TCRA wanamlinda Mwigulu Nchemba? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TCRA wanamlinda Mwigulu Nchemba?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by makoye2009, Jul 25, 2012.

 1. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Baada ya Mbunge wa CCM Bwana Mwigulu Nchemba kutoa tuhuma nzito Bungeni kuwa ametishiwa maisha na Wabunge wa CHADEMA kwa njia ya SMS kupitia simu za mkononi imebainika kuwa SMS hizo ni za kughushi kupitia mfumo wa Mawasiliano wa SMSGang. Inasikitisha kuwa mpaka sasa Tume ya Mawasiliano(TCRA) ambao ni wadhibiti wa mifumo yote ya Mawasiliano wamekaa kimya!!!


  Mfumo wa SMSGang ni mtandao ambao mtu anaweza akatuma SMS kwenda namba yoyote ya simu ya mkononi bila kujulikana kwa vile anaweza kuandika namba bandia kwenye sehemu ya KUTOKA(From:) kama inavyoonyesha hapa chini:

  [​IMG]
  Spoof SMS Service. Send anonymous SMS from any number or name

  To send web SMS fill form below!
  Make surprise send fun SMS or jokes for your love :)

  [TABLE]
  [TR]
  [TD]SMS To:

  [/TD]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]From:

  [/TD]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Pincode:

  [/TD]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Text Message:

  Non-English characters? Send SMS in Unicode (70 symbols)

  [/TD]
  [TD]160 symbols left

  70 symbols left
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][/TD]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  reset

  SMSGang.com is a SMS spoofing service that you can use to send anonymous SMS jokes and spoof text messages to your friends worldwide. To spoof means to appear from somewhere or someone else than the original number. When you use SMSGang.com receiver won't understand that text message is fake and sent online. Basically to send spoof sms by GSM standard you can use up to 11 alphabetical characters or up to 15 numeric characters.
  Feel free yo use our anonymous SMS jokes database for spoofing, but don't send illegal text messages, we keep all informaton about you.
  Tags: sms text, anonymous sms, dirty sms, sms sender, sms spoofing, sms to any mumber, flirt sms messages

  Hi there! [TABLE]
  [TR]
  [TD]You are from Tanzania, United Republic of
  [/TD]
  [TD][​IMG]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 2"]You can send SMS to Tanzania, United Republic of
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [​IMG]

  SMS Text Examples

  SMS From: Sniper
  Text: Please take one step to the left.
  I dont see you!

  (Category: Best SMS messages)
  SMS From: Girlfriend
  Text:I know you think I'm cute, I know you think I'm fine, but like the other guys, take a number and wait in line!
  (Category: Flirt SMS messages)
  SMS From: Boyfriend
  Text: Please buy toilet paper and come home immediately!
  (Category: Dirty SMS jokes)


  TCRA wanatakiwa watoe maelezo ya kina kuhusu habari hizi za kupotosha Watanzania kwa kutumia mifumo ambayo inaweza kuhatarisha amani ya nchi na Watanzania wote kwa ujumla. Kama TCRA wataendelea kulinyamazia tatizo hili basi Watanzania tutajua kuwa TCRA wako kwa ajili ya kulinda Serikali ya CCM ambayo kwa kuwatumia viongozi wake wanaweza kutumia mifumo ya Mawasiliano kwa maslahi yao wenyewe.

  Mimi naamini kabisa kuwa TCRA wana taarifa hizi na wanajua kinachoendelea nyuma ya pazia unless watuambie kuwa hawana wataalamu wenye weledi wa kugundua upuuzi huu unaofanya na kina Mwigulu Nchemba na Nnape Nauye.Kitu ambacho si kweli hata kidogo.

  TCRA wamekuwa ni kama kichaka cha kuficha madhambi na maovu yanayofanywa na mifumo mbalimbali ya mawasiliano nchini yakiwemo Makampuni ya simu za mikononi(Mobile operators) ambayo huwa yanawakamua Watanzania kwa gharama kubwa za kupiga simu,kutuma sms na internet. Pia makampuni haya yamekuwa yakiwasumbua Watumiaji wa simu za mikononi kwa kuwatumia SMS ambazo hazina lazima(garbage sms) ambazo huleta usumbufu mkubwa kwa watumiaji lakini TCRA wakiwa hawafanyi lolote.

  Tunaomba TCRA wafanye kazi zao kwa weledi ikiwemo kufuatilia hizi SMS za Mwigulu Nchemba kujua zilitumwa saa ngapi,toka simu gani na ya mtandao upi. Watu tunajua kuwa hakuna simu yoyote inaweza kutuma/kupokea SMS au kupigiwa/kupiga halafu isiweke kumbumbuku kwenye mitambo mama(BASE Station) au MSC(Mobile Switching Centre)ambayo inapatikana kwenye kila kampuni inayofanya biashara ya simu ziwe za mkononi au za mezani. Kinachotakia ni Wataaalmu wa TCRA wakishirikiana na Wahandisi(IT/Telecommunication Engineers) wa Kampuni husika ku-retrieve/trace history kwenye Data base yake kupata hizo kumbukumbu ili kujua ukweli wa sakata hili na hatimaye kukomesha kabisa huu ujinga.

  Nawasilisha
   
 2. bakuza

  bakuza JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2012
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 488
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nani atafanya hayo wakati nao wanahusika na upuuzi huu....
   
 3. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Hatuna TCRA wazalendo HUMU JF?

  Wafanye hiyo kazi bana.lol!
   
 4. L

  Lugeye JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 18, 2011
  Messages: 1,080
  Likes Received: 1,379
  Trophy Points: 280
  january hawezi kumtosa mwigulu
   
 5. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nilichogundua Serikali ya JK ni janga la kitaifa, hakuna kitu inafanyika ni genge la wahuni. Na sasa hivi wamemaliza public fund wanaingia kwenye individual fund zetu ambazo huwa tunajipatia toka mifuko ya hifadhi ya jamii. Binafsi sijakubali bora damu imwagike.
   
 6. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Naomba kuulizwa mimi nimetumiwa SMS imeonesha inatoka kwa number ya Mr X.

  Lakini kumbe hiyo SMS ni spoofing/fake.

  Je mimi niliyetumia SMS kuna njia ya kutambua hiyo SMS ni fake au real? Yaani imetoka kweli kwa Mr. X, au simu ya Mr. X imeingiliwa?

  kama mimi mpokeaji siwezi kutambua kwamba hiyo SMS niliyotumiwa ni fake, Je huo hauwezi kuwa utetezi wa Mwingulu Nchemba aka Lameck Mkumbo Madelu?
   
 7. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #7
  Jul 25, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Kasheshe hapo ni hao waliotuma hiyo sms fake walitumwa na nani....
   
 8. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,570
  Likes Received: 571
  Trophy Points: 280
  Mwigulu laazima atakuwa ndio masterplan wa hilo, haiwezekani ikawa alikuwa hajui! Na kwaupeo wake atakuwemo tuu!
   
 9. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #9
  Jul 25, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,570
  Likes Received: 571
  Trophy Points: 280
  Kinachonifanya niamini kuwa ni masterplan ni michango ya hovyo kwa kujiamini! Huwa hajitambui na analack chalisma!
   
 10. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #10
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Bobuk,

  Kwenye hii tasnia ya Tekinohama(ICT) hakuna kinachofichika kwa watu wanaojua hivi vitu.
  Nakumbuka kuna jamaa mmoja aliwahi kutuma e-mail ya kumtukana Bosi wake ofisini kwa kutumia mtandao nje ya ofisi. Lakini baada ya uchunguzi wa kina ilikuja gundulika kuwa e-mail ile iliandaliwa kwenye computer yake na akaenda kuituma kwenye mtandao tofauti.

  Kumbuka kwamba computers zote maadamu zilizoko kwenye mtandao wa internet(world wide website-www)zinaweza kutambulikana na computer nyingine yoyote mahali popote duniani! Kama Mwigulu Nchemba alitumia mtandao wa computer au Smart phone yake yenye mtandao(internet)kujitumia SMS fake kwenye simu yake ili zionekane zimetoka kwa Mhe.Mnyika au Mhe.Mdee bado zinaweza kuwa traced back na zikaonekana zilitoka kwenye computer(L/top or D/top)gani au smartphone gani na ya nani. Hiyo ndiyo kazi ya TCRA,kufuatilia wanachokiita MALICIOUS CALL TRACING(MCT)AND ABUSIVE TXT MESSAGE TRACING.

  Yawezekana ikawa ngumu kupata namba za simu ya mtu aliyetuma SMS kutoka kwenye computer kwenda kwenye Mobile phone lakini bado upo uwezekano wa kugundua computer iliyotuma SMS hiyo.

  Let TCRA play their party it can be done!
   
 11. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #11
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280

  Kasimba G,

  Umesema kweli kabisa.

  Hili jamaa linafikiri kuwa lina akili nyingi sana kuzidi watu wote Bungeni,ndani ya CCM na Serikali yake. Hakika hili jamaa PR yake ni very poor au can say ni zero pc. Watu wanasema ukikuta mtu anapenda kujigamba/kujisifia ujue ni mtu mwenye inferiority complex au ana matatizo ya kisaikolojia na anahitaji counselling!Hii tabia ya kusimama na kudai yeye ni 1st class economist inatokana na vitu kama hivo! Ogopa sana mtu anayeogea huku akijisonta kidole kichwani au kifuani. Watu kama hao mara nyingi wako tayari KUUA au KUJIUA(Judas Iskariote type)!

  CCM wasipogundua udhaifu wa huyu jamaa na matatizo aliyonayo basi ataendelea kuibomoa na kuimegia CCM kidogodogo mpaka iishie kuzimu.
   
 12. agatony8l

  agatony8l JF-Expert Member

  #12
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Serikali ya CCM ipo bize kuhakikisha inajiongezea mapato kwa kupitia migongo ya wananchi wake, hii inatia doa kubwa sana serikali hii inayojiita sikivu. Kumbe inawasikiliza wawekezaji na mafisadi tu!!!!!!!
   
Loading...