TCRA watizameni Airtel ni wezi sana

Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
17,034
7,590
Hawa jamaa wa hovyo sana. Wiki moja imepita nilianza kujiunga na kifurushi cha wiki dakka 31 kwa 2000, baada ya siku mbili wakati natuma text nikaambiwa sina sijajiunga kifurushi chochote. Nikajiuliza limetokeaje nikakosa majibu, nikaachana nao. Haikunisumbua sana nikaamua kujiunga tena kwa kiwango kile kile. Hazikuisha siku tatu nikaambiwa sina kifurushi, niseme ukweli kabisa mie si mtumiaji Sana wa simu. Huwa kuna wakati naweza kumaliza siku saba za wiki nikiwa na hata dakka 5 zote, sasa haziishi siku mbili naambiwa tena sina kifurushi, niliumia nikaachana nao.

Leo sasa nilikuwa sehemu mbovu nikatafuta vocha sikuweza kupata, nikaamua kuomba mkopo kupitia *149*49#. Nikachagua daka salio kisha nikaomba Tshs 1999 nikapewa, nikaingia kujiunga nikaomba mitandao yote nikakubaliwa nikapata kifurushi cha dkka 31 na meseji zake nyingi na meseji nikaletewa. Hajabu nimepiga simu kama tatu zisizozidi dakka 10 kwa jumla ghafla naambiwa sina Salio. Nikajaribu kuangalia salio la kifurushi nikaambiwa sijajiunga, ikabidi nipige 100. Majibu niliyopewa ni kwamba, ule mkopo wa daka salio hauruhusiwi kujiunga kifurushi chochote, nikashangaa. Kwanini iko hivyo na kwanini haya maelezo hayapo wakati unauomba hayaonekani popote ili kunielekeza mie nisifanye hivyo? Mhudumu hakunijibu, nikamuuliza tena. Iweje mmerespond kuonesha mmeniunga kwenye hicho kifurushi tena kwa kunitumia meseji na sahivi mnaniambia huo mkopo hauruhusu hicho kifurushi, ni kwanini mlinipa move forward wakati si harari? Yaani mnamwacha mteja ajiunge then akishajiunga ndo mnasema alikosea, kwanini hamtoi maelekezo kabla? Je, huu si wizi nao?

Hawa jamaa nimekuja kugundua wana mbinu nyingi sana za kutuchezea na kutuibia, kama TCRA mtashindwa kuwachukulia hawa jamaa hatua sie wateja hatutakuwa na namna zaidi ya kuwahama. Pesa zetu zinatengenezewa mazingira ya kutafunwa. Haivumiliki kwa kweli.
 
Back
Top Bottom