TCRA yachemka kwa Star times

TCRA yachemka kwa Star times

SN.BARRY

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2012
Posts
4,049
Reaction score
8,997
Ni kuhusu malipo ya bure kwa TV za ndani. Startime wamegoma kabisaaa hadi dakika hii nakwenda hewani. Jamaa walitoa tamko kutafuta kiki ya mwisho wa mwaka ila wamekutana na watoto wa mjini zaidi yao.
 
Hawa Tcra meno yao yako kwenye kutoza faini vyombo vya habari vile vinavyoandika kinyume na mitazamo ya mkulu
 
Dawa ya hawa star times ni kuwadukua tu na sisi tuangalie bure. Kwanza nilisikia hawalipi Kodi
 
Huwa nashangaa eti watu kuambiwa kuna mabadiliko ya kiutendaji nchi hii. Hao TCRA sio mara moja tumewaandikia e-mail na wala hawajibu huu uhuni unaofanywa na hayo makampuni. Ukienda kwenye ofisi za hao jamaa wa ving'amuzi utakuta wanakutoza malipo ya kubadili smart card eti ili uone hizo local channels bure.

Kuna wakati napata hisia ni mchezo unachezwa kati ya hao watu na serikali ili kuibia wananchi wake. Ni nani hajasikia hilo tangazo la TCRA kuhusu local channels kuwa bure, na kwanini halitekelezwi bali ya kurudiwarudiwa kila mara?
 
Nilisha wahi wauliza startimes wakasema haiwezekani wao walipie local Chanel afu wafanye bure kuzionesha so wataendelea kuziuza, nadhani kunatatizo some where.
 
Hakuna chombo cha habari kinachoweza kuandika wala kutangaza habari hii, maana nao utakuwa UCHOCHEZI
 
Nilisha wahi wauliza startimes wakasema haiwezekani wao walipie local Chanel afu wafanye bure kuzionesha so wataendelea kuziuza, nadhani kunatatizo some where.
Tatizo ni TCRA kutoweza kutekeleza wanachozungumza au kudanganya wananchi.
 
Naamini ingekua muda wa uchaguzi umekaribia,hakika TCRA ingefanya kila njia hadi wenye ving'amuzi waachie chanels za ndani kuonekana.
 
No kihusu malipo ya bure kwa TV za ndani. Star time wamegoma kabisaaa hadi dakika hii nakwenda hewani. Jamaa walitoa tamko kutafuta kiki ya mwisho wa mwaka ika wamekutana na watoto was mjini zaidi yao.
Wajua hili tamko liko kisiasa zaidi kwakuwa ili warushe hizo channel bure inabidi wenye hizo channel walipe kampuni za ving'amuzi kufanya hivyo wasipolipa hawazirushi.
Hapo ndipo utata ulipo ndiyo maana naona hili jambo haliwezekani
 
juzi niliwapigia simu huduma kwa wateja star times nikaambiwa : inabidi niende ofisini kwao na kadi ya kisimbuzi chao na sh. 24,000/= 12,000 za kubadili kadi na 12,000 za kupata huduma. Bahati nzuri kingamuzi sio changu ni cha mwajiri wangu vinginevyo ningekitia kiberiti!
 
Ni upuuzi mtu kununua decoder afu ategemee channel za bure
 
Huwa nashangaa eti watu kuambiwa kuna mabadiliko ya kiutendaji nchi hii. Hao TCRA sio mara moja tumewaandikia e-mail na wala hawajibu huu uhuni unaofanywa na hayo makampuni. Ukienda kwenye ofisi za hao jamaa wa ving'amuzi utakuta wanakutoza malipo ya kubadili smart card eti ili uone hizo local channels bure. Kuna wakati napata hisia ni mchezo unachezwa kati ya hao watu na serekali ili kuibia wananchi wake. Ni nani hajasikia hilo tangazo la TCRA kuhusu local channels kuwa bure, na kwanini halitekelezwi bali ya kurudiwarudiwa kila mara?
Hapo ndio huwa naona watz wengi wajinga. Kabisa unakuta wanapongeza kwa mabadiliko. Mabadiliko yepi?eti rushwa imeisha,wakati huohuo kuna jitu lina vyeti feki na ni RC?nini maana ya rushwa?
 
Tanzania kila kitu Blah! Blah! Blah!

Maneno mengi ila utekelezaji sifuri.

 
Dah aisee napata wakati mgumu sana kuielewa kauli ya TCRA. Kutokana na vyuma kukaza kutokana na kauli ile niliamua nisinunue vifurushi niangalie local Chanel tu bure, kifurushi cha awali kilipoisha nikaachiwa TBC1 tu.
 
TCRA wanaongopea wananchi?
Mbona kauli zao makampuni hayatekelezi, au tunachezewa?
 
Back
Top Bottom