote hao star time, pamoja na kero zao, hata hivyo Star TV hawana right ya kujiondoa kwenye king'amuzi ambacho ni haki yetu kuwaona. Juzi ilibidi nihamie kwenye king'amuzi cha DSTv kwa kuwa there was a programme nilikuwa naangalia Star TV kupitia hicho king'amuzi. Afadhali.

Hivi ni nani anakupa wewe haki ya kuwaona Star TV ?, na kwanini hio haki asiwe nayo mwenye product either aionyeshe bure au aifanye premium ?

Hawa TCRA waache kutumia mabavu waongee na Star TV ili kama TBC inapewa ruzuku za kujiendesha basi hivyo hivyo waangalie na hawa wengine. Nadhani mwenye product anayo haki product yake iendeshwe vipi.., na kumbuka merit anayopata mtu kwenye Free to Air Channels ni matangazo (sasa kama anaona matangazo hayalipi tena) ni nani wa kumlazimisha asibadilishe product yake from Free to Air na kuwa Premium ? au hio ndio Haki ?
 
TCRA nao ni janga lingine la kitaifa tu, hawana maana. Walisema ving'amuzi vyote vitakuwa na channels zote za bure nchini, lakini wameahindwa kusimamia hilo. Pia waliamua kuzima analogue bila kujali ubora wa kampuni za digital walizowapa leseni. Ving'amuzi vingi vina quality za hovyo, na ukienda km chache tu pembeni ya mji hazikamati. Alafu eti tunaambiwa wizara na TCRA yenyewe zinaongozwa na maprofesa!!! My foot...
 
Na wale TBCCM ambao mara waonekanae mara wasionekane inakuaje? hapa huu ni upuuzi mtupu wala hamna lolote
 
Back
Top Bottom