TCRA wanafanya kazi kwa upendeleo, wakati wakipiga mikwara wanaojiunga mubashara na vituo mbalimbali, wale wa CCM wanaachwa

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,500
3,478
Wakuu Salaam,

Nchi yetu Utawala wa Sheria wa Sheria Umeshrink Nchini Tanzania, Tunafuata Matanko ya Wanasiasa ndiyo yamegeuka kuwa Sheria.

Hivi karibuni MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilivitaka vituo vya redio, televisheni na wanaotoa huduma za maudhui mtandaoni kuomba kibali/ ruhusa ya kurusha mubashara matangazo ya vituo vya utangazaji vilivyoko nje ya nchi na vya ndani na pia viwasilishe makubaliano yao kwenye mamlaka hiyo ili kuleta ufanisi katika kusimamia maudhui yanayorushwa mubashara na vituo hivyo.

Lakini ajabu ni pale rais anapokuwa anaongea sehemu yoyote, wapo wanaojiunga wala hawasemwi wala kusumbuliwa kama Watu wengine.

Kitendo cha TCRA kuwaacha watu warushe live Mikutano ya CCM au Viongozi wa CCM, Lakini Wakirusha Mikutano ya Wapinzani au Habari yoyote inayokosoa Serikali Wanaaitwa na kupigwa faini kubwa, naona ni Upendeleo. Si Vizuri kwa Taasisi kubwa kama TCRA kuwa na double standard.

Lissu alipochukua Fomu ya Kugombea Urais Dodoma Watu hawakuonesha Live baada ya kutishwa kwamba ni kinyume cha Sheria.

Leo rais Magufuli ametembelea Kanisa la TAG Dodoma na Watu Wameruhusiwa Kurusha Matangazo ya rais Mubashara. Nataka kuona watafanywa nini.

Hii nchi ya Vyama vingi, watu wake wamegawanyika kwa Imani za kiitikadi japo Wanatii Sheria za Nchi, lakini huwezi kuwalazimisha kisa una Mamlaka kwamba iwe lazima kuonesha kile Unachopenda hasa kulazimisha vyombo vya habari kupendelea chama Tawala.

Sio Ustaarabu. Ngoja tuone Hawa walioazimishwa leo kurusha live Shughuli ya TAG kama watafanywa kitu.

Vituo vya utangazaji vyatakiwa kuomba kibali TCRA kurusha matangazo ya Vyombo vya Habari vya Nje

Uchaguzi 2020 - Lissu ailipua TCRA na Idara ya Habari Maelezo kwa kunyanyasa Vyombo vya Habari vinavyoripoti habari zake, aahidi kuifutilia mbali

Live.PNG
Live2.PNG
live3.PNG
 
Back
Top Bottom