GE2025 TCRA:Wanahabari msibebe umbea, hojini sera za vyama

GE2025 TCRA:Wanahabari msibebe umbea, hojini sera za vyama

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Meneja wa Huduma za Utangazaji katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi Andrew Kisaka, amewataka waandishi wa habari na watangazaji nchini kuzingatia sera za vyama vya siasa katika uripoti na mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa 2025, badala ya kuendesha mahojiano kwa misingi ya mambo binafsi au upendeleo wa kikabila na kidini.

Akizungumza katika Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Habari na Utangazaji Kanda ya Kaskazini uliofanyika tarehe 16 Agosti 2025 katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), mkoani Arusha, Kisaka amesema ni wajibu wa wanahabari kuhakikisha kila chama kinahojiwa kwa sera zake katika sekta muhimu kama elimu, afya na kilimo, ili kuwawezesha wananchi kulinganisha na kufanya maamuzi sahihi ya kisiasa.

"Katika uripoti wetu tuwe tunaripoti sera za vyama, usiripoti kitu kingine. Waacheni wanasiasa waeleze sera zao halafu wananchi wenyewe watalinganisha na kuona mahali sahihi. Mambo ya umbea hayana nafasi kwenye habari za uchaguzi," amesema Kisaka.

Aidha, Kisaka amekemea tabia ya baadhi ya watangazaji kuuliza maswali yasiyo na tija au kuendeleza mazungumzo yanayochochea ubaguzi wa kidini, kikabila, kijinsia au kimaeneo.

"Inatokea kwamba safari hii tumekuwa na desturi kwamba Rais akiwa Mkristo anayekuja ni Muislamu na wewe unang'ang'ana studio una- entertain hilo. Tumezoea kuwa Rais akiwa mwanamke sasa tuna zamu ya mwanaume, na mtu anakupeleka hukohuko na wewe mtangazaji unaona ni mahojiano mazuri kabisa?", amehoji.


Mkutano huo ulioandaliwa na TCRA kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), uliambatana na mafunzo maalum yanayolenga kuhakikisha uripoti wa Uchaguzi Mkuu wa 2025 unafuata kanuni, weledi na maadili ya kitaaluma.

Washiriki wa mkutano walijumuisha waandishi wa habari, watangazaji na maafisa waandamizi wa Jeshi la Polisi kutoka mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga na Manyara.

Chanzo: Jambo TV
 

Attachments

  • Screenshot_20250816-143223_Instagram.jpg
    Screenshot_20250816-143223_Instagram.jpg
    185.4 KB · Views: 13
Mnajua maana ya mwelekeo na matakwa ya soko/walaji??

Hii ngoma soko linataka left nenda left gentleman

Usisikilize miruzi mingi itakupoteza angalia soko linataka nini peleka sokoni
 
Back
Top Bottom